Jumatatu, 27 Aprili 2015

WAKAMATWA NA VIFAA VYA JESHI LA ULINZI WA WANANCHI WA TANZANIA HUKO TUNDUMA



MNAMO TAREHE 24.04.2015 MAJIRA YA SAA 09:30 ASUBUHI HUKO MAENEO YA MTAA WA SOGEA KATIKA MJI MDOGO WA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA, VIJANA WAWILI WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. MATHEW ANGANILE MWAFONGO @ RASI (27) MKAZI WA TUNDUMA NA MWENZAKE AITWAYE SALEHE TABULEI SICHALWE (22) MKAZI WA MAJENGO TUNDUMA WALIKAMATWA NA POLISI BAADA YA WANANCHI WA ENEO HILO KUWATILIA MASHAKA KUWA NI WAHALIFU, HII NI KUTOKANA NA MVAO WAO AMBAO ULIKUWA UMEFICHA SURA ZAO.

VIJANA HAO WALIKUWA WAKITUMIA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.855 CDQ AINA YA T-BETTER NA WALIKUWA NA BEGI MOJA AMBALO MMOJA WA VIJANA HAO ALIKUWA AMELIVAA MGONGONI.

POLISI WALIPOWAPEKUA KATIKA BEGI HILO WALIKUTA VISU VIWILI, MANATI MBILI, MAWE AROBAINI YA KURUSHWA KWA MANATI NA NATI NNE ZA KURUSHWA KWA MANATI, KOFIA MBILI ZA JESHI, BUTI JOZI MBILI, MIWANI MIKUBWA INAYOTUMIWA NA POLISI KATIKA MISAFARA, SHEEGUARD JOZI NNE (VIFAA MAALUM VYA KUVAA KWENYE MAGOTI NA VIWIKO VYA MIKONO), MAKOTI MAWILI MAREFU, VIFAA VYA KUFANYIA MAZOEZI YA “PUSH UP” NA KAMBA YA KUFANYIA MAZOEZI YA KURUKA.

AIDHA KATIKA BEGI HILO KULIKUTWA PIA T-SHIRT MOJA YA CHADEMA, BENDERA MBILI NDOGO ZA CHADEMA, KITAMBAA/KILEMBA KIMOJA NA BARUA TATU ZA KUWATAMBULISHA WATUHUMIWA KWENDA KUTOA MAFUNZO KWA RED BRIGADE HUKO MAENEO YA KATA YA CHITETE, MSANGANO NA KAMSAMBA  WILAYANI MOMBA.






KATIKA KUHOJIWA, WATUHUMIWA HAO WALIKIRI KUWA WANAENDA KUTOA MAFUNZO KWA VIJANA WA RED BRIGADE KATIKA KATA HIZO TAJWA HAPO JUU. KUTOKANA NA MATISHIO TULIYONAYO YA USALAMA NA VIASHIRIA VYA UVUNJIFU WA AMANI NA UTULIVU NCHINI, WATUHUMIWA HAO WALIFIKISHWA POLISI MKOA KWA MAHOJIANO ZAIDI NA BAADA YA UCHUNGUZI, JALADA LITAPELEKWA KWA MWANASHERIA WA SERIKALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANAWASHUKURU WANANCHI KWA KUCHUKUA TAHADHARI ZA KIUSALAMA KWA KUTOA TAARIFA HARAKA. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA HARAKA KATIKA VYOMBO VYA USALAMA PALE WANAPOTILIA MASHAKA MTU/WATU AU VITENDO VYA MTU/WATU AU KIKUNDI CHA WATU ILI HATUA STAHIKI ZICHUKULIWE HARAKA IWEZEKANAVYO.

Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Jumatano, 22 Aprili 2015

LIVE..... DR. MARY MWANJELWA AWA MGENI RASMI MAHAFALI YA 13 YA KIDATO CHA SITA MBEYA SECONDARY

 Mwanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya Mbeya sekondari iliyopo Jijini Mbeya, akimweleza Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya Dr. Mary Mwanjelwa, jinsi teknolojia ya simu inavyoweza kutoa fursa ya umwagiliaji bila binadamu kuwa shambani.
 Mwanafunzi Jerry Mahenge (19) wa kidato cha tano katika shule ya Mbeya sekondari iliyopo Jijini Mbeya, akimweleza Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya Dr. Mary Mwanjelwa, jinsi uchanganyaji wa kemikali unavyofanywa katika kujifunza masomo ya sayansi katika shule hiyo.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya Dr. Mary Mwanjelwa, akishika simu ambayo inatumika katika teknolojia ya umwagiliaji wa bustani au shamba bila mwanadamu kuwa shambani kwa muda unaotakiwa kumwagilia.

 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya Dr. Mary Mwanjelwa, akiingia katika ukumbi wa mikutano wa shule ya Mbeya Sekondari Jijini Mbeya, ambapo yeye ndiye mgeni rasmi katika mahafali ya 13 ya kidato cha sita tangu kuanzishwa shule hiyo mwaka 1962.
 Meza kuu.

Sanaa na maonesho ya mitindo ikiendelea ukumbini.






Jumatatu, 20 Aprili 2015

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 20.04.2015.



KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MWENDESHA PIKIPIKI ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA BONY ALLY MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 25-30 MKAZI WA NZOVWE JIJINI MBEYA ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA PIKIPIKI ALIYOKUWA AKIENDESHA YENYE NAMBA ZA USAJILI MC 709 AFQ AINA YA KINGLION KUGONGANA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.101 BFB AINA YA TOYOTA PRIMEO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE SETH MWAKYALABA (54) MKAZI WA MWAKIBETE.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 19.04.2015 MAJIRA YA SAA 16:30 JIONI HUKO ENEO LA MBEMBELA, KATA YA NZOVWE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA AMEKAMATWA, GARI NA PIKIPIKI ZIPO KITUO CHA POLISI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.


TAARIFA ZA MISAKO:

KATIKA MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. FRANK JOSEPH (24) MKAZI WA MWANJELWA 2. BURTON MWAIPOPO (37) MKAZI WA SAE 3. HARUNA JOSEPH (24) MKAZI WA MAJENGO NA 4. BENEDICTOR DAUD (28) MKAZI WA ITIJI WAKIWA NA BHANGI MISOKOTO MITATU YENYE SAWA NA UZITO WA GRAM 15.

WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.04.2015 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO ENEO LA STENDI KUU YA MABASI, KATA NA TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA KITONGOJI CHA MAPILI WILAYANI CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NYAMIZI LUBHANGA (23) AKIWA NA NYARA ZA SERIKALI VIPANDE VINNE VYA  MAGAMBA YA KAKAKUONA, MKIA WA NGIRI NA MAFUTA YA SIMBA.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.04.2015 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KITONGOJI CHA MAPILI, KIJIJI CHA BITIMANYANGA, KATA YA MAFYEKO, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA MBEYA.


KATIKA MSAKO WA TATU, JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA HALUNGU – MGOMBANI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MICHAEL SHUGHULI (22) AKIWA NA BHANGI KETE TATU SAWA NA UZITO WA GRAM 15. 

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.04.2015 MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KIJIJI CHA MPONA, KATA YA TOTOWE, TARAFA YA SONGWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA MBEYA. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MTUHUMIWA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.


Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Alhamisi, 9 Aprili 2015

AUAWA KWA KUCHOMWA KISU NA MKE MWENZA.




MWANAMKE MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA NGWALA WILAYANI CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ELIZA SWEETY (44) ALIUAWA KWA KUCHOMWA KISU SEHEMU ZA SHINGONI, MGUU NA MKONO WA KUSHOTO NA MKE MWENZA WAKE AITWAE PAULINA EFESTI MWAMBE (46) MKAZI WA NGWALA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 06.04.2015 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA NGWALA, TARAFA YA SONGWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.

INADAIWA KUWA, CHANZO CHA TUKIO HILO NI WIVU WA KIMAPENZI KWANI PAULINA EFESTI MWAMBE AMBAYE NI MKE MWENZA ALIKUWA AKIMTUHUMU MAREHEMU KUPENDWA ZAIDI NA MUME WAO AITWAE GERVAS MWAIPOSI (50) MKAZI WA NGWALA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA UPELELEZI ZAIDI UNAENDELEA.


KATIKA TUKIO LA PILI:

MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 03 ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AIRICH JACKSON MKAZI WA IGAWILO ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU KATIKA KITUO CHA AFYA IGAWILO BAADA YA KUGONGWA NA MKOKOTENI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 07.04.2015 MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI HUKO IGAWILO, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.


TAARIFA ZA MISAKO:

KATIKA MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. VICTOR EDGAR (24) MKAZI WA ILEMI 2. JAMES PASCHAL (21) MKAZI WA PAMBOGO 3. RULES KAJIGILI (27) MKAZI WA MAKUNGULU NA 4. IKE MWAKYAMBIKI (30) MKAZI WA MAKUNGULU WAKIWA NA BHANGI KETE 35 NA MISOKOTO 24 SAWA NA UZITO WA GRAM 295.

WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 07.04.2015 MAJIRA YA SAA 13:30 MCHANA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO ENEO LA MAKUNGULU, KATA YA RUANDA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.





KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA MAPELELE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MARTHA FUNGO (60) AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 03 NA MTAMBO MMOJA WA KUTENGENEZEA POMBE HIYO.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 07.04.2015 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO ENEO LA MAPELELE, KATA YA NSALALA, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA KIPOLISI MBALIZI, MKOA WA MBEYA.

KATIKA MSAKO WA TATU, JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA ILEMBO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FRANK JOHN (34) MVUVI AKIWA NA NYAVU ZA KUVULIA SAMAKI AINA YA KOKOLO ZILIZOPIGWA MARUFUKU KUVULIA SAMAKI KATIKA ZIWA RUKWA.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 07.04.2015 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA KIJIJI CHA ILEMBO, KATA YA GALULA, TARAFA YA SONGWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA NA POMBE MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA WAVUVI KUACHA KUTUMIA NYAVU ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA MAENDELEO YA VIUMBE VYA MAJINI.



[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Alhamisi, 2 Aprili 2015

TUME YA MIPANGO YAPONGEZWA KWA UFANISI


Na Adili Mhina.

Ofisi ya Rais, tume ya mipango imepongezwa kwa hatua kubwa iliyopiga katika kutekeleza majukumu mbalimbli ya kitaifa.

 
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo wakati akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango lililofanyikia mjini Kibaha mwishoni mwa juma.


Mheshimiwa Ndikilo alieleza kuwa Tume ya mipango imepiga hatua kubwa katika kutekeleza majukumu yake ambayo ni pamoja na kutayarisha mpango wa taifa wa kila mwaka, kusambaza machapisho mbalimbali ya Tume ya Mipango, Kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya taifa, na kufanya mapitio ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano (2011/12-2015/16).


Pamoja na mafanikio makubwa katika kutekeleza majukumu ya Tume, Mkuu wa Mkoa alieleza kufurahishwa kwake na ufanisi wa viongozi pamoja na watumishi wa Tume ya Mipango kwa kuandaa mwongozo wa usimamizi wa uwekezaji wa umma, “ninaipongeza tume ya mipango kwa kundaa mwongozo wa usimamizi wa uwekezaji wa umma (Public Investment Management Manual), pamoja na kukamilisha tafiti mbalimbali zinazoharakisha mendeleo ya uchumi wa nchi yetu na mahitaji ya kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Mendeleo 2025.”


Vilevile uongozi wa Tume ya mipango umepongezwa kwa kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wake wa kada mbalimbali kwa kuwapeleka mfunzo ya muda mrefu na mfupi, semina na warsha zinazofanyika ndani na nje ya nchi ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi za kila siku.


Aidha Mheshimiwa Ndikilo amesisitiza wajumbe wa baraza hilo kuwaelimisha watumishi wenzao juu ya  umuhimu wa kila mfanyakazi kutimiza wajibu wake katika sehemu ya kazi ili kufikia malengo ya pamoja baina ya mwajiri na watumishi. 


“Pamoja na mambo mengine Baraza linawajibu wa kuishauri Tume kwa lengo la kuleta tija na mshikamano baina ya mtumishi na mwajiri, si jambo la busara kwa watumishi kutumia muda mwingi katika kudai maslahi zaidi kuliko kupima kiwango cha utekelezaji wa wajibu wao,” alisisitiza mhandisi Ndikilo.


Awali, Kaimu Katibu Mtendaji kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo, alieleza kuwa katika mkutano huo wajumbe watapata fursa kujadili mada nne amabazo ni mpango wa makisio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha 2015/16, Elimu ya jinsia mahala pa kazi, utekelezaji wa sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013, na haki na wajibu wa mwajiriwa mahala pa kazi. Lengo la mada hizo ni kutoa fursa kwa watumishi kujifunza zaidi ili kuweza kuboresha utendaji wao wa kazi ili kufikia lengo la Tume ya mipango la kukuza uchumi wa Taifa.


Mkutano huo wa siku mbili unaozingatia mwongozo wa Mkataba wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Baraza hilo limehudhuriwa na wakuu wote wa Klasta, Idara na vitengo, wajumbe wa TUGHE Taifa, TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam, Halmashauri ya TUGHE tawi la Tume ya Mipango, pamoja na mjumbe mmoja mmoja kutoka klasta, Idara na Vitengo.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...