Jumatatu, 30 Juni 2014

KANDORO AKANA SERIKALI KUTOZA USHURU ''VITENDANISHI'' VYA DAWA ZA KULEYA

 Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, akijibu maswali ya waandishi wa habari, kabla ya kuazimishwa kwa siku ya kupiga vita dawa za kulevya duniani mwaka huu 2014.
 Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akisoma taarifa ya ujio wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Mohamed Bilal, mkoani Mbeya, ambapo alikuwa mgeni rasmi katika kilele cha siku ya kupiga vita dawa za kulevya.
  Baadhi ya waandishi wa habari waliokuwepo ofisini kwa mkuu wa mkoa wa Mbeya siku hiyo.
 
MKUU wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, amekana serikali kutoza ushuru vitendanishi vya dawa za kulevya hapa nchini.

Kandoro alisema serikali haihusiki kutoza ushuru vitu vinavyotumika kuvutia dawa za kulevya, bali watumiaji wanageuza matumizi sahihi ya vitendanishi hivyo.

Jibu hilo alilitoa ofisini kwake Juni 24, mwaka huu, alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari ambao waliuliza kuwa karatasi aina ya Rizila, ambazo kwa sasa zinatumika kusokotea bangi, serikali inachukua ushuru, hivyo je serikali haioni kuwa inachochea matumizi ya bangi?

Kabla hajajibu swali hilo, alilirejesha swali hilo kwa waandishi hao kama wanajua lengo la karatasi hizo ambazo zinatozwa ushuru. 

Baadhi walijibu kuwa karatasi hizo zimetengenezwa kwa ajili ya matumizi ya kusokotea tumbaku.

Ijumaa, 27 Juni 2014

VIONGOZI WA SERIKALI MBEYA WAKUTANA KUJADILI UBORESHAJI WA BIMA YA AFYA YA JAMII




 Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, Charles Kajege, akizungumza neno mbele ya viongozi waliokuwa wamehudhuria, wakiwemo wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Mbeya.
 Baadhi ya wenyeviti wa Halmashauri za mkoa wa Mbeya, wakisikiliza.
 Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, Charles Kajege.
 Wakuu wa wilaya za Ileje na Kyela mkoani Mbeya, wakisikiliza na kufurahia...
 Mkuu wa wilaya ya Rungwe, akifurahia jambo baada ya kutaniwa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, ambaye aliuwa mgeni rasmi.
 Wakuu wa wilaya za Mbarali na Mbozi.
 Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Dr. Norman Sigalla.
 Picha ya pamoja kati ya viongozi wa Bima ya Afya, Mkuu wa mkoa wa Mbeya na wakuu wa wilaya za Mbeya. Kisha zikafuata picha zingine za pamoja.



 Meneja wa NHIF Mkoa wa Mbeya, Dr. Mohamed Kilolile(kushoto), wakiwa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro baada ya kufungua mkutano huo.
 Baadhi ya waganga wakuu wa Hospitali za wilaya za mkoa wa Mbeya.
 Meneja Matekelezo wa NHIF makao makuu, Grace Lobulu, ambaye alimwakilisha Naibu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, akitoa mada.
 Afisa wa NHIF Mbeya.
  Meneja wa NHIF Mkoa wa Mbeya, Dr. Mohamed Kilolile, akizungumza jambo katika mkutano wa CHF kwa viongozi wa mkoa wa Mbeya wakiwemo Wakuu wa wilaya za Mbeya, Wakurugenzi, waganga wakuu, Wenyeviti wa Halmashauri na wenyeviti wa bodi za afya za halmashauri, ulioandaliwa na Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa,  (NHIF).
 
 Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, akifungua mkutano wa CHF kwa viongozi wa mkoa wa Mbeya wakiwemo Wakuu wa wilaya za Mbeya, Wakurugenzi, waganga wakuu, Wenyeviti wa Halmashauri na wenyeviti wa bodi za afya za halmashauri, ulioandaliwa na Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa,  (NHIF).
Mkutano wa CHF kwa viongozi wa mkoa wa Mbeya wakiwemo Wakuu wa wilaya za Mbeya, Wakurugenzi, waganga wakuu, Wenyeviti wa Halmashauri na wenyeviti wa bodi za afya za halmashauri, umefanyika jana katika hospitali ya mkoa wa Mbeya, kwa maandalizi ya Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa,  (NHIF).
Imebainika kuwa, mfuko wa KfW, alisema ni mradi mzuri ambao unalenga kupunguza vifo vya mama na mtoto ili kutekeleza malengo ya milenia kufikia mwaka 2015 na kwamba tayari kwa mkoa wa Mbeya, wanawake 70,000 wamejiunga.
Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, Charles Kajege, alisema lengo la mkutano huo na viongozi hao, ni kuhakikisha viongozi hasa wakuu wa wilaya kupanga mipango ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma zkiwemo dawa kwa wanachama wa CHF.
“Fedha zipo nyingi kwenye mfuko wetu kwa ajili ya dawa na vifaa tiba, leteni maombi ya mahitaji, tutawapeni ili wananchi wapate huduma’’ alisema Kajege.
Meneja Matekelezo wa NHIF makao makuu, Grace Lobulu, ambaye alimwakilisha Naibu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, alisema kuwa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ulianza rasmi jukumu la kusimamia mfuko wa Afya ya Jamii(CHF), Kitaifa mwezi Julai 2009.
Meneja wa NHIF Mkoa wa Mbeya, Dr. Mohamed Kilolile, alizitaja sababu za kuanzishwa kwa CHF kuwa ni Kushirikisha jamii kutoa mawazo yao ili kuboresha huduma za afya kupitia mikutano na kamati mbalimbali watakazozichagua wao wenyewe.
“Kuiwezesha jamii kumiliki hudum za Afya zinazowahusu katika maeneo wanayoishi na kuboresha huduma za matibabu kupitia utaratibu rahisi na nafuu wa uchangiaji kwenye mifuko ya bima ya jamii’’ alisema Dr. Kilolile.

Alhamisi, 26 Juni 2014

WAZAZI LUBALA SEKONDARI, WANAVYOLIPA KUNI NA MBOGA KAMA ADA

 
SHULE ya sekondari Lubala iliyopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya, ni shule inayomilikiwa na Mbujah Brothers Association nan i moja kati ya shule zinazofanya vizuri kitaalum yakiwemo masomo ya Sayansi.
 
Kuwepo kwa shule hiyo katika eneo la kitongozji cha Lubala, Kijiji cha Lukata, kata ya Kinyala, Tarafa ya Ukukwe, kumesaidia kupatikana na kupanuka kwa miundombinu ya maji na umeme katika eneo hilo.
 
Wanakijiji pia wamepata ajira ndogondogo kama vile vibarua, wajenzi, wapishi na walinzi.
 
Mbali na faida hizo, pia wanafunzi walio jirani na shule hiyo wanapewa nafasi za kufundshwa bure nyakati za usiku na Jumamosi na walimu wa shule hiyo ili kukuza mahusiano na taaluma.
 
Wanafunzi wa shule hiyo, wanasema hakuna masomo mepesi kama ya sayansi kutokana na masomo hayo kuwa na hisia za viumbe hai.
 
Wanafunzi waliokutwa katika maabara ya somo la Biolojia shuleni hapo, waliliambia gazeti hili kuwa tangu waanze masomo katika shule hiyo, wamehamasika kusoma masomo hayo kutokana na shule hiyo kuwa na maabara na vifaa vya kutosha.
 
Mwanafunzi wa kidato cha pili, William Kulwa(15), anasema alifaulu kujiunga na kidato cha kwanza shule ya serikali ya Tukuyu Day, lakini wazazi wake wakampeleka katika shule hiyo ambapo malengo yake kwa baadae ni kuwa Daktari wa binadamu.
 
“Natarajia kuwa Daktari maaana masomo ninayosoma ya sayansi yana hisia za binadamu na viumbe hai jinsi wanavyoishi, ingawa somo la Fizikia bado linanisumbua kidogo’’ alisema mwanafunzi William.
 
Happy John(15) wa kidato cha pili, anasema kuwa anatarajia kuwa Injinia baada ya kuhitimu masomo yake hapo baadae.
 
Katika hafla fupi ya maazimisho ya miaka kumi ya mafanikio ya shule hiyo yaliyofanyika shuleni hapo mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu, Mkurugenzi wa shule ambaye pia ni mkuu wa shule, Noah Mwasiposya, anasema shule hiyo imepata mafanikio makubwa kutokana na kuhamasisha kwa vitendo masomo ya sayansi.
 
“Mwaka 2004, tulianza na wanafunzi 215 na sasa tuna wanafunzi 1031 huku tukizidi kuimarisha taaluma, majengo na mazingira na tunaishukuru Hospitali ya Igogwe iliyopo karibu nasi, kwa ajili ya matibabu ya watumishi na wanafunzi’’ alisema Mkuu wa shule hiyo.
 
Kwa upande wake, Mwalimu Paison Mwalinga, anasema hamasa wanayoitia kwa wanafunzi kupenda masomo ya sayansi katika shule hiyo kwa vitendo, ndiyo nguzo moja wapo ya wanafunzi wao kupenda masomo hayo.
 
“Tunahamasisha vijana wengi kupenda masomo ya sayansi kwa kuwa na stream mbili za sayansi na kila mwaka zaidi ya vijana 60 wanajikita katika masomo hayo. Wanafunzi wengi wapo katika vyuo vya uuguzi na sekondari kidato cha tano na sita’’ alisema Mwakalinga.
 
Mwalimu Peter Nkanje, alisema mbali na mafanikio ya shule hiyo ya Lubala, changamoto wanayopata ni pamoja na kupata taarifa za wanafunzi wao wa kidato cha Nne wanaohitimu hapo na kujiunga na shule za sekondari katika masomo ya sayansi ambao wanashindwa kufaulu vizuri kutokana na shule wanazoenda kutokuwa na mazoezi ya mara kwa mara tofauti na shule yao.
 
Anasema mafanikio ya shule hiyo haiwezi kukamilika bila kuwataja baadhi ya watumishi wa shule hiyo ambao wapo zaidi ya miaka tisa tangu kuanzishwa shule hiyo.
 
Anawataja Noah Mwasiposya, yeye menyewe Peter Nkanje, John Charles Ngullah, Paison Mwakalinga, Yonathan Yaunde, Isaack Jonas na Maiko Maganga.
 
Wengine ni wafanyakazi wasio walimu ambao ni Alimundu Pasukali, Getruda Michael, Matrida Tosigwe, Rose Mwangamilo, Tumaini Samboma, Lucia Kabuje na Upendo Sambo.
 
Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo, Dr. John Mwakatage, anasema ni vema wazazi wa wanafunzi wanaohitimu katika shule hiyo kidato cha Nne na kufaulu, wakawabakiza watoto wao ili waendelee na kidato cha tano na sita hap badala ya kuwapeleka kwenye shule za serikali.
 
Anataja sababu kubwa ya hoja yake hiyo kuwa ni shule nyingi za serikali kumejaa migogoro mingi kati ya walimu na serikali na migomo ya mara kwa mara inayosababisha athari kubwa kwa wanafunzi.
 
“Mzumbe na nyingine zilikuwa shule nzuri, kwasasa wote tunashuhudia ilivyo, mwacheni mfugaji aendelee kulelewa na mfugaji aliyemzoea’’ anasema Mwenyekiti huyo wa bodi.
 
Afisa elimu Sekondari wa Halmashauri ya Rungwe, Anna Chigulu, anasema kuwa tangu utumishi wake, hajawahi kuona shule inayozawadia wanafunzi waliohitimu na kufaulu kama inavyofanya shule hiyo ya Lubala.
 
Mbali na mshangao huo, pia aliitaja shule hiyo kuwa ya mfano katika mkoa wa Mbeya kama siyo nchi nzima kwa ujumla, kutokana na uogozi kuruhusu wazazi maskini wa kipato cha fedha, kupeleka kuni ama mazao, kisha kuthaminishwa kuwa ada ya mwanafunzi.
 
“Wilaya ya Rungwe kwa mkoa wa Mbeya, tumeweza kuwa vinara wa matokeo makubwa sasa(BRN), shule ya Lubala imetupandisha chati’’ alisema Afisa elimu huyo.

Jumanne, 24 Juni 2014

ASKOFU MWAIJANDE AFARIKI DUNIA. NI WA JIMBO LA MBEYA

ALIYEKUWA  Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship Jimbo la Mbeya, Kingdom Mwaijande,(pichani), amefariki dunia nchini Afrika Kusini alikokwenda kupatiwa matibabu baada ya kuishi na kufanya kazi ya Kuhubiri Injili, kwa zaidi ya miaka saba baada ya kuvamiwa na majambazi.

Mwili wa Askofu huyo, unatarajiwa kufika katika uwanja wa ndege wa Songwe mkoani Mbeya kesho Jumatano Tarehe 25,06,2014 kwa usafiri wa ndege na kwenda kuuhifadhi wilayani Rungwe.

Tunatoa pole kwa kanisa zima la FGBF, wananchi na familia ya askofu Mwaijande.

Mungu alitoa na sasa ametwaa, jina lake libarikiwe.

SIKU YA KUPIGA VITA DAWA ZA KULEVYA KUFANYIKA MBEYA KESHO KUTWA TAREHE 26/06/2014

MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO.

Kutokana na mkoa wa Mbeya kuwa ni moja ya mikoa hapa nchini yenye milango ya kupitisha dawa hizo na pombe zinazoitwa haramu(viroba), Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, alisema Mkoa wake umepata bahati ya kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya kitaifa.

Aliitaja siku hiyo kuwa ni kesho kutwa June 26, mwaka huu na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais, Dr. Mohmed Gharib Bilal na shughuli zote zimeanza katika viwanja vya Ruanda Nzovwe Jijini Mbeya tangu leo Juni 24, mwaka huu.

Alitaja lengo la maadhimisho hayo kuwa ni kuiasa na kuikumbusha jamii juu ya athari za utumiaji wa madawa ya kulevya na pia kuihamasisha jamii kuachana na matumizi ya dawa hizo.

“Maonyesho yatakuwa na lengo la kutoa elimu ya jinsi ya kuzuia uingiaji wa dawa hizo, kupima waathirika na kutoa tiba kwa waathirika na taasisi zaidi ya 10 zitashiriki zikiwemo TFDA, Mkemia Mkuu wa serikali, Hospitali ya mkoa wa Mbeya, Rufaa, Ofisi ya kamanda wa polisi na NGO’s’’ alisema Kandoro.

Sanjari na hayo, alisema mkoa wa Mbeya unazalisha bangi, jambo ambalo serikali imeendelea kupambana nalo kwa kushirikiana na serikali za mitaa na vijiji ili kufichua wanaolima zao hilo.
 
 
*Tani 2.5 zanaswa


Wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya nchini, wamekamatwa huku wengine wakiendelea kusakwa.

Akieleza mbele ya waandishi wa habari, mchambuzi mkuu wa tume ya kudhibiti dawa za kulevya nchini, January Ntisi, alisema kuwa wafanyabiashara hao tayari wamefikishwa kwenye vyombo vya sheria.

“Kwa muda wa miezi sita tayari dawa za kulevya tani 2.5 zimekamatwa katika baadhi ya njia kuu ikiwemo bahari ya Hindi, bandari ya Dar es Salaam na wanaendelea kukamatwa’’ alisema Ntisi.

Mbali na jitihada hizo za serikali kudhibiti dawa hizo za kulevya hapa nchini, alisema kuna kazi ngumu ya kupambana na vigogo hao ambao alikiri kuwa mtandao wao ni mkubwa na wana uwezo wa kununua hata boti ziendazo kasi na manohari, lakini vyombo vingi vinaendelea kushughulika nao.

Kiongozi huyo, alilazimika kueleza jambo hilo baada ya kuulizwa kama tume yake inashindwa kutokomeza tatizo hilo nchini ili kuendelea kulinda ajira zao kwasababu wakitokomeza, kitengo hicho kinaweza kufutwa.

Ofisa kutoka kitengo cha mkemia mkuu wa serikali, Grolia Omary, alisema ofisi yake inafanya kazi kwa uadilifu mkubwa, hivyo tatizo la kwamba dawa zinabadilika kutokea ofisi yake si kweli, bali wao wanapima wanachopelekewa.

TMAA YAOKOA BILIONI 15 ZA MADINI, YAPONGEZWA

Na Saidi Mkabakuli


Serikali imeupongeza Wakala wa ukaguzi wa madini nchini (TMAA) kwa kufanikiwa kuokoa kiasi kikubwa cha madini yaliyokuwa yakitoroshwa kinyemela katika viwanja vya ndege nchini hivyo kuokoa zaidi ya bilioni 15 zilizolipwa kama mrahaba tangu ilipoanzisha ukaguzi maalum kwa wasafiri waendao nje ya nchi.


Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Hab Mkwizu alipokuwa akikagua utendaji kazi wa Wakala katika maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


Bw. Mkwizu alisema kuwa kwa muda mrefu sasa wafanyabiashara wasio waaminifu wamekuwa wakiitia hasara Serikali kwa kukwepa ulipaji wa kodi wa madini yaendayo nje ya Tanzania kinyume na utaratibu uliowekwa.


“Hongereni sana kwa kuweza kuokoa kiasi kikubwa cha madini yaliyokuwa yakisafirishwa bila kufuata taratibu zetu za usafirishaji wa madini yaendayo nje ya Tanzania,” alisema Bw. Mkwizu.


Naibu Katibu Mkuu Mkwizu aliwasihi viongozi na watumishi wa Wakala kuongeza uchapaji kazi na uzalendo ili kuweza kukomesha kabisa tabia ya wafanyabiashara hao wasio waaminifu.


Akikaribishwa kwenye banda la Wakala kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja na Afisa Habari wa Wakala hiyo, Mhandisi Yisambi Shiwa, Bw. Mkwizu alijulishwa kuwa moja kati ya mafanikio yaliyofikiwa na Wakala mara baada ya ukaguzi wa ziada kwa wasafiri waendao nje ya Tanzania, ni pamoja na kubainika mamia ya wafanyabiashara wa madini ambao wamekuwa wakitorosha kinyemela madini ya thamani kubwa ya fedha bila kufuata taratibu.


“Katika kuboresha utendaji kazi wa Wakala, tulitambulisha mpangokazi mpya wa ukaguzi wa ziada katika viwanja vyetu vya ndege vikubwa vya Dar es Salaam, Kilimanjaro na kile cha Mwanza lengo ni kubaini wafanyabiashara wasio waaminifu na ndipo tulipobaini wizi huu,” alisema Mhandisi Shiwa.


Akizungumzia thamani ya madini hayo, Mhandisi Shiwa alisema kuwa kufuatia ukaguzi huu, mpaka sasa Wakala imeweza kuokoa madini yenye thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania bilioni 15.


“Ukaguzi huu umesaidia kuokoa kiasi kikubwa cha madini yenye thamani ya shilingi bilioni 15.3 hadi kufikia mwaka na hivyo kuiongezea serikali yetu mapato ambayo yalikuwa yatoroshwe na wafanyabiashara hao wasio waaminifu,” aliongeza.


Kwa mujibu wa Mhandisi Shiwa, kiasi hiki cha fedha ni sehemu ya mrahaba wa kisheria unaostahili kuchangiwa na wafanyabiashara hao kwa umiliki wao wa madini hayo kabla ya kusafirisha nje ya nchi.


Mhandisi Shiwa aliongeza kuwa katika kuendelea kudhibiti tabia hizi, Wakala kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali imekuwa ikishikilia na kutaifisha madini yanayotiliwa shaka ama kumilikiwa isivyo halali yanayopatikana katika viwanja hivyo.


Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania ni Wakala wa Serikali ulioanzishwa tarehe 2 Novemba, 2009 chini ya Sheria ya Wakala wa Serikali, Sura ya 245. Tamko la Waziri la kuanzisha Wakala lilichapishwa kwenye Gazeti la Serikali Namba 362 la tarehe 6 Novemba, 2009. 


Lengo la Wakala ni kuhakikisha kwamba, Serikali inapata mapato stahiki kutoka kwenye shughuli za uzalishaji na biashara ya madini nchini kupitia usimamizi na ukaguzi makini wa shughuli za uchimbaji, na kuhakikisha kuwa shughuli hizo zinafanyika kwa kuzingatia uhifadhi na utunzaji thabiti wa mazingira katika maeneo ya migodi.

Alhamisi, 19 Juni 2014

DR. MWANJELWA ATAKA WAFANYABIASHARA MBEYA WAPATE NAFASI SOKO LA KIMATAIFA




WAKATI kukiwa na tetesi za kwamba baadhi ya wafanyakazi wa Jiji la Mbeya na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa Jijini hapa wamejigawia vyumba katika soko jipya la Mwanjelwa, Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, ameiomba serikali kutupia macho soko hilo na kuhakikisha hata wafanyabiashara wa kawaida wanapata nafasi.

Hayo aliyasema jana wakati anachangia Hotuba ya Bajeti kuu ya serikali mjini Dodoma.

Alisema soko hilo kwa sasa licha ya kutokamilika kwa wakati, serikali kupitia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Jiji la Mbeya limepata mkopo mwingine wa Bilioni tatu kwa ajili ya kukamilisha ujenzi na wamepata mkandarasi mpya.

‘’Kama unavyoelewa Mheshimiwa Spika, kule kwangu Mbeya, kuna soko la kimataifa na Waziri Mkuu anajua na katika miezi nane ijayo soko litakamilika na ninaomba Wizara ya Fedha itupatie gurantee ya 3.4 bilioni ili tuweze kupata mara moja na wafanyabiashara wote wanufaike na soko ambalo lina jina langu la Mwanjelwa’’ alisema Dr. Mwanjelwa.

Pia aliiomba serikali kuchepusha barabara ya magari makubwa kutoka Uyole mpaka Songwe Mbeya Vijijini, ambako kuna uwanja wa Ndege ili kusaidia kuondoa msongamano wa magari Jiji la Mbeya ambalo linapanuka kila siku.

Mbali na jambo hilo, alichangia mambo mbalimbali likiwemo suala la misamaha ya kodi inayotolewa na serikali kwa wafanyabiashara wakubwa, migodi na makapuni ya simu, huku akieleza kuwa serikali inapaswa pia kufufua viwanda ili kupunguza tatizo la ajira.

“Mheshimiwa spika, uchumi wa nchi tunaambiwa kuwa unakua sana, sasa watanzania hawana kipato na maisha yao yanazidi kushuka, sasa uchumi unakua kwa namna gani? Deni la taifa linatishia usalama wa taifa, ongezeko la asilimia 29 najiuliza je tutafika?’’ alihoji Mbunge huyo.

‘’Tumekuwa tunazungumzia kuhusu walimu, naishauri serikali walimu wasikatwe maana wafanyakazi wote Tanzania wanaokatwa, wakienda sokoni pia wanaendelea kukatwa tena, wakati wanakatwa kodi mishahara yao’’.

Alishangaa kuwa Bunge linaidhinisha bajeti lakini pesa haitoki na kwamba matumizi mengine yanatumika bila kuidhinishwa, hivyo alihoji kama bunge hilo linatUmika kama stempu au la.

Aliitaka Wizara ya fedha pamoja na wabunge kurudi bungeni kuelezana mrejesho wa matumizi ya fedha za serikali na kwamba ifike mahala wabunge wawe wakali na sheria kali zitungwe ili wanaochelewesha fedha au kuhusika kwenye Fund Location na fund department wawajibishwe, pesa zisipotolewa kwa wakati.

“Kuna kipindi nilisimama hapa na kusema halmashauri zote zilizo na hati chafu ziadhibiwe, kwanini mambo yanafichwafichwa, kuna nini? makampuni ya simu na madini mbona hatuambiwi mikataba yake na misamaha ya kodi? Watanzania wajulishwe na wawekwe wazi’’ alisema.

Alisema watanzania wa kawaida wanaumia kutokana na bajeti ya kutegemea pombe na sigala na vinywaji, kwasababu ndiyo wanaotumia vitu hivyo kila siku.

‘’Ninaomba sana, tuangalie jinsi gani tufufue viwanda vyetu kusaidia ajira kwa vijana wanaokimbilia mijini na haya ndiyo maendeleo yenyewe. Kwenye private sector kule watu wanafanya kazi hakuna rongorongo na hii PPP, itasaidia kufufua viwanda na kuongeza ajira’’ alisema.

Jumatatu, 16 Juni 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 16.06.2014.


Kamanda wa polisi mkoani Mbeya,Ahmed Msangi.


KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU MMOJA MWANAUME ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 35- 40 AMEFARIKI DUNIA BAADA YA GARI GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.974 CMC AINA YA CANTER LIKITOKEA MBEYA MJINI KUELEKEA MAKAMBAKO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AMBAYE BADO KUFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI KULIGONGA GARI T.777 AHF/T.107 BVB AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIMEHARIBIKA NA KUEGESHWA PEMBENI YA BARABARA.

AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 15.06.2014 MAJIRA YA SAA 19:15 JIONI KATIKA KIJIJI NA KATA YA IMEZU, TARAFA YA TEMBELA, WILAYA YA KIPOLISI MBALIZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA, DEREVA ALIKIMBIA  NA KULITELEKEZA GARI  MARA ENEO LA TUKIO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.  MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.

KATIKA TUKIO LA PILI:

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI KATIKA SHULE YA SEKONDARI SWAYA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA SIMON JULIUS (16) MKAZI WA IYELA AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.745 NBA AINA YA CANTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA BARAKA ABDI (25) MKAZI WA IYELA KUPINDUKA.

AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 15.06.2014 MAJIRAYA SAA 14:00 MCHANA KATIKA ENEO LA MAKABURINI IYELA, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU WENGINE WANNE WALIPATA MAJERAHA KATI YAO WANAWAKE WATATU NA MWANAUME MMOJA WOTE WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA AMEKAMATWA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.


KATIKA MISAKO:

MSAKO WA KWANZA:

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKAKWA JINA LA ELIAS LUCAS (38) MKAZI WA KIJIJI CHA ITUMBI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 25.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.06.2014 MAJIRA YA SAA 17:50 JIONI KATIKA KIJIJI CHA ITUMBI, KATA YA MATUNDASI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA.



MSAKO WA PILI:

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BARAKA MWAMBUNGU (23) MKAZI WA KIJIJI CHA ITUMBI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI GRAM 500.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.06.2014 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI KATIKA KIJIJI CHA ITUMBI, KATA YA MATUNDASI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] NA BHANGI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.


MSAKO WA TATU:

MTU MMOJA MKAZI WA NAKONDE NCHINI ZAMBIA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JAMES SILUMBWE (28) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NOTI BANDIA 02 ZA TSHS 10,000/= SAWA NA TSHS 20,000/= ZIKIWA NA NAMBA BU-7282385. 

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.06.2014 MAJIRA YA SAA 10:30 ASUBUHI KATIKA MTAA WA TUKUYU, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, MKOA WA MBEYA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUCHUKUA TAHADHARI NA MATAPELI PIA KUTOA TAARIFA ZA MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA UTENGENEZAJI WA NOTI BANDIA ILI WAKAMATWE.


MSAKO WA NNE:

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA TIMOTH KAPALISYA (33) MKAZI WA KYELA  ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BIDHAA ZILIZOPOGWA MARUFUKU NA SERIKALI.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.06.2014 MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI KATIKA MTAA WA BENKI- MWANJELWA, KATA YA RUANDA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKAMATWA AKIWA NA POMBE KALI [VIROBA] AINA YA DOUBLE PUNCH ZIKIWA KWENYE MIFUKO MIKUBWA MITATU YA  SANDARUSI KILA MMOJA UKIWA NA UJAZO WA DEBE SITA [06] BAADA YA  KUINGIZWA NCHINI KUTOKA NCHINI MALAWI.

Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...