Jumatatu, 29 Desemba 2014

NAWATAKIA MAANDALIZI MEMA YA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2015

SAMBAZA TAARIFA 2015

ZIARA YA MABALOZI WA TANZANIA, UHURU PEAK

 Mabalozi wakiwa katika Mwamba wa Pundamilia “Zebra Rock” katika safari ya kuelekea Kilele cha Uhuru (Uhuru Peak).

(Picha zote na Charles Ndagulla)

Mlima Kilimanjaro (Tanzania) una vilele vitatu, Kibo, Mawenzi na Shira. Mlima huu umepewa heshima na kuingizwa katika maajabu saba hapa ulimwenguni hasa ikizingatiwa ni mlima uliosimama pekee yake bila kuungwa kwenye safu za milima kama ilivyo Everest (Asia) kwenye mapangano ya milima ya Himalaya, Drakensburg kwenye safu za milima ya Drakensburg (Afrika Kusini).


Mlima huu una urefu wa meta 5,895 sawa na futi 19,341 kutoka usawa wa bahari (a.s.l).
Ndagulla Blog inaufunga mwaka 2014 ikiwa na rekodi ya kuupanda mlima huo.
Tukio hili la kuupanda mlima lilianza Desemba 16 hadi 21 kupitia geti la Marangu hadi kilele cha Uhuru (Uhuru Peak).
Mandhari nzuri katika safari hiyo kunadhihirisha na namna gani mlima huu ulistahili kupewa heshima.
Katika safari hiyo Ndagulla blog iliongoza na Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi akiwemo Batlida Buriani anayeiwakilisha Tanzania nchini Kenya.
Balozi Lazia Msuya, anayeiwakilisha Tanzania huko Bondeni kwa Madiba alikuwepo katika safari hiyo ngumu.
Mabalozi wengine
Na.
Jina la Balozi
Nchi anayowakilisha
1
Dkt. Batlida Buriani
Kenya
2
Radhia Msuya
Afrika Kusini & Swaziland
3
Adadi Rajabu
Zimbabwe & Maritius
4
Dkt. Ladislaus Komba
Uganda
5
Mbarouk N. Mbarouk
UAE
6
Dkt. Aziz P. Mlima
Malaysia
7
Dkt. Bernard Achilwa
8
Shamimu Nyanduga
Msumbiji & Madagascar
9
Grace Mwijuma
Zambia
10
Patrick TSere
Malawi
11
Ramadhan Mwinyi
UN
12
Mbelwa Kairuki
Mkurugenzi wa Asia
13
Celestine Mushi
Mkurugenzi Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya nje
14
Daniel Ole Njoolay
Nigeria
15
Joseph Sokoine
Mkurugenzi Idara ya Amerika na Ulaya
16
John Kijazi
17
Charles A. Sanga
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii
Hebu Tazama mtiririko mzima wa safari hiyo.

Ijumaa, 19 Desemba 2014

MATUKIO TOFAUTI YA MBUNGE, DR.MARY MWANJELWA, ZIARANI MBARALI MBEYA NA KUPIGA KURA SERIKALI ZA MITAA

 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akivishwa skafu na vijana wa uvccm wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya jana, alipofika wilayani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi.
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akipiga kura wakati wa kuchagua viongozi wa serikali za mitaa Jijini Mbeya tarehe 14/12/2014.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa,(kushoto), akiwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya, Amani Kajuna, walipokutana katika vikao vya Chama Cha Mapinduzi(CCM), ofisi za mkoa wa Mbeya.

Alhamisi, 18 Desemba 2014

KAGERA KUJIVUNIA UWANJA WA NDEGE WA KISASA


Na Saidi Mkabakuli, Kagera
Mkoa wa Kagera na maeneo ya jirani wataanza kujivunia uwanja wa ndege wa kisasa kufuatia kukamilika kwa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.
Akizungumza na Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo toka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kagera, Mhandisi Suleiman Athuman, amesema kwamba maendeleo ya ujenzi wa jengo la abiria la kiwanja hicho upo kwenye hali nzuri na mkandarasi atabidhi kazi hiyo mapema mwakani.
“Katika mwaka wa fedha wa 2013/14 kazi zilizopangwa ni ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kiwanja, ikijumuisha barabara ya kuruka na kutua ndege, maegesho ya ndege, barabara ya kiungio, kwa sasa ujenzi unaendelea vizuri na Mkandarasi atatukabidhi kazi mapema mwakani,” alisema Mhandisi Athuman.
Akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Kiwanja cha Bukoba, Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa kiwanja hiko, Mhandisi Pius Gobolo amesema kuwa kazi za usimikaji wa mfumo wa taa za kuongozea ndege, ujenzi wa jengo jipya la abiria na uzio wa usalama zimeshakamilika kwa asilimia 80.
“Kama unavyojionea, sehemu kubwa ya kazi imekamilika, kwa makadirio ni zaidi ya asilimia 80 ya ujenzi wa kiwanja hiki imeshakamilika,” aliongeza   Mhandisi Gobolo.
Kwa mujibu wa mpangokazi wa ujenzi wa kiwanja hicho hadi kufikia mwezi Juni 2014, hatua iliyofikiwa ni pamoja na kukamilika kwa ukarabati wa barabara ya kuruka na kutua ndege, barabara ya kiungio na maegesho ya ndege kwa kiwango cha lami; na ujenzi wa jingo jipya la abiria kufikia hatua ya usimikaji wa paa na mifumo ya maji safi, maji taka na umeme; na kuendelea kwa ujenzi wa jengo la abiria na kituo cha umeme.
Naye, Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri amesema kuwa Serikali imeazimia kuendelea kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege hususan miradi iliyoibuliwa katika Programu ya Matokeo Makubwa Sasa.
“Kwa mujibu Programu ya Matokeo Makubwa Sasa, serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini ipo kwenye mkakati wa kuuendeleza viwanja vya ndege vyote ili viwe na kiwango kizuri kwa watumiaji wa viwanja hivyo,” alisema Bibi Mwanri.

Jumatano, 10 Desemba 2014

Wadai walifungwa kizazi na serikali Kenya

Baadhi ya wanawake wanaodai kuwa walifungwa kizazi kwa lazima kutokana na hali yao ya HIV.
 
 
Kikundi cha wanawake wenye virusi vya HIV nchini Kenya, kimewasilisha kesi mahakamani dhidi ya serikali kikiituhumu kwa kuwapangaia wafungwe kizazi kwa lazima kutokana na hali yao ya HIV.


Kwa mara ya kwanza katika historia ya kenya, kundi la kina mama ambalo lilikuwa limepokea kile serikali inadai kuwa msaada na ushauri wa afya, limejitokeza na kuwasilisha keshi mahakamani dhidi ya serikali, ikidai kuwa wao walishurutishwa kufunga uzazi na wengine baadhi yao wakifanyiwa upasuaji huo hata bila ufahamu wao.


Akina mama hao ambao wanaishi na virusi vya HIV wanasema mpango huo unaoendeshwa na serikali kupitia wizara ya afya na mashirika mengine unakiuka katiba ya nchi na sasa wanataka kulipwa fidia na pia serikali kuharamisha mpango huo mbali na kuweka sera mpya kuhusu mpango wa kufunga uzazi.


Allan Malechi, ambaye ni wakili wao, anasema kuwa idadi ya wanawake hao waliofanyiwa upasuaji wa kufunga uzazi bila idhini yao huenda ikaongezeka zaidi kwa kuwa kuna ripoti kuwa mradi huo unaendelea katika sehemu zingine.
Wanawake hao wanataka serikali iwalipe fidia kwa oparesheni walizofanyiwa kinyume na matakwa yao.
Mashirika ya kutetea haki za kijamii pia yalijiunga na kina mama hao kwa maandamano ya amani mjini Nairobi.


Wakiwa wamevalia mavazi yenya maandishi , ''koma mpango wa kulazimisha kina mama wanaoishi na virusi vya ukimwi, kufunga uzazi, '' wanaharakati hao wamesema kuwa mradi huo ni sawa na ukatili wa kibinadam na kutaka serikali kuptia kwa wizara ya afya kutoa taarifa rasmi.


Inviolata Mwali ni mshirikishi wa kimataifa wa shirika la wanawake wanaoishi na virusi vya ukimwi Kenya.
Wanawake hao wanataka kulipwa fidia na serikali pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyowafanyia operesheni hizo.

Pia wametoa wito kwa serikali operesheni kama hizo zikomeshwe.
Kesi kama hizi zimewahi kuwasilishwa mahakamani katika mataifa kadhaa ya Afrika.


Mahakama nchini Botswana mnamo mwaka 2012, iliamua kuwa wanawake watatu wanaoishi na virusi vya HIV waliofungwa kizazi kwa kulazimishwa walipwe fidia na serikali.

Chanzo;BBC SWAHILI

WEKA NA USHINDE

WEKA NA USHINDE.

Kampeni kambabe yenye zawadi zenye thamani zaidi ya Milion 500!

Wateja kushinda Bajaj, Bodaboda na Baiskeli.
NMB  Tanzania

NMB Tanzania

Bank/Financial Institution

KONGAMANO LA SIKU MBILI LA UKATILI WA JINSIA DHIDI YA WANAWAKE NA WALEMAVU LILILOANDALIWA NA SHIRIKA LA SEED TRUST LAFIKIA TAMATI MKOANI MOROGORO DESEMBA 9-2014

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Seed Trust, Margareth Mkanga (MB) akizungumza katika kongamano hilo. Kulia ni Mwenyekiti wa Shirika hilo, Stephen Mashishanga. Kongamano hilo la Majadiliano kuhusiana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na walemavu limeshirikisha wadau mbalimbali kutoka baadhi ya mikoa ya Tanzania na kuandaliwa na Shirika la Seed Trust la mjini Morogoro kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA).
Mwenyekiti wa Shirika hilo, Stephen Mashishanga, akichangia mada katika kongamano hilo.
Dk.Ernest Rugiga akitoa mada kuhusu afya ya uzazi.
Mwezeshaji Victor Mulimila akizungumzia kwa ujumla kuhusu vitendo vya ukatili. Kulia ni Dk.Ernest Rugiga
Ofisa Tarafa wa Manispaa ya Morogoro, Mlange Pakalapakala Jumamosi, akichangia mada kwenye kongamano hilo.
Wanahabari walikuwepo kwenye kongamano hilo wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi. wa Bwalo la JKT mkoani humo.

MAGAZETI LEO JUMATANO TAREHE 10/12/2014 NCHINI TANZANIA

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...