Jumamosi, 26 Septemba 2015

CCM YARUSHA JESHI LA ANGA, MWIGULU AONGOZA KIKOSI...WAIMARISHA USHINDI WA KISHINDO MAJIMBO YA NZEGA

Chama Cha Mapinduzi hii leo kimerusha Helcopta yake ya kwanza kwenye kila pembe ya Nchi kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu kwenye nafasi zote za Udiwani,Ubunge na Urais.Kazi ya kupasua anga hilo linaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Ushindi Ndg.Mwigulu Nchemba ambaye katika Jimbo lake la Iramba kwa asilimia 98 amejihakikishia Ushindi wa kishindo hapo Tar.25.10.2015
Vijana Imara wa Chama cha Mapinduzi Fieldmarshall Mwigulu Nchemba na Hamis Kigwangalla wakipiga Push-Up kuonesha sapoti kwa Mgombea wao J.Pombe Magufuli aliyefanya tukio hilo siku si nyingi kwenye Jukwaa la Kampeni.
Picha na Sanga Festo Jr.

Mwigulu Nchemba ambaye ni Mjumbe wa kamati ya CCM ya Ushindi na Mgombea Ubunge Jimbo la Nzega Vijijini Ndg.Kigwangalla akiwasili kwenye Ufunguzi wa kampeni za Ubunge Jimbo la Nzega Mjini hii leo.Mjumbe wa timu ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi Comrade Mwigulu NChemba ambaye hii leo ameanza safari za Anga kwa Anga kusaka kura Nchi nzima,Hapa akizungumza na Wananchi wa Nzega namna CCM ilivyosimamisha Mgombea Bora wa Urais ambaye sifa yake kuwa ni KAZI na rafiki yake Mkubwa ni TANZNAIA.Mwigulu amesema,Uchaguzi wa mwaka 2015 ni mwepesi sana kwa chama cha Mapinduzi kwakuwa wagombea wote ni zao la CCM na wanawajua vizuri.Pia wagombea wengine wa vyama vya Upinzani wanazungukwa na makundi ya Ubadhilifu wa mali za Umma wakati Magufuli yeye anazungukwa na Watu wa kazi.
Hivyo Uchaguzi huu ni DILI vs KAZI,Hivyo kazi mbayo ni J.Pombe Magufuli itashinda kwa kishindo.
 Mbunge Mtarajiwa wa Nzega Mjini Mh.Bashe akizungumza na Wananchi wake wakati wa Ufunguzi wa kampeni kwa Jimbo la Nzega Mjini hii leo.Bashe amewaomba Wananzega kumpatia Ridhaa ya kuwambunge wa Jimbo hilo ili aweze kusimamia vyema shughuli za Maendeleo kama Uimarishaji wa Huduma za Afya kwa Hospitali ya Nzega,Kusimamia haki za Bodaboda na Mamantilie wa Nzega,Kusimamia shughuli za Halmashauri ya Mji wa Nzega kwa Ufanisi.Pia amesisitiza yeye ni TEAM MAGUFULI na anaamini Maendeleo ya kweli na ya kasi yataletwa na Magufuli kwa awamu hii ya tano ya Uongozi wa Taifa letu.Wananchi wakifurahia jambo kutoka kwa Mbunge wao mtarajiwa Mh.Hussein Bashe.Mbunge Mtarajiwa wa Chama cha Mapinduzi Jimbo jipya la Nzega Vijijini Mh.Hamis Kigwangala akisalimiana na Wananchi wa Nzega mjini alipokwenda kusapoti Ufunguzi wa kampeni za Mgombea Jirani Ndg.Hussein Bashe."Ndani ya CCM ni Raha na
Furaha"

Jumatano, 23 Septemba 2015

AMUUA MKEWE KWA FIMBO



KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA, AHMED MSANGI.

MWANAMKE mmoja mkazi wa kijiji cha Mafyeko wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, aitwaye Zaina Juma@Mageta (24), aliuawa kwa kupigwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na mumewe aitwaye Malaika Wayesu (42).

Kisa cha mauaji hayo ni mtuhumiwa huyo kumkuta marehemu mkewe akifanya uzinzi na mwanaume mwingine aitwaye Kagusa Japhari, ambaye alikimbia baada ya kufumaniwa.

Mtuhumiwa amekamatwa na yupo chini ya ulinzi wa Polisi.

Shule tano za mkoa wa Mwanza zafungwa baada ya Kipindupindu kuua watu Nane


HADI sasa mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Morogoro, Singida na Mwanza, imekumbwa na kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na ugonjwa wa kipindupindu ambao umeua watu kadhaa, ambapo hali inazidi kuwa mbaya katika maeneo mbalimbali nchini, hali iliyopelekea Shule nne za Msingi na moja ya Sekondari katika Kata ya Irugwa wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, zimefungwa kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo kisiwani humo. 

Shule hizo ambazo ni za Buruza, Nabweko, Sambi na Kulazu, ambazo ni za msingi pamoja na shule ya Sekondari ya Irugwa, zimefungwa leo baada ya wanafunzi 22 wa shule za Msingi Nabweko kuambukizwa kipindupindu na watu wengine waliokuwa wanakusmbuliwa na ugonjwa huo. 

Diwani wa kata hiyo ya Irugwa, Juma Msongi ameithibitishia FikraPevu kwamba tangu ugonjwa huo ulipolipuka wiki iliyopita katika baadhi ya maeneo ya Kata hiyo, watu 8 wamefariki na hali inazidi kuwa mbaya kutokana na kukosekana kwa huduma madhubuti. 

Kwa mujibu wa diwani huyo, kutokana na hali ilivyo sasa wananchi wanatakiwa kuzingatia usafi wa mazingira ikiwemo matumizi sahihi ya kutumia vyoo na kujiepusha na ulaji ovyo wa vyakula.
FikraPevu inaendelea kufuatilia tukio hilo kwa karibu na kadri tutakapopata taarifa zaidi tutawataarifu.

WAJENGEWA UWEZO ILI KUFANYA UTAFITI WA HALI YA KIELIMU WILAYANI TARIME KUPITIA MRADI WA UWEZO.

Washiriki wa Semina ya wadau watakaoshiriki katika Utafiti wa Ujifunzaji wa Watoto (Wanafunzi) walio na Umri kati ya Miaka Saba hadi 16 katika Kusoma Kiswahili, Kiingereza na Kufanya Hesabu inayofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime kuanzia leo Septemba 22,2015 hadi kesho Septemba 23, 2015 wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Enock Waitara (Wa pili kushoto Waliokaa) ambae ni Afisa Elimu Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.

Na:Binagi Media Group
Semina hiyo imeratibiwa na Shirika la Maendeleo Tarime SHIMATA chini ya Shirika la TWAWEZA kupitia mradi wake wa UWEZO ambao unafanya tathmini ya Kielimu katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda kwa wanafunzi walio na umri wa miaka Saba hadi 16 katika kujua kusoma Kiswahili, Kiingereza na Kufanya Hesabu.

Baada ya Semina hiyo, Washiriki hao watatembelea shule za Msingi pamoja na Kaya mbalimbali kwa ajili ya utafiti huo na baadae kuwasilisha taarifa yao kwa SHIMATA na baadae TWAWEZA kwa ajili ya kupata tathimini ya hali ya elimu ilivyo Wilayani Tarime. Nchini Tanzania Mradi huo wa UWEZO unajumuisha Wilaya 159.

Akifungua Semna hiyo, Afisa Elimu Wilaya ya Tarime Enock Waitara amewataka washiriki hao kuja na tathimi ya hali halisi ya kielimu Wilayani Tarime na namna ya kufanya ili kupandisha kiwango cha ufaulu kwa kuwa tafiti zilizopita zinaonyesha kuwa hali ya ufaulu kwa shule za msingi siyo nzuri huku akisikitishwa wanafunzi kumaliza darasa la saba na kuijiunga na kidato cha kwanza huku wakiwa hawajui kusoma na kuandika. 
Washiriki wa Semina ya wadau watakaoshiriki katika Utafiti wa Ujifunzaji wa Watoto (Wanafunzi) walio na Umri kati ya Miaka Saba hadi 14 katika Kusoma Kiswahili, Kiingereza na Kufanya Hesabu inayofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime kuanzia leo Septemba 22,2015 hadi kesho Septemba 23, 2015 wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Enock Waitara (Wa pili kushoto Waliokaa) ambae ni Afisa Elimu Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
Washiriki wa Semina ya wadau watakaoshiriki katika Utafiti wa Ujifunzaji wa Watoto (Wanafunzi) walio na Umri kati ya Miaka Saba hadi 14 katika Kusoma Kiswahili, Kiingereza na Kufanya Hesabu inayofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime kuanzia leo Septemba 22,2015 hadi kesho Septemba 23, 2015 wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Enock Waitara (Wa pili kushoto Waliokaa) ambae ni Afisa Elimu Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
Washiriki wa Semina ya wadau watakaoshiriki katika Utafiti wa Ujifunzaji wa Watoto (Wanafunzi) walio na Umri kati ya Miaka Saba hadi 14 katika Kusoma Kiswahili, Kiingereza na Kufanya Hesabu inayofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime kuanzia leo Septemba 22,2015 hadi kesho Septemba 23, 2015 wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Enock Waitara (Wa pili kushoto Waliokaa) ambae ni Afisa Elimu Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
Edward Mulemwa ambae ni Mratibu wa Mradi wa UWEZO Wilayani Tarime akizungumza wakati wa semina
Edward Mulemwa ambae ni Mratibu wa Mradi wa UWEZO Wilayani Tarime akizungumza wakati wa semina
Edward Mulemwa ambae ni Mratibu wa Mradi wa UWEZO Wilayani Tarime akizungumza wakati wa semina
Edward Mulemwa ambae ni Mratibu wa Mradi wa UWEZO Wilayani Tarime akizungumza wakati wa semina
Mwenyekiti wa Shirika la Maendeleo Tarime SHIMATA Joseph Magabe akizungumza wakati semina
Mgeni Rasmi ambae ni Afisa Elimu Wilaya ya Tarime Enock Waitara
Mgeni Rasmi ambae ni Afisa Elimu Wilaya ya Tarime Enock Waitara akifungua Semna
Seemina ikiendelea
Washirki wa Semina
Wshiriki wa Semina
Washiriki wa Semina
Washiriki wa Semina
Chai
Chai
Chai
Muda wa Chai
Mapumziko kwa ajili ya chai
Washiriki wa Semina Wakitokelezea na kamera ya BMG
Kushoto ni Mwanahabari kutoka Sahara Media Group akifanya Mahojiano na Edward Mulemwa ambae ni Mratibu wa Mradi wa UWEZO unaosimamiwa na Taasisi ya TWAWEZA Wilayani Tarime
Kushoto ni Mwanahabari kutoka Sahara Media Group akifanya mahojiano na Mwenyekiti wa Shirika la Maendeleo Tarime SHIMATA Joseph Magabe (Kulia)
Baita Matinyi ambae ni Mratibu kutoka Shirika la Maendeleo Tarime SHIMATA

Jumanne, 22 Septemba 2015

CCM NI CHAMA KINACHOPENDWA TANZANIA, UTAFITI WA TWAWEZA 2015 KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WATHIBITISHA

TAKWIMU zinaonyesha kwamba wananchi hawaelewi nafasi rasmi ya Ukawa
22 Septemba, Dar es Salaam: 
 
Asilimia 62 ya wananchi wanasema kwamba wanajisikia wapo karibu zaidi na chama cha CCM kuliko vyama vingine. 
 
Aidha, walipoulizwa watawachagua wagombea wa chama gani – bila kutajiwa majina ya wagombea – wananchi 6 kati ya 10 walisema kwamba watawachagua wagombea wa CCM kwa Urais (66%), Ubunge (60%) na Udiwani (60%). Takwimu hizi zinatoa picha kwamba CCM inaungwa mkono, kama ilivyokuwa mwaka 2012.

Chadema ni chama cha pili kinachopendwa kushinda vyama vingine vya upinzani. Lakini wananchi wanaosema kwamba watawachagua wagombea wa Chadema kwa Urais, Ubunge na Udiwani wamepungua kidogo. Ikumbukwe kuwa, inawezekana wananchi wanaopenda zaidi mseto wa Ukawa waliunga mkono vyama vya CUF, NCCR-Mageuzi au NLD.

Mbali ya CCM na vyama vinavyounda Ukawa, chama cha ACT-Wazalendo kilitajwa na zaidi ya asilimia moja ya wananchi.

Walipoombwa kutaja moja kwa moja jina la mgombea Urais ambaye wangemchagua, asilimia 65 ya wananchi walimtaja mgombea wa CCM, John Magufuli. Asilimia 25 walimtaja mgombea wa Chadema (na Ukawa), Edward Lowassa. Asilimia 10 iliyosalia iligawanyika kati ya wale waliomtaja mmoja miongoni mwa wagombea urais wengine, waliokataa kujibu na waliokuwa bado hawana mgombea waliyempendelea. Hata hivyo, takwimu zilikusanywa kabla vyama vingine, kikiwemo ACT-Wazalendo, kuteua wagombea wao wa Urais. Takwimu hizi (zilizokusanywa kati ya Agosti na Septemba) sio utabiri wa matokeo ya uchaguzi. Zinaonyesha tu kwamba mwanzoni mwa kipindi cha kampeni, mgombea Urais wa CCM, John Magufuli, alikuwa anaongoza katika kura za maoni.

Aidha, vigezo muhimu vinavyohusu makundi mbalimbali ya watu (demografia) vilitumika kuchambua ni nani au makundi gani yanayowaunga mkono John Magufuli na Edward Lowassa. Wahojiwa ambao walikuwa vijana zaidi, wasomi zaidi, wanaume na wakazi wa mijini, walimuunga mkono Edward Lowassa. Makundi ya wahojiwa wazee zaidi, waliokuwa na elimu ya msingi tu, wanawake na wakazi wa vijijini walielekea kumuunga mkono zaidi John Magufuli kuliko vijana zaidi, wasomi zaidi, wanaume au wanaoishi mijini.

Hata hivyo, katika makundi yote haya, John Magufuli wa CCM anaonekana kuongoza. Kwa mfano, asilimia 33 ya wananchi wenye umri wa 18 – 29 na asilimia 30 ya wenye umri wa 30 – 39 wanamuunga mkono Lowassa, tofauti na asilimia 15 ya watu wenye umri zaidi ya miaka 50. Pamoja na hayo, asilimia 57 ya watu wenye umri wa 18 – 29 na asilimia 76 ya watu wenye umri wa 30 – 39 wanamuunga mkono Magufuli. Upande wa makazi, asilimia 28 ya wakazi wa mijini walimuunga mkono Edward Lowassa tofauti na asilimia 24 ya wakazi wa vijijini. Asilimia 66 ya wakazi wa vijijini na asilimia 61 ya wakazi wa mijini wanamuunga mkono John Magufuli.

Asilimia 26 ya wanaomuunga mkono John Magufuli walidai kwamba ni kwasababu yeye ni mchapakazi, na asilimia 12 ya wanaomuunga mkono Edward Lowassa walisisitiza kwamba anaweza kuleta mabadiliko yanayohitajika nchini. Izingatiwe kwamba kauli hizi zinafanana karibu neno kwa neno na kauli mbiu za kampeni za wagombea hawa wawili.

Hata hivyo, wananchi hawana taarifa sahihi juu ya nafasi rasmi ya Ukawa kama mseto. Asilimia 49 ya wananchi wanafikiri kwamba Ukawa ni chama cha siasa kilichosajiliwa, kinyume na hali halisi. Asilimia 57 wanafikiri kwamba neno ‘Ukawa’ litakuwepo kwenye karatasi zao za kupigia kura. Hii pia, sio kweli. Bila kampeni na juhudi za kuwaelimisha wapiga kura ili wawe na taarifa sahihi kuhusu jambo hili, hali hii inaweza kuleta wasiwasi siku ya uchaguzi. 

Matokeo haya yalitolewa na Twaweza katika muhutasari wa utafiti mwenye jina la Sema mwananchi, sema | Maoni ya wananchi kuhusu uongozi wa kisiasa. Muhtasari huu umetumia takwimu kutoka Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika unaotumia simu za mkononi na wenye uwakilishi wa taifa zima. Matokeo yanatokana na Awamu ya 1 ya kuwapigia simu wahojiwa wapya 1,848 iliyoendeshwa kati ya Agosti na Septemba 2015. 
 
Wahojiwa waliteuliwa kwa kutumia njia kama zinavyotumika na asasi za utafiti duniani kote. Unasibu (sampling) huu ulifanyika katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Takwimu hizi zimelinganishwa na zile za awamu za utafiti katika miaka ya nyuma, zikiwemo:
  • Utafiti wa awali wa kwanza wa Sauti za Wananchi 2012
  • Sauti za Wananchi Awamu ya 10 ya Octoba 2013
  • Sauti za Wananchi Awamu ya 24 ya Septemba 2014
  • Awamu za utafiti za Sauti za Wananchi Aprili-Julai 2015
  • Utafiti mpya wa awali ulioendeshwa kati ya Julai na Agosti 2015

Twaweza ilibaini kuwa zoezi jipya la kuwaandikisha wapiga kura lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa. Asilimia 98 ya wahojiwa waliripoti kwamba wameshajiandikisha chini ya mfumo mpya wa Biometric Voter Registration (BVR). Hata hivyo, wananchi wengi walikumbwa na changamoto nyingi katika mchakato huo. Asilimia 68 ya wananchi walitaja urefu wa foleni za kujiandikisha kama tatizo kuu.
 
 Asilimia 51 walisema walisubiri au walishuhudia wananchi wengine wakisubiri muda wa zaidi ya masaa sita kabla ya kujiandikisha. Aidha asilimia 37 waliona au wao wenyewe walipa matatizo ya kusukumana kwenye foleni. Mashine za BVR kushindwa kufanya kazi ipasavyo kuliripotiwa na asilimia 26 ya wananchi. Upendeleo kwenye vituo vya kujiandikisha uliripotiwa na asilimia 19. Ukosefu wa uzoefu wa BVR ulilalamikiwa na asilimia 16 ya wananchi.

Pamoja na kujiandikisha kupiga kura, asilimia 99 ya wananchi walisema kwamba wanadhamiria kupiga kura katika uchaguzi wa mwaka huu. Hata hivyo, izingatiwe kwamba asilimia 79 ya wahojiwa hawa walidai pia kwamba walipiga kura wakati wa uchaguzi wa 2010 wakati hali halisi inaonesha kuwa waliopiga kura walikuwa asilimia 43 tu. Aidha, ni asilimia 57 tu ya wananchi ndio walioweza kutaja tarehe sahihi ya uchaguzi, yani Oktoba 25. Takwimu hizi zinaonyesha kwamba mara nyingi kuna tofauti kati ya majibu ya watu wakati wa kura za maoni au tafiti mbalimbali, na vitendo vyao halisi.

Asilimia 64 ya wananchi walisema kwamba wanakumbuka vyema ahadi zilizotolewa na Wabunge wao katika uchaguzi uliopita, na asilimia 86 kati ya hao walisema kwamba mbunge wao hakutekeleza ahadi hizo au alizitekeleza chache.

Aidha, wananchi waliorodhesha changamoto kuu walizoona hapa nchini. Kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma, huduma za afya ni changamoto kwa asilimia 59 ya Wananchi, ukosefu wa maji ikitajwa na asilimia 46, elimu duni na asilimia 44, na umaskini, asilimia 39. Hata hivyo, kumekuwa na mabadiliko kadhaa. Watu wachache zaidi walitaja umaskini (wamepungua kutoka asilimia 63 mwaka 2014) na watu wengi zaidi walitaja maji (wameongezeka kutoka asilimia 27 mwaka 2014).

“Kuna mambo kadhaa ya kuzingatia hapa,” alisema Aidan Eyakuze, Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza. “Wananchi wanabadilisha mawazo kuhusu vipaumbele vyao. Waliweka kipaumbele kwa afya badala ya umasikini katika kipindi kifupi cha miezi 12.”

“Watu wana hamu kubwa sana ya kupiga kura” aliongeza, “lakini hali hii si kigezo cha kuaminika katika kutabiri wangapi kweli watapiga kura siku ya uchaguzi. Wakijitokeza kwa wingi, itaipa uhalali mkubwa serikali ya awamu ijayo. Wakijitokeza wachache, inaweza kuashiria ama hali ya wananchi kukata tamaa, au hali ya kujiamini kwamba tayari wameshinda, au hali zote mbili kwa pamoja.”

“Kwa pamoja, mambo haya mawili yanatoa picha kwamba huenda wapiga kura wakawa hawana uhakika wamchague nani. Yanaimarisha ujumbe kwamba mashindano haya ndio kwanza yameanza kupamba moto. Wagombea hawana budi kuimarisha mahusiano yao na wapiga kura wakiwa na malengo mawili makuu; Lengo la kwanza ni kunadi ubora wa ilani na sera zao. Lengo la pili ni kuhakikisha kwamba watajitokeza kwa wingi kuwapigia kura siku ya uchaguzi, Oktoba 25.”

BAJAJI NA BASI VYAUA WATU MBEYA



KATIKA TUKIO LA KWANZA: 

WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ABILAH PHILIMON (17) MKAZI WA ILEMI, DEREVA WA BAJAJI NA 2. BARAKA SELEMANI (23) MKAZI WA SIMIKE WALIFARIKI DUNIA BAADA YA BAJAJI YENYE NAMBA ZA USAJILI MC 276 APL ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA MAREHEMU KUGONGA GARI  T.588 AMR AINA YA MITSUBISHI FUSO ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA EMANUEL FRANSIS (35).

AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 21.09.2015 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO KIJIJI CHA HATWELO, KATA YA HATWELO, TARAFA YA TEMBELA, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.

AIDHA KATIKA AJALI HIYO, WATU SITA KATI YAO WANAUME WATANO NA MWANAMKE MMOJA WALIJERUHIWA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA BAJAJI. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA, MAJERUHI WAMELAZWA HOSPITALINI HAPO.


KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA MKAZI WA TEWELE – NAKONDE –ZAMBIA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FRAID AINKALA (67) AFARIKI DUNIA BAADA YA BAJAJI YENYE NAMBA ZA USAJILI MC 630 AFC IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 21.09.2015 MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO KIJIJI CHA NKANGAMO, TARAFA YA NDALAMBO, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA, BARABARA KUU YA TUNDUMA/SUMBAWANGA.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO, WATU WAWILI WALIJERUHIWA AMBAO NI 1. MAGRETH MTAMBO (52) NA 2. ANASTAZIA NYAMUNGALA (55) WOTE WAKAZI WA KAKOZI –NAKONDE – ZAMBIA.  CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA NA MAJERUHI WAMELAZWA KITUONI HAPO.




KATIKA TUKIO LA TATU:
MTU MMOJA AMBAYE BADO KUFAHAMIKA JINA LAKE, TINGO WA BASI MALI YA KAMPUNI YA SAI BABA AFARIKI DUNIA BAADA YA BASI HILO LENYE NAMBA ZA USAJILI T.668 BLD AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIKITOKEA DAR ES SALAAM KUELEKEA SUMBAWANGA KUGONGA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.771 ATV/T.771 AUU SCANIA LORI ILIYOKUWA IMEEGESHWA BAADA YA KUHARIBIKA ENEO LA MLIMA NYOKA.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 21.09.2015 MAJIRA YA SAA 22:00 USIKU HUKO ENEO LA MLIMA NYOKA, KATA YA NSALAGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/NJOMBE.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO, ABIRIA WAWILI AMBAO PIA MAJINA YAO BADO KUFAHAMIKA WALIJERUHIWA NA WOTE WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA BASI HILO. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA/MICHORO NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA WA BASI LA SAIBABA AZITOE ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.

Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...