Jumatano, 29 Oktoba 2014

MTOTO WA KIKE ATEKWA MBEYA

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Biton Bomani Mwashilindi, mkazi wa Airport Jijini Mbeya anatuhumiwa kumteka mtoto Zalida Rogers (2),  kutoka kwa mama yake mzazi aitwaye Juliana Josia(22) eneo la Mwanjelwa Jijini hapa.


Tukio hilo limetendeka eneo la Kituo cha mafuta Mwanjelwa Oktoba 27 mwaka huu, majira ya mchana baada ya mtekaji kufanikiwa kumfungua mbeleko mama ya mtoto kisha kufanikwa kuvuka barabara kuu kuelekea upande wa pili kutokea Airport kuelekea eneo la Makunguru.


Mama huyo alitoa taarifa katika kituo cha Polisi Mwanjelwa na kuanza kumsaka mtekaji huyo bila mafanikio huku mtekaji akituma ujumbe kupitia simu yake ya kiganjani akimtaka mama wa mtoto huyo ili kuyajenga  na aweze kumkabidhi mtoto wake.


Hata hivyo mtekaji huyo aliendelelea kutuma ujumbe wa vitisho kwa mama mzazi wa mtoto huyo kuwa wafanye mazungumzo eneo la njia panda Magege ili amwachie mwanawe na asipofanya hivyo hatamkabidhi mtoto wake.


Jana mtekaji huyo alimtaka Juliana Josia aende eneo la Magege akiwa peke yake ili wazungumze kisha amkabidhi mtoto na ndipo Juliana akiwa na Askari kanzu walifika eneo hilo majira ya mchana huku akitumia simu ya rafiki yake na Askari walipofika eneo husika mtuhumiwa alimtuma rafiki yake ambaye hakufahamika mara moja na yeye kutokomea na mtoto kusiko julikana.


Polisi wanamshikilia rafiki yake Biton kwa mahojiano ingawa Biton mwenyewe akiendelea kutuma jumbe za vitisho mfululizo na moja ya ujumbe ukidai kwa kuwa Polisi wamemkamata rafiki yake basi ataozea jela lakini yeye hatamkabidhi mtoto.


Taarifa zinadai kuwa mama wa mtoto huyo, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa na mtuhumiwa miaka miwili iliyopita na mtuhumiwa alidai kuwa huyo ni mtoto wake.



Jalada la uchunguzi  limefunguliwa kituo kikuu cha Polisi Mbeya, lenye namba MB/RB/9384/2014 .

Jumanne, 28 Oktoba 2014

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI JESHI LA POLISI TANZANIA.






TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 28.10.2014.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA SAMANGOMBE ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA SHIDA WILSON MAZWILE (35) ALIUAWA KWA KUCHOMWA KISU TUMBONI BAADA YA KUVAMIWA NA MTU/WATU WASIOJULIKANA AKIWA AMELALA NYUMBANI NA MKE WAKE MDOGO AITWAYE CHRISTINA SAITON TANDALA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.10.2014 MAJIRA YA SAA 00:01 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA SAMANGOMBE, KATA NA TARAFA YA KAMSAMBA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO HAKIJAFAHAMIKA. JUHUDI ZA KUWATAFUTA WATUHUMIWA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO/WALIPO WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.

KATIKA TUKIO LA PILI:

MTU MMOJA MKAZI WA SENJELE WILAYA YA MBOZI ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA SEMENI SHANGU (22) ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.426 CXT AINA YA YUTONG LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE BRUGE MZAVA (37) MKAZI WA SUMBAWANGA.

AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 27.10.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA SENJELE, KATA YA MYOVIZI, TARAFA YA IYULA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI, DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.

TAARIFA ZA MISAKO:

KATIKA MSAKO WA KWANZA, MTU MMOJA AITWAYE EDAH SING’OMBE (32) MKAZI WA MACHINJIONI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 05 PAMOJA NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA POMBE HIYO.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 27.10.2014 MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.  MTUHUMIWA NI MPIKAJI NA MUUZAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.



KATIKA MSAKO WA PILI, MTU MMOJA AITWAYE JOSHUA MWAKAJA (43) MFANYABIASHARA NA MKAZI WA MAJENGO ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU AINA YA DOUBLE PUNCH PAKETI 66.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 27.10.2014 MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI HUKO KATIKA MTAA WA MAJENGO, KIJIJI NA KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIZO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.


KATIKA MSAKO WA TATU, MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ELIZABETH ERNEST (20) MKAZI WA MAKONGOLOSI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 10.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 27.10.2014 MAJIRA YA SAA 14:30 MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MACHINJIONI, KIJIJI NA KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO.


KATIKA MSAKO WA NNE, MTU MMOJA MKAZI WA MKWAJUNI WILAYANI CHUNYA AITWAYE SHUGHULI SIX (30) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI UZITO WA ROBO KILO.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA NA KUKUTWA NA BHANGI HIYO MNAMO TAREHE 27.10.2014 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KIKUYU, KIJIJI NA KATA YA MKWAJUNI, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKUTWA NA BHANGI HIYO BAADA YA KUPEKULIWA KATIKA BANDA LAKE LA KUUZIA POMBE. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA [BHANGI], POMBE HARAMU YA MOSHI PAMOJA NA POMBE KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU AU MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI NA USAMBAZAJI WA BIDHAA HARAMU ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.

Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Jumamosi, 25 Oktoba 2014

MAHAFALI ST. AGGREY MBEYA, MBUNGE WA VITI MAALUM CCM, DR. MARY MWANJELWA AWA MGENI RASMI

 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, Kulia, akiwa na Meneja wa taasisi za St. Aggrey, Jackson Kamugisha wakati wa mahafali ya shule ya sekondari ya St. Aggrey Mbeya jana.

 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, Kulia, akicheza twist na wanafunzi wa St. Aggrey chanji ya Sumbawanga, wakati wa mahafali ya shule ya sekondari ya St. Aggrey Mbeya jana.
 Kwaito nayo ilikuwepo, kushoto ni Mkurugenzi msaidizi wa taasisi za St. Aggrey, Neema Mwambusi.



 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, katikati, akiwa anavalishwa skafu na vijana wa skauti wa shule ya St. Aggrey Mbeya, wakati wa mahafali ya shule ya sekondari ya St. Aggrey Mbeya jana.


 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa,  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa taasisi za St. Aggrey, wakati wa mahafali ya shule ya sekondari ya St. Aggrey Mbeya jana.


 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, Kulia, akiwapongeza wanafunzi Amani Mwakyelu na Matha Samwel wa kidato cha Nne shule ya sekondari St. Aggrey Mbeya jana, baada ya kupata zawadi za nidhamu. Kulia ni Makamu Mkurugenzi wa taasisi za St. Aggrey, Neema Mwambusi na kushoto ni Meneja wa taasisi hizo, Jackson Kamugisha, wakati wa mahafali ya shule ya sekondari ya St. Aggrey Mbeya yaliyofanyika juzi shuleni hapo.

MBUNGE MULUGO NA DR. MWANJELWA WAAGA MWILI WA MZEE NICODEM KAZUMBA MBEYA VIJIJINI

 Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akizungumza jambo katika msiba wa mzee Nicodem Kazumba, aliyefariki baada ya kugongwa na gari mjini Mbalizi wilaya ya Mbeya, mbkoani hapa. Mbunge huyu aliungaa na Mbunge wa Jimbo la Songwe wilayani Chunya, Philipo Mulugo kuhani msiba huo na kumpa pole mtoto wa marehemu, aitwaye, George Kazumba.
 Waombolezaji wakiomboleza msiba huo, eneo la Mtakuja Mbalizi Mbeya.
Mbunge wa Jimbo la Songwe wilayani Chunya, Philipo Mulugo kuhani msiba na kumpa pole mtoto wa marehemu, aitwaye, George Kazumba, kufuatia kifo cha Baba yake mzazi, Nicodem Kazumba, aliyefariki baada ya kugongwa na gari mjini Mbalizi wilaya ya Mbeya, mbkoani hapa.

 George Kazumba akizungumza na Mama yake mzazi katika msiba huo jana, mjini Mbalizi Mbeya.
 Mbunge wa Jimbo la Songwe wilayani Chunya, Philipo Mulugo na Mbunge viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, wakiaga mwili wa marehemu, Nicodem Kazumba, aliyefariki baada ya kugongwa na gari mjini Mbalizi, wilaya ya Mbeya Vijijini na  kumpa pole mtoto wa marehemu, aitwaye, George Kazumba(kulia).

MBUNGE VITI MAALUM ALIPOKUWA MGENI RASMI HIVI KARIBUNI KATIKA KANISA KATOLIKI MJINI CHUNYA MKOANI MBEYA NA AKAZINDUA KANDA YA KWAYA



Jumamosi, 18 Oktoba 2014

89 MBEYA MJINI, WAIKIMBIA CHADEMA NA KUJIUNGA CCM

 Mbunge wa viti maalum mkoani Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akizungumza na baadhi ya vijana waliotoka Chadema na kujiunga na CCM jimbo la Mbeya mjini jana.
 Mbunge wa viti maalum mkoani Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akizungumza na baadhi ya vijana waliotoka Chadema na kujiunga na UVCCM jimbo la Mbeya mjini jana kisha akawakabidhi jezi.

VIJANA 89 waliokuwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Mbeya mjini linaloongozwa na Mbunge Joseph Mbilinyi(Sugu), wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Wanachama hao wapya wa CCM, walijiunga na chama hicho jana katika kata za Ilomba na Ruanda wakitokea katika maeneo ya Ilomba, Mama John, Makunguru, Mwanjelwa na Kabwe.

Akiwapokea na kuwakabidhiwa kadi zao mpya za CCM na UVCCM, Mbunge wa Viti maalum mkoani Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, aliwapongeza kwa uamuzi wao wa kurejea na wengine kujiunga na kuchukua kadi za chama hicho.

“Nawapongezeni wote maana hamjakosea kurejea kwenye chama salama ambacho kinajali vijana kwa kuwawezesha kuwa wajasiliamali”alisema Dr. Mwanjelwa.

Awali akisoma risala ya chama tawi la Ilomba, Katibu wa tawi hilo Lucian Kapinga, alisema kuwa wakati wa vurugu zilizotokea Jijini Mbeya na kupachikwa jina la “Maandamano ya machinga”, baadhi ya wajumbe walinusurika kufa baada ya ofisi hiyo kuvamiwa na vijana na kuichoma moto wakati wajumbe wakiwa kwenye kikao.


Alisema kutokana na uhalibifu huo, jengo lao liliungua na kulazimika kulifumua na kulifanyia ukarabati ambapo kwa sasa umebaki ukarabati mdogo unaogharimu kiasi cha Tsh.6000,000/=.

Dr. Mwanjelwa aliwapa pole na kuchangia kiasi cha Tsh.200,000/= huku akiwaasa vijana kuepukana na mkumbo wa siasa za vurugu, huku akiwapatia jozi moja ya jezi na mipira minne kwa ajili ya vijana wa kike na kiume.

Nape nnauye akumbushwa ahadi.

Katika mfululizo wa ziara za Mbunge Dr. Mary Mwanjelwa Jimbo la Mbeya Mjini za kupokea wanachama wapya kutoka Chadema, alisomewa risala ya kumkumbusha Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Taifa, Nape Nnauye aliyowaahidi vijana wa mtaa wa Blue house Kabwe Mwanjelwa, kuhusu ujasiliamali.

Akisoma risala hiyo kwa niaba ya wenzake 50,ndani ya ukumbi wa Mfikemo Hotel, Mariam Hamisi, alisema kuwa Nape alitembelea eneo hilo na kuwaahidi vijana hao kuwapatia mtaji endapo watafungua akaunti benki, ambapo kwa sasa tayari wamefungua akaunti na kuunda kikundi chao kinachojuliakana kwa jina la Halimpya kasi mpya.

“Sisi tumebadilika na kurejea CCM, wapo wengi nyuma yetu, tunakiomba chama kimsimamishe mtu anayekubalika ili kukomboa jimbo la Mbeya mjini na sisi tuna imani na wewe, tunaomba pia ututangaze hata kwa marafiki zako ili tuwe mfano kwa wenzetu kuhusu uchumi” alisema Mariam.
Baada ya risala hiyo, kundi lingine la vijana walijitokeza na kutamka kuwa nao wanahitaji kujiunga na CCM na kuwa na kikundi kilichosajiliwa ili wawe wajasiliamali na kwamba wametumikishwa vya kutosha na Chadema bila kupewa maarifa ya kujikwamua kiuchumi.

Akijibu risala na maoni ya waliojitokeza katika eneo hilo, Dr, Mwanjelwa aliwahakikishia kuwa risala hiyo ataifikisha kwa Nape Nnauye na yeye akawakabidhi Tsh. 200,000/= na kumwagiza Katibu wa UVCCM wilaya ya Mbeya Mjini, Julius Msaka kuwa akutane na vijana wanaohitaji kurejea na kujiunga na CCM na kutaka kuwa wajasiliamali ili wapange jinsi ya kuanzisha kikundi na utaratibu wa kupewa kadi za chama hicho.


Mbali na mambo mengine, aliwasihi wanachama hao wapya na wengine kujitokeza kujiandikisha katika uboreshaji wa daftari la kudumu, zoezi ambalo alisema litaanza mwezi ujao.

Sanjali na hayo alitetea suala la rasimu ya tatu ya katiba kuwa imejaa maslahi ya wananchi likiwemo suala la hamsini kwa hamsini kwa wanawake ambalo aliwasihi wanawake kutolitumia vibaya ikiwemo kuvuruga maadili na utu wa mwanamke matokeo yake litavunja ndoa.

Jumatano, 15 Oktoba 2014

MWANAMKE AUAWA KWA KUSHINDWA KULIPA T.SH,3,000/=





Kamanda wa polisi mkoani Mbeya,Ahmed Msangi.
 


WAKATI wajumbe maalum wa katiba wakiwa wamependekeza suala la haki za binadamu na mgawanyo sawa wa madaraka kati ya mwanamke na mwanaume, vitendo vya ukatili na mauaji kwa wanawake vimezidi kushika kasi mkoani Mbeya.

Katika tukio la hivi karibuni, mwanamke mmoja aliyejulikana kwa kwa jina la Rutina Ng’ekele(75), mkazi wa kijiji cha Mabondeni, kata ya Bulyaga, tarafa ya Tukuyu mjini wilayani Rungwe, amefariki dunia katika hospitali ya Makandana wilayani Rungwe, akiwa anapatiwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa mateke na ngumi.

Taarifa zinasema kuwa, Bibi huyo alishambuliwa vikali sehemu mbalimbali za mwili wake na mtu aliyefahamika kwa jina la Nicolous Afyasisye.

Tukio hilo limeelezwa kutokea Octoba 4, mwaka huu, majira ya saa moja usiku na kupelekea marehemu kulazwa hospitalini hapo mpka mauti yalipomfika jana Octoba 14, mwaka huu, saa sita mchana.

Chanzo cha tukio hilo, kimeelezwa kuwa ni marehemu kumlipa mtuhumiwa Tsh.7,000/= badala ya Tsh.10,000/= aliyokuwa akidaiwa na mtuhumiwa, jambo ambalo lilisababisha mtuhumiwa aanze kumshambulia marehemu.

Baada ya kitendo hicho, mtuhumiwa alikimbilia kusikojulikana na Jeshi la polisi limethibitisha kuwepo kwa tukio hilo.

Kamanda wa polisimkoani Mbeya, Ahmed Msangi, alisema kuwa anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mahala alipo mtuhumiwa wa tukio hilo, azitoe katika mamlaka husika ili akamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

Ijumaa, 10 Oktoba 2014

DR. MWANJELWA AMWAKILISHA VEMA KATIBU MKUU WA CCM TAIFA, AWASILISHA MABATI 40 ALIYOAHIDI KATA YA NSALAGA MBEYA

 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, (CCM), akizungumza na wanawake wa kikundi cha ujasiliamali cha bonde la Uyole maarufu kwa jina la Amka Woman Group, kabla ya kuwakabidhi cherehani yenye thamani ya Tsh, 300,000/= na fedha taslimu Tsh, 100,000/=.

 Waohhhh!....
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, (CCM), akimpatia kadi ya uanachama wa Chama Cha Mapinduzi, mmoja wa wananchi aliyeamua kujiunga na chama hicho katika kata ya Nsalaga, Jijini Mbeya leo. Wananchi 26, wamepatiwa kadi za chama hicho.
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, (CCM),akiwapatia kadi wanachama wapya, katika kata ya Nsalaga Uyole Jijini Mbeya leo.

 Baadhi ya wananchi wakimpongeza na kumshukuru Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, (CCM),baada ya kufikisha salama mabati 40, ambayo Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulhaman Kinana, aliahidi Desemba 4, 2013, alipotembelea Jijini Mbeya na kuona jitihada za wanachama wa CCM wa kata hiyo kujenga ofisi nzuri.

 Mbunge wa viti malum mkoa wa Mbeya, (MNEC), Dr. Mary Mwanjelwa, akisalimiana na baadhi ya waasisi wa CCM, waishio katika kata ya Nsalaga Jijini Mbeya.
 Ndiyo maana ninzile.... wakiimba viongozi wa ccm na baadhi ya wanachama kata ya Nsalaga Jijini Mbeya, baada ya Dr. Mary Mwanjelwa kufika eneo hilo.
 Kulia ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mbeya, Fatuma Kasenga, wakifurahi pamoja baada ya kuwasili katika viwanja vya ofisi ya CCM kata ya Nsalaga wilaya ya Mbeya Mjini, kwa ajili ya kukabidhi mabati 40 ambayo aliahidi katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulahman Kinana.
 Kizazi hiki pia kilikuwepo kikifurahia matukio..
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, (CCM), akizungumza na wanachama wa CCM na baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wake wa kukabidhi mabati 40, ambayo Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulhaman Kinana, aliahidi Desemba 4, 2013, alipotembelea Jijini Mbeya na kuona jitihada za wanachama wa CCM wa kata hiyo kujenga ofisi nzuri.

Dr. Mwanjelwa, pia yeye alichangia kiasi cha Tsh.200,000/= na kuahidi kutoa mifuko 20 ya saruji.


Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, (CCM),akikabidhi mabati 40, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulhaman Kinana, ambaye aliahidi Desemba 4, 2013, alipotembelea Jijini Mbeya na kuona jitihada za wanachama wa CCM wa kata hiyo kujenga ofisi nzuri.


 Baadhi ya wanachama wa CCM kata ya Nsalaga, wilaya ya Mbeya Mjini, wakimshukuru Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, (CCM),baada ya kufikisha salama mabati 40, na kuwakabidhi kwa uaminifu, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulhaman Kinana, aliyeahidi Desemba 4, 2013, alipotembelea Jijini Mbeya na kuona jitihada za wanachama wa CCM wa kata hiyo kujenga ofisi nzuri.
 MUNGU AKUBARIKI..
Picha ya pamoja kati ya Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, (CCM), na baadhi ya wanawake wa kikundi cha ujasiliamali cha bonde la Uyole maarufu kwa jina la Amka Woman Group, kabla ya kuwakabidhi cherehani yenye thamani ya Tsh, 300,000/= na fedha taslimu Tsh, 100,000/=.

Jumatatu, 6 Oktoba 2014

MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA, DR. MARY MWANJELWA, KUANZA ZIARA YAKE MBEYA MJINI

 Kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Songwe mkoani Mbeya, Philipo Mulugo, Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa na Mbunge wa Jimbo la Kyela, Dr. Harrison Mwakyembe. 

TAARIFA kutoka ofisi ya Mbunge wa Viti maalum mkoani Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, zimesema kuwa Mbunge huyo baada ya kumaliza shughuli za Bunge maalum la Katiba mjini Dodoma wikiiliyopita, anatarajia kuanza ziara yake katika Jimbo la Mbeya mjini.

Mbunge huyo, anatarajia kutembelea makundi mbalimbali ya kijamii ikiwa ni pamoja na kutimiza ahadi ambazo alizikubali baada ya kupelekewa maombi ofisini kwake kutoka kwa wananchi.

Ziara hiyo inategemewa kuanza tarehe 9/10/2014.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...