Afisa Habari Mamlaka ya Majisafi na
usafi wa mazingira Jijini Mbeya, Neema Stantoni akizungumza na kalulunga
blog ofisini kwake.
Akifafanua jambo....
Akifafanua jambo....
TAASISI za
serikali mkoani Mbeya, zinaongoza kwa kukwepa kulipia huduma za maji, hivyo
kukwamisha tija ya uboreshaji wa usambazaji wa maji kwa wananchi mkoani hapa.
Mamlaka ya
maji safi na usafi wa Mazingira Jijini Mbeya (MBEYA-UWSA) imesema imekuwa
kwenye changamoto kubwa, ingawa taasisi hizo zimekuwa zikipewa fedha na
serikali ya kulipia huduma hiyo.
Afisa habari
wa Mamlaka hiyo, Neema Stantoni, ameeleza kuwa, taasisi hizo
zinadaiwa kiasi cha Tsh. Mil. 466,899,942.
Alisema
tayari mamlaka hiyo imeanza zoezi la kuwakatia maji wateja wote ambao wanadaiwa
na kwamba wateja zaidi ya Elfu mbili wamekatiwa maji.
‘’Tunahudumia
wateja wa aina Nne, wakiwemo wa majumbani, Viwandani, biashara na taasisi za
serikali ambapo wateja wanaoongoza kulipa vizuri ni wateja wa viwandani ambao
wanalipa kwa wakati’’ alisema Neema.
Kati ya
taasisi ambazo zinadaiwa ni pamoja na maeneo ya Afya, Magereza na Polisi ambapo
imeelezwa kuwa taasisi hizo zikikatiwa maji kunauwezekano wa kutokea milipuko
ya magonjwa kikiwemo kipindupindu.
Afisa habari huyo amezitaka taasisi za
serikali kulipa deni hilo hata kwa kupunguza, vinginevyo zoezi la kukata maji
linaweza kuzikumba.
‘’Kwasababu
Mamlaka na wateja tunategemeana ambapo mteja akilipa anasaidia matengenezo ya
mabomba yanayopasuka, kununua dawa za kutibu maji na kulipia umeme ambao
unasaidia kusukuma mashine kisha wateja kupata maji’’ alisema Neema Stantoni.
Alizitaja
changamoto zinazoikabili mamlaka hiyo kwa sasa kuwa ni pamoja na baadhi ya
wateja kuiba maji kwa kuchepusha kabla ya mita, kubonda mita kwa lengo la kuiba
maji na kutoa mita kisha kuchota maji.
Zoezi la
kuwakatia maji wateja wote ambao hawajalipa kuanzia mwezi mmoja, amesema
linaendelea nyumba kwa nyumba, wateja wa biashara yakiwemo mahotel kisha
taasisi kwa taasisi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni