Ijumaa, 28 Februari 2014

MWIGULU NCHEMBA ASEMA SERIKALI HAITAONGEZA POSHO KWA WABUNGE WA BUNGE LA KATIBA

Nchemba katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCm Ifunda


NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amewataka wabunge wa bunge maalumu la Katiba wanaotaka nyongeza ya posho kujiondoa katika bunge hilo kama hawaridhiki nayo.

“Ndio wachape mwendo; maana kuna wengine wanasema wana biashara zao zinawalipa zaidi ya Sh 300,000 zinazotolewa kwa siku na serikali, ni vizuri wakaenda kusimamia biashara zao,” alisema.

Akizindua kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Kalenga kwa kumnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM , Godfrey Mgimwa, Nchemba serikali haitawatendea haki watanzania kama itakubaliana na matakwa ya baadhi ya wabunge wanaotaka nyongeza ya posho.

 “Nimekataa, sitakubali serikali iongeze posho kwa kuzingatia sababu zilizotolewa na baadhi ya wabunge wanaotaka nyongeza hiyo.”

Alisema anajua kuwepo kwa kamati iliyokuwa ikilifanyia kazi suala hilo na mapendekezo yake kuyawasilisha kwa Rais Jakaya Kiwete.

“Rais ni mtu mwenye hekima na busara nyingi, amesikia kilio cha watanzania, anajua hali ya kiuchumi ya taifa hili, anajua mahitaji mengine mengi ya watanzania kwa kutumia rasilimali hizi hizi tulizonazo; ni lazima atatuomba ushauri sisi kama wasaidizi wake,” alisema.

Alisema posho wanayopewa wabunge hao inazingatia hali halisi ya nchi na kwamba hatakubali iongezwe.

Alisema badala ya kudai nyongeza ya posho, wabunge wanaoshiriki bunge hilo wanatakiwa kuonesha uzalendo kwa kujisifu kupata fursa hiyo muhimu ili wawakilishe watanzania wenzao kutengeneza sheria mama ya nchi.

“Ni mambo ya uzalendo; nakumbuka nikiwa mdogo kuna watu walisikitika kukosa fursa ya kwenda kupambana na Nduli Idd Amin wakati wavita ya Kagera, na wale waliokwenda walifuraji na kuonesha ushajaa wao pamoja na kwamba maisha yao yalikuwa hatarini,” alisema.

Alisema watu wanaotaka kuikomboa nchi yao wakitanguliza maslai yao mbele ni hatari kwa maendeleo ya Taifa.

Alisema wabunge wa bunge maalumu la Katiba hawajakodishwa, hawafanyi kazi kama washauri wataalamu, wanafanya kazi hiyo kwa niaba ya watanzania wengine wanaotaka kuona nchi inakuwa na Katiba Mpya.

Alisema wakati wabunge hao wakidai nyongeza ya posho wanasahau kwamba nchi hii ina mambo mengi yanahitaji fedha ili isonge mbele.

“Wanajua kwamba hatujalipa wakandarasi, wanajua kwamba walimu zaidi ya 36,000 wanaidai serikali na wanajua kwamba kuna baadhi ya watumishi wa serikali wanapata kwa mwezi chini ya kiwango wanacholipwa wao kwa siku,” alisema.

Alisema ili nchi ipate maendeleo ni lazima mambo yote ya msingi yaendelee kufanyika kwa kutumia rasilimali zilizopo.

“wanajua wananchi wanahitaji mbolea ya ruzuku, maji, barabara, umeme, huduma nzuri za afya, shule na mengine mengi” alisema.

Alisema wanaona kiasi hicho hakiwatoshi na wana matumizi zaidi ya Sh 300,000 kwa siku wakendelee na shughuli zinazowafanya wapate zaidi ya kiasi hicho.

Akimnadi Godfrey Mgimwa, Nchemba alikishangaa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuingia katika uchaguzi huo.

“Watanzania lazima waelewe dhana ya uchaguzi mdogo; uchaguzi huu hauendi kubadili serikali, serikali iliyopo ni ya CCM na inatekeleza Ilani yake,” alisema.

Alisema wananchi walikwishatoa ridhaa mwaka 2010 kwa kuchagua mbunge na madiwani wote wa CCM kwahiyo kinachofanyika katika uchaguzi huo ni kuziba nafasi.

“Haiwezekani mchezaji wa Simba akatolewa uwanjani akaingizwa wa yanga au wa Yanga akatolewa akaingizwa wa Simba; kwenye siasa hatuhitaji ushabiki, mpeni kura zenu mgombea wa CCM kwasababu yeye ndiye anayetekeleza Ilani ya CCM,” alisema.

Alisema CCM ina mkataba na wana Kalanga na imejipanga vyema kutekeleza Ilani yake kama ilivyoahidi wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Alisema hakuna litakalofanywa na mgombea wa Chadema katika kipindi kilichobaki kama atachaguliwa kuwa mbunge wao.

“Mkimchagua na mtakapomuuliza tena majibu yake yatakuwa yale yale, sijatekeleza ahadi zangu kwasababu serikali ya nchi hii imeundwa na CCM,” alisema. 
CREDIT; Bongo leaks 

MWIGULU ALIVYOZINDUA KWA KISHINDO KAMPENI ZA CCM KALENGA.

 Abdul Adam, Mtoto wa Spika wa Bunge wa zamani Chifu Adamu Sapi Mkwawa, akimpongeza mgombea wa CCM katika Uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, Godfrey Mgimwa, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
 Wananchi wakinyoosha mikono kuunga mkono kuwa mgombea wa CCM anafaa, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba akionyesha makada wa CCM,  Alphonce John (kushoto) na Musa Tesha, walionusurika kuuawa na watu wanaodaiwa kutumwa na Chadema kwa mmoja kumwagiwa tindikali na mwingine kutobolewa jicho kwenye kampeni zinazohusu udiwani na Ubunge, katika maeneo ya Igunga na Kahama, alipokuwa akieleza fuji za Chadema, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
  Alfonce aliyetobolewa jicho Kahama akizungumza jukwaani.
  Mwigulu akihutubia, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
 Mwigulu (4th) na mgombea wakitroti na Green Guard, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
 Katibu wa CCM, wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu, alionyesha mbao zenye misumari inayodaiwa kutegwa njiani na Chadema, kwa nia ya kudhuru msafara wa mgombea wa CCM ktk jimbo la Kalenga.
 Katibu wa CCM  mkoa wa Iringa, akishauriana jambo na Mwenyekiti wake Joyce Msavatavangu
 Mjumbe Kamati Kuu ya CCM, Pindi Chana,  akitema cheche jukwaani, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.

Godfrey Mgimwa-Mgombea wa CCM uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa.
Imetayarishwa na theNkoromo Blog

Alhamisi, 27 Februari 2014

MAMLAKA YA MAJI MBEYA YAZIDAI TAASISI ZA SERIKALI ZAIDI YA MILIONI 400

 Afisa Habari Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Jijini Mbeya, Neema Stantoni akizungumza na kalulunga blog ofisini kwake.
 Akifafanua jambo....

TAASISI za serikali mkoani Mbeya, zinaongoza kwa kukwepa kulipia huduma za maji, hivyo kukwamisha tija ya uboreshaji wa usambazaji wa maji kwa wananchi mkoani hapa.

Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Jijini Mbeya (MBEYA-UWSA) imesema imekuwa kwenye changamoto kubwa, ingawa taasisi hizo zimekuwa zikipewa fedha na serikali ya kulipia huduma hiyo.

Afisa habari wa Mamlaka hiyo, Neema Stantoni, ameeleza kuwa, taasisi hizo zinadaiwa kiasi cha Tsh. Mil. 466,899,942.

Alisema tayari mamlaka hiyo imeanza zoezi la kuwakatia maji wateja wote ambao wanadaiwa na kwamba wateja zaidi ya Elfu mbili wamekatiwa maji.

‘’Tunahudumia wateja wa aina Nne, wakiwemo wa majumbani, Viwandani, biashara na taasisi za serikali ambapo wateja wanaoongoza kulipa vizuri ni wateja wa viwandani ambao wanalipa kwa wakati’’ alisema Neema.

Kati ya taasisi ambazo zinadaiwa ni pamoja na maeneo ya Afya, Magereza na Polisi ambapo imeelezwa kuwa taasisi hizo zikikatiwa maji kunauwezekano wa kutokea milipuko ya magonjwa kikiwemo kipindupindu.

 Afisa habari huyo amezitaka taasisi za serikali kulipa deni hilo hata kwa kupunguza, vinginevyo zoezi la kukata maji linaweza kuzikumba.

‘’Kwasababu Mamlaka na wateja tunategemeana ambapo mteja akilipa anasaidia matengenezo ya mabomba yanayopasuka, kununua dawa za kutibu maji na kulipia umeme ambao unasaidia kusukuma mashine kisha wateja kupata maji’’ alisema Neema Stantoni.

Alizitaja changamoto zinazoikabili mamlaka hiyo kwa sasa kuwa ni pamoja na baadhi ya wateja kuiba maji kwa kuchepusha kabla ya mita, kubonda mita kwa lengo la kuiba maji na kutoa mita kisha kuchota maji.

Zoezi la kuwakatia maji wateja wote ambao hawajalipa kuanzia mwezi mmoja, amesema linaendelea nyumba kwa nyumba, wateja wa biashara yakiwemo mahotel kisha taasisi kwa taasisi.

TANZANIA PRISON KUWAWEKA ''RUMANDE'' MGAMBO

 Mashabiki a Mbeya City, wakiipokea kwa shangwe timu yao.

MASHABIKI wa timu ya Tanzania Prison, wamesema kuwa Mgambo kazi yao ni kufundisha mchakamchaka na wala siyo kucheza mpira, hivyo timu ya Mgambo, wajiandae kufungwa katika uga wa Sokoine.



Kocha wa timu ya kukuza vipaji ya Mbeya umoja Sports Academy, ambaye ni shabiki  wa timu ya Tanzania Prison, Peus Nsheka, aliyasema hayo jana ukumbi wa magereza, wakati wa hafla ya mapokezi ya timu hiyo mbele ya mkuu wa magereza mkoa wa Mbeya(RPO), Emmanuel Sanguti.



Wadau hao walikabidhi matunda na juice kwa wachezaji ambapo nahodha wa timu hiyo Lugano Mwangama, alipokea zawadi hizo kwa niaba ya wachezaji wenzake.



Shabiki mwingine, Christopher Nyenyembe, ambaye ni mwandishi wa habari, aliuambia uongozi wa timu hiyo kuwa, hawapaswi kubadilisha walimu kwasababu imeonesha kuwa walimu wazalendo wanao uwezo mkubwa wa kufundisha timu za Tanzania.



“Makocha kutoka nje ya nchi wanakula fedha za timu pasipo sababu yeyote. Fedha hizo zinapaswa kuimarisha timu badala ya kuwapa makocha hao kwasababu makocha wazalendo akiwemo Mwamwaja wanao uwezo mzuri’’ alisema Nyenyembe.



Mkuu wa Magereza mkoa wa Mbeya, aliwapongeza wachezaji, mashabiki, askari na vyombo vya habari kuifikisha timu hiyo hapo ilipo na kwamba mchezo uliooneshwa na timu hiyo kwenye uwanja wa Chamanzi wa Azam Jijini Dar es Salaam, inaonesha timu hiyo inao uwezo wa kufikia nafasi ya tatu bora.



“ Kila mechi iwe fainali, kama ilivyokuwa pale chamanzi, Azam waliomba mechi iishe haraka na hizi timu kubwa zina mambo yao, tulinyimwa penati zaidi ya tatu lakini tuliishusha kutoka kileleni’’ alisema Sanguti.



Mkuu wa gereza la Ruanda, SSP Ismail Misama, aliwaambia wachezaji wa timu hiyo kuwa hawapaswi kubweteka ili kufikia nafasi ya tatu bora na kwamba uwezo na nia kwa pamoja na umoja wa wadau ipo.


Naye mkuu wa chuo ambaye ni mlezi wa timu hiyo, Mashaka Soja na mhamasishaji SP Enock Lupyuto, walisema timu zilizobakiza mechi na timu hiyo zijiandae kisaikolojia.

Jumanne, 25 Februari 2014

TRA YAWATOA HOFU WAFANYABIASHARA JUU YA EFD



Na Kenneth Ngelesi, Mbeya

MAMLAKA ya mapato nchini TRA imewatoa hofu wafanyabishara kutumia mashine za EFD kwani kodi inakatwa asilimia 30 ya faida baada ya kutoa gharama zote za uendeshaji na manunuzi.


Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa juma na Afisa Mwandamizi Mkuu wa Elimu wa mamlaka ya Mapato nchini (TRA) makao Makuu Hamis Lepenza katika hotel ya Paridise jiji hapa katika Mkutano na waandishi kutoka vyombo mbalimbali ambao  uliyo itishwa na mamlaka hiyo kwa lengo la kuwataka wandishi wasaidie kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa mashine hizo.


Lupenza alisema kuwa hofu ya wafanyabiashara wengi kuto taka kutumia mashine hizo ni kuto kuwa tayari kukatwa asilimia hiyo ni kwamba wengi hawana elimu ya juu utumiaji wa mashine hizo.


Afisa huyo alisema kuwa wengi wao wamekuwa na malalamiko kuwa hawaja soma hivyo  kuwa nguma kwao kuzitumia miashine hizo jambo alilodai siyo la kweli bali ni janja ya wafanyabishara kwani wana hofia mashine hizo zitasababisha kuonyesha mauzo kuongezeka na kodi ya kulipa kuwa kubwa.


Aliongeza kuwa kutokana makato kuwa wazi katika ulipaji wa kodi ndiyo sabababu wafanyabiashara kutokuwa tayari kutuma mashine hizo.


Lepenzi alisema kuwa wafanyabishara wengi wamekuwa wakilala mika kuwa hawaja soma jambo hivyo uwezo wa kutumia msahine ni mgumu.


'Ndugu zangu huyu mfanyabishara anasema hajasoma hivyo hataweza kutumia mashine hizo lakini mtu huyo huyo unanunua simu nzuri kubwa na yenye mambo mengi kuliko hata hiyo mashine ya EFD' alisema Lupenza.


Aliongeza kuwa tatizo lingine lililopelekea zoezi kuwa gumu ni ugeni wa utamaduni wa kutumia mashine hizo katika jamii yetu na siyo kigezo cha elimu kama kinavyo tolewa na baadhi ya wafanyabishara walio wengi.


Katika hatau nyingine Afisa elimu na huduna ya mlipa kodi kutoka
makao Makao Makuu Sigsimund Kafuru aliwataka waandishi kusaidia kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhumu wa kudai risiti pindi wanapo nunua bidhaa kwani kutochukua risiti ni kuisosesha serikali mapato na hatimaye inashindwa kutoa huduma stahiki kwa wananchi wake.


Aidha Aliongeza kuwa ni vema wananchi wakajenga utamaduni wakudai risiti pindi wanapoa nunua bidhaa  yoyote ile.


Akijibu swali kwa waandishi habari sababu za kuteua makampuni kumi na moja tu kupewa jukuma na kusambaza mashine hizo kutokana na kushinda tenda baada ya kushindanisha kwa mujibu wa sheria ya manunuzi.


Tangu mwaka 2010 serikali kupitia kwa mamlaka ya mapato nchi iliwatka wafanyabisha kutoa risiti  kwa kumtumia mashine hizo kwa sawamu ya kwanza ikianza na wafanyabisha lakini 200,000/ lakini mpka sasa bado kumekuwa na mvutano mkubwa baini ya ya Serikali na wafanya bishara hao.


Hata hivyo  zoezi hilo bado lina leta mvutano mamlaka hiyo imesema kuwa ipo katika mchakato wa kuanza kutoa hudumnu ya risiti kwa kutumia mashine hizo kwenye magari makubwa na mabasi ya kusafirishia abiria.

Jumatatu, 24 Februari 2014

ZIJUE KATA 36 ZA JIJI LA MBEYA


Mlima Loleza uliojitokeza karibu na Mbeya Peak, ndio huonekana
kutokea Mbali pale unapoingia Mbeya Mjini.
 
 
Foresti • Ghana • Iduda • Iganjo • Iganzo • Igawilo
Ilemi • Ilomba • Isanga • Isyesye • Itagano • Itende • Itezi •
Itiji • Iwambi • Iyela • Iyunga • Iziwa • Kalobe • Maanga •
Mabatini • Maendeleo • Majengo • Mbalizi Road • Mwakibete •
Mwansekwa • Mwansanga • Nonde • Nsalaga • Nsoho • Nzovwe •
 

PRISON YAZOA MASHABIKI MBEYA, KUPOKELEWA KESHO KUTWA J5.


TIMU ya soka ya Tanzania Prison(wajelawajela) ya Jijini Mbeya, imeandaliwa mapokezi mazito baada ya mashabiki kuridhishwa na kiwango cha wachezaji wake.

Mapokezi hayo yatafanyika kesho kutwa Jumatano eneo la Oil Com Uyole Jijini hapa, huku mashabiki kadhaa wakifika katika ofisi za Jiji la Mbeya kuomba vibali vya kufungua matawi ya timu hiyo.

Mjumbe wa kamati tendaji ya timu hiyo Mohamed Lalika, amethibitisha kuwepo kwa mapokezi hayo na kwamba wanawakaribisha mashabiki wa timu zingine ambao waliasi.

‘’Kama ilivyo kauli mbiu yetu kuwa tumejipanga hatoki mtu, hivyo wale wote waliopotea wanaruhusiwa kurudi kushabikia timu yao halisi bila masharti yeyote’’ alisema Lalika.

Naye mwanachama wa Yanga Christopher Nyenyembe ambaye amesema kuwa ni shabiki  timu ya Prison, alisema timu hiyo ina umbo la timu.

‘’Mimi ni shabiki mkubwa wa timu ya Prison na nitaendelea kuwa shabiki kwasababu timu hiyo ina umbo la timu tofauti na timu ya Mbeya City ambayo wachezaji hawachezi kama timu bali kila mmoja anacheza kwa uwezo wake’’ anasema Nyenyembe.

Ayas Yusuph(Asia), mkazi wa Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini, alisema kuwa katika eneo la Mbalizi tayari wamefanya uchaguzi wa tawi la timu hiyo kwa lengo la ushindani.


Shabiki wa muda mrefu wa timu hiyo Jijini hapa, Herode Mdoe, alisema katika ligi kuu kuna timu Nne pekee ambazo zina mfumo wa timu ambazo ni Tanzania Prison, Mtibwa, Azam na Coast Union.


Aidha alichangia mfuko mmoja wa saruji kwa ajili ya ujenzi wa tawi la Mbeya Peack ambalo linaongozwa na Christopher Nyenyembe ambaye kitaaluma ni Mwandishi wa Habari.

Wakielezea mafanikio ya timu hiyo na juhudi zinazofanywa na uongozi wa Prison, shabiki Emmanuel Baganda(Swahida) na Adamu, alisema kuwa siri kubwa ni kutokana na Mwalimu David Mwamwaja kusikiliza ushauri kwa kila mtu bila dharau.
 
Credit;kalulunga blog

Jumamosi, 22 Februari 2014

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2013 KWA MKOA WA MBEYA BOFYA HAPA CHINI KUTAZAMA MATOKEO YA SHULE

ST. FRANCIS GIRLS SECONDARY SCHOOL
















































HOJA YA MWANAKIJIJI

Wapo wenye mapenzi na CCM, CDM isisahau hili!

KAMA nilivyodokeza wiki iliyopita naomba wiki hii niangalize jambo moja ambalo inaonekana kwa wale wapinzani na wengine wanaopenda mabadiliko ya kweli ya kisiasa wanaanza kulisahau; kuwa, wapo Watanzania wenye mapenzi kweli na Chama Cha Mapinduzi!
CDM kama chama kikuu cha upinzani nchini kinaonekana wakati mwingine kinajisahau katika hili na mara zote kinapofanya hivi kinajikuta kinashangazwa ama na matokeo ya kura au na mwitikio wa Wana CCM kutoka kwa viongozi wao.
Kosa kubwa sana la mtu kupendwa ni kudhani kuwa wewe peke yako ndiye unapendwa. Na wakati mwingine ukigundua kuwa na wengine wapo wanaopendwa unaweza kujisikia donge la kwanini na wao wanapendwa na hata unaweza usielewe kwanini na wao wanapendwa.
Watu wanapenda kwa sababu mbalimbali; wapo wenye kupenda kwa sababu za kihistoria, wengine wanapendwa kwa sababu ya vile wanavyofanyiwa na wale wanaowapenda au sababu nyingine mbalimbali.
Katika siasa ni hivyo hivyo; wapo watu wanapenda chama tawala kwa sababu mbalimbali na wengine wanapenda vyama vya upinzani.
Katika nchi yetu wapo watu wanaipenda CUF na wengine wanaipenda NCCR-Mageuzi; na wapo wenye kuipenda CDM kama vile wapo wenye kukipenda Chama Cha Mapinduzi.
Binafsi naamini makosa ya wapinzani – na hasa CDM – ni kufikiria (hata kwa mbali) kuwa hakuna watu wenye kuipenda CCM kwa dhati!
Wapo wenye sababu
Kuna watu watu wanaipenda kwa sababu mbalimbali; na sababu hizo zinatofautiana na ni nyingi kama idadi ya watu walionazo.
Wapo wenye kuipenda kwa sababu ya wazazi wao, wengine wanaipenda kwa sababu wana imani nayo, na wengine wanaipenda kwa sababu wanaona hakuna mbadala wake.
Na wengine wana sababu za ndani kabisa ya mioyo kiasi cha kuwa tayari kufanya lolote na vyovyote kuona kuwa CCM inaendelea kuwa madarakani.
Wapo wengine hawana sababu
Na wapo wengine ambao wanaipenda na ukiuwaliza sababu utaona hawana sababu zaidi ya kukubali tu kuwa “wanaipenda tu yaani”.
Huwezi kushangaa wengine wanaipenda kwa kuziona zile rangi tu za kijani na njano! Wengine wanaipenda kwa sababu rafiki zao, mashosti wao, au wenza wao wanaipenda!
Wapo wenye kuipenda kimkakati zaidi
Wengine wapo humo ndani na wanaipenda CCM kimkakati zaidi; wanaichukulia CCM kama ngalawa ambayo wanahitaji kuitumia kuwavusha wanakotaka kwenda.
Wanaweza wasikubaliane na sera zake, uongozi wake au hata kuchukia mfumo wake lakini kwa vile inawaahidi kuwapeleka sehemu basi wanavumilia na kuimba sifa zake!
Wengi wao hawa hujulikana wakati wa uchaguzi pale ambapo majina yao yasipopitishwa kugombea au wasipopata vile walivyodhani watapata kwa kubakia CCM.
Yanaweza kuwa ni mapenzi ya kinafiki lakini bado ni mapenzi kwani wakipata kile wanachokitaka utawaona hadi kwenye nyumba zao kuna bendera za CCM!
Wapo wanaoipenda kwa sababu wanaichukia CDM
Wapo wengine wanaipenda CCM na wanaichagua kila kukicha si kwa sababu nyingine, ila kuonyesha chuki na dharau yao dhidi ya CDM.
Hawa wanaipenda CCM kwa sababu hawawezi kuipenda CDM! Wanaweza kabisa kukubali mapungufu ya CCM, na wakakubali kuwa ina matatizo lukuki lakini watakuambia bila kupepesa macho kuwa “sijaona mbadala wa CCM” na wengine wanasema tu “siwezi kuipenda CDM”.
Mtu anaweza asielewe mantiki hiyo lakini ndani ya fikra za watu hao mawazo hayo yanaonekana kuwa na mantiki!
CDM ni lazima itambue jambo hili na inapofanya mikakati yake iliweke mawazoni. Kwamba, si watu wote wanaichukia CCM nchini na wapo ambao hata wakiitwa kuifia wataifia kuitetea!
Na hawa ambao wanaipenda CCM hivi ndio hawa hawa ambao watajiandikisha kupiga kura na wakati wa kupiga kura bila makeke wala mbwembwe wataenda na kuchagua wagombea wa CCM.
Hili ni muhimu kulifikiria ukiangalia matokeo mbalimbali ya uchaguzi. Katika mawazo ya kawaida unaweza kuamini kuwa katika Tanzania hakuna watu wenye kuipenda CCM kabisa.
Ukiangalia mikutano na hamasa ya CDM mijini na vijijini unaweza kuamini kabisa kuwa CDM inakubalika kila sehemu.
Ikifanyika mikutano ya kampeni unaweza kuamini kabisa kuwa kwenye eneo husika wapenzi wa CDM ni wengi kuliko wapenzi wa CCM. Lakini kura zinapokuja watu wanashangaa CCM wameshinda!
Ni rahisi kulaumu mfumo, kulaumu daftari la wapiga kura, au kulaumu matumizi ya vyombo vya dola. Ni kujaribu kuamini kuwa hivyo vyote visingekuwa vilivyo basi CDM wangeambulia kura zote na CCM isingeambulia hata moja.
Lakini ukweli ni kuwa hata daftari la wapiga kura likiboreshwa kila mwezi, hata polisi wakiwa huru bila upendeleo na mfumo ukawa wa haki kwa kiasi chote kinachowezekana bado utakuta kuwa wapo watu kwa maelfu bado wataipigia kura CCM!
Kwanini?
Kwa sababu binadamu si ng’ombe anayechungwa na kupelekwa kula anakotaka mchungaji na kupewa maji kwa jinsi anavyotaka mchungaji!
Mwanadamu ana uhuru wa kuamua kukubali au kukataa jambo hata kama jambo hili halina faida ya mara moja kwake.
Mwanadamu anaweza tu kushawishiwa katika siasa kufuata mrengo fulani au siasa za upande fulani lakini katika demokrasia hawezi kulazimishwa kukubali au kukataa siasa hizo.
Ni kwa msingi huo basi utaona kuwa CDM inaweza kujikuta kwenye matatizo ya mara kwa mara kudhania kuwa wote wanaokuja na kunyosha vidole viwili juu wakiimba “people’s power” ndio wana mapenzi!
Kuangalia picha za maelfu ya watu wakiangalia kwa matumaini wakishika vichwa kwa maombolezo na kufikiria kuwa wote hawa wanaiunga mkono CDM ni kujidanganya na kutokuielewa Saikolojia ya Siasa (Political Psychology).
Maandiko yanamnukuu Yesu akionya kuwa: “Si wote waniitao Bwana Bwana wataingia mbinguni”. Kwamba, wapo ambao hata watafanya miujiza na ishara lakini kumbe si wafuasi wake!
Hili ni kweli; wapo wenye kuvaa nguo za CDM, wenye kuimba na kusema lugha yote nzuri ya kiupinzani lakini wakati ukifika wanapiga kura zao kuichagua CCM.
Wale wenye kutaka mabadiliko na wapinzani kwa ujumla nchini tukitambua hili tutajipunguzia matumaini ya uongo na kuanza kupanga mikakati ambayo inalichukulia jambo hili kwa undani.
Mikakati ambayo itapangwa kuangalia ni jinsi gani tunaweza kuwashawishi watu wenye mapenzi na CCM kubadili upande. Maana kama tunaendelea kila kukicha kuwashawishi watu ambao tayari wameshashawishiwa tuna uhakika gani wa kufanya vizuri kama wale ambao wanatakiwa kushawishiwa hawajashawishiwa?
Jukumu na changamoto kubwa kwa CDM sasa hivi ni kutafuta njia ya kuweza kuwafikia wale ambao hawajaamua kuja kwenye upinzani na ambao bado wana imani na CCM.
Kama hawa hawajashawishiwa na mahubiri ya ufisadi, na hotuba za kina Lissu bungeni; kama watu hawajashawishiwa na hotuba kali za kina Mbowe na Slaa kwenye majukwaa ya kisiasa tangu 2010; hawa watashawishiwa na kitu gani?
Fikiria hakuna mahali popote ambapo umefanyika uchaguzi ambapo CDM ilishinda huku CCM ikipata kura sifuri! Kwani hata huko wapo masalia wa CCM!
Tukipata jibu la swali hili tutakuwa tumepata njia ya kuvuka kizingiti kikubwa zaidi cha kuweza kugeuza mwelekeo wa kura kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na ule wa rais.
Hivi sasa ukiangalia sana utaona kuwa CCM bado ina wapenzi wengi tu tena wale walioapa na kuahidi kabisa kuwa “Mapinduzi Nitakulinda Mpaka Kufa”! Kama wale waliofanya hivyo kwa CDM.

Jumamosi, 15 Februari 2014

TAMKO LA WADAU WA AFYA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA HAKI YA AFYA NA RASIMU YA KATIBA MPYA

Kwanza tunapenda kuipongeza Tume ya Katiba kwa kazi kubwa waliyofanya katika kukusanya maoni na kuandaa rasimu ya pili ya Katiba na vilevile kwa kugusia Afya katika Haki za binadamu kwa baadhi ya makundi kama vile katika Haki ya wanawake Ibara ya (47) kifungu cha 1(g) mwanamke ana haki ya kupata huduma bora ya Afya, katika Haki ya watoto Ibara (43) kifungu cha (1)e kinachosema mtoto ana haki ya kupata lishe bora, huduma ya Afya, makazi na mazingira yanayomjenga kimaadili.


Hata hivyo, tunasikitika kwamba Haki ya Afya haijatambuliwa kwenye rasimu kama haki ya Msingi ya kila mwananchi. Tukiwa kama wadau wa Afya, tunapenda kufafanua kuwa Afya ni kuwa mzima kiakili, kimwili, kijamii, kimaadili na kimazingira, hivyo Afya ni haki ya msingi ya kila mwananchi. Mwananchi anapokosa haki hii ya msingi hushindwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za kuleta maendeleo, na kupata madhara mengine yanayoweza kusababisha kifo.


Katika rasimu ya pili ya Katiba iliyokabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kujadiliwa katika Bunge la Katiba Februari 2014, Afya kama Haki ya msingi ya binadamu haijatambuliwa kama vile haki zingine zilivyotambuliwa kwa mfano elimu.


Tunatambua kwamba Katiba ndiyo sheria Mama, hivyo basi, pasipo kutambua Haki ya Afya, sheria ndogondogo haziwezi kulitambua suala hili nyeti, na hivyo kuiweka jamii na vizazi vijavyo katika hali hatarishi kiafya.

Juni 2013, Sikika iliomba na hatimaye ikapata kibali rasmi kutoka Tume ya mabadiliko ya Katiba cha kutambuliwa kama Baraza la Katiba kwa ajili ya kuchambua na kukusanya maoni juu ya Rasimu ya Katiba. 

Sikika ilishirikisha wananchi na Asasi mbalimbali kama Tanzania Public Health Association (TPHA), Medical Association of Tanzania (MAT) na Kituo cha Sheria  na Haki za Binadamu (LHRC) katika kuchambua rasimu ya kwanza ya Katiba na hatimaye kutoa mapendekezo ya kutambua haki ya afya kwenye Katiba.  

Mapendekezo hayo yaliwakilishwa kwa Tume Agosti 2013 lakini hayakuchukuliwa, kwa sababu moja au nyingine.


Kutokana na umuhimu wa Afya kwa kila mwanadamu, tunapendekeza Afya itambulike kama Haki ya msingi katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na iwe ni wajibu wa kila mwananchi kutunza Afya yake, kushiriki na kusimamia masuala yanayohusu afya ya jamii. Pia serikali ya Jamhuri ya Muungano, mamlaka  za  nchi pamoja  na  taasisi zihakikishe  kuwa Haki hii ya msingi inasimamiwa vyema.  

Pia itambuliwe kuwa ni kosa la jinai kwa mwananchi kufanya tendo lolote linalohatarisha afya ya mtu mwingine na jamii kwa ujumla.


Pia tunaomba serikali na wadau wa Katiba waangalie na kutambua Afya kama suala la msingi linalotakiwa lizingatiwe katika sera zote za maendeleo ili kuweza kulinda afya ya Watanzania wote.


Aidha, tunapendekeza ibara ya 41 inayozungumzia uhuru na haki ya mazingira safi na salama iongeze masuala haya; 

(1) Serikali ihakikishe kuwa kila mwekezaji afanye tathmini ya kiafya kabla mradi haujaanza na utekelezaji wa mapendekezo ushirikishe wadau wote hususan, ngazi ya jamii. 

(2) Serikali na vyombo husika vidhibiti uingizwaji na utumiaji wa vifaa/vyakula/madawa vyenye viwango duni na pia kutoruhusu matumizi ya madawa au vyakula bila ya ushahidi wa kitafiti unaothibitisha usalama wa mtumiaji/mlaji.  

Kutompatia mwananchi haki ya afya ni sawa na kumnyima haki ya kuishi kama ilivyoainishwa katika ibara 24 ya rasimu ya Katiba, maana uhai wa mtu unategemea afya aliyo nayo.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...