TIMU ya soka
ya Tanzania Prison(wajelawajela) ya Jijini Mbeya, imeandaliwa mapokezi mazito
baada ya mashabiki kuridhishwa na kiwango cha wachezaji wake.
Mapokezi
hayo yatafanyika kesho kutwa Jumatano eneo la Oil Com Uyole Jijini hapa, huku
mashabiki kadhaa wakifika katika ofisi za Jiji la Mbeya kuomba vibali vya
kufungua matawi ya timu hiyo.
Mjumbe wa
kamati tendaji ya timu hiyo Mohamed Lalika, amethibitisha kuwepo kwa mapokezi
hayo na kwamba wanawakaribisha mashabiki wa timu zingine ambao waliasi.
‘’Kama
ilivyo kauli mbiu yetu kuwa tumejipanga hatoki mtu, hivyo wale wote waliopotea
wanaruhusiwa kurudi kushabikia timu yao halisi bila masharti yeyote’’ alisema
Lalika.
Naye mwanachama
wa Yanga Christopher Nyenyembe ambaye amesema kuwa ni shabiki timu ya Prison, alisema timu hiyo ina umbo la
timu.
‘’Mimi ni
shabiki mkubwa wa timu ya Prison na nitaendelea kuwa shabiki kwasababu timu
hiyo ina umbo la timu tofauti na timu ya Mbeya City ambayo wachezaji hawachezi
kama timu bali kila mmoja anacheza kwa uwezo wake’’ anasema Nyenyembe.
Ayas Yusuph(Asia),
mkazi wa Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini, alisema kuwa katika eneo la Mbalizi
tayari wamefanya uchaguzi wa tawi la timu hiyo kwa lengo la ushindani.
Shabiki wa
muda mrefu wa timu hiyo Jijini hapa, Herode Mdoe, alisema katika ligi kuu kuna
timu Nne pekee ambazo zina mfumo wa timu ambazo ni Tanzania Prison, Mtibwa,
Azam na Coast Union.
Aidha alichangia
mfuko mmoja wa saruji kwa ajili ya ujenzi wa tawi la Mbeya Peack ambalo
linaongozwa na Christopher Nyenyembe ambaye kitaaluma ni Mwandishi wa Habari.
Wakielezea mafanikio
ya timu hiyo na juhudi zinazofanywa na uongozi wa Prison, shabiki Emmanuel Baganda(Swahida)
na Adamu, alisema kuwa siri kubwa ni kutokana na Mwalimu David Mwamwaja
kusikiliza ushauri kwa kila mtu bila dharau.
Credit;kalulunga blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni