Jumatano, 30 Julai 2014

MBEYA CEMENT YAWEKA MKONO UJENZI WA UWANJA WA KISASA WA MICHEZO CHUNYA MBEYA


Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro akikabidhiwa mifuko ya saruji na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya saruji ya Lafarge ya SONGWE mkoani Mbeya ikiwa ni sehemu mifuko 1000 iliyotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo wilayani Chunya.


 

UWANJA wa kisasa wa michezo utakaogharimu jumla ya sh. Bilioni 8, umeanza kujengwa wilayani Chunya Mkoani Mbeya.
 
 
Uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 50,000 pia unatarajiwa kuwa kitega uchumi cha aina yake kuwepo katika wilaya ya Chunya na mkoa wa Mbeya na katika wilaya za mikoa mingine nchini mbali na Jiji la Dar es salaam.
 
 
Akizungumzia ujenzi wa uwanja huo Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro alisema kuwa uwanja huo unajengwa na wananchi wenyewe kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya hiyo ambapo pendekezo la ujenzi wa uwanja huo aliliwasilisha kwenye vikao vya halmashauri na kuridhiwa na baraza la Madiwani.
 
 
Alisema katika vikao vyake, ambapo Halmashauri ya wilaya hiyo ilipendekeza kutenga Sh. Milioni 70 katika bajeti yake ya kila mwaka huku kila mwananchi akiwajibika kuchangia ujenzi wa uwanja huo kuanzia sh.2000 kwa kila mwaka ambapo matazamio uwanja huo unatarajia kukamilika 2016.
 
 
Katika mkakati wa ujenzi huo Kinawiro alisema kuwa wadau mbalimbali wamejitokeza kuchangia ujenzi wa Uwanja huo ambao upo katika hatua za awali wakiwemo Kampuni ya Lafarge inayozalisha saruji aina ya Tembo waliochangia saruji mifuko 1000.
 
 
Akizungumza wakati wa kuchangia ujenzi wa uwanja huo Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Lafarge Catherine Langreney alisema kuwa kampuni yake imepokea maombi hayo kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Chunya na kukubali kuchangia saruji mifuko 1000.
 
 
Langreney alisema kuwa mbali na kufanya biashara kampuni yake inachangia huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi waliopo maeneo ya karibu na kiwanda chao hivyo msaada huo ni sehemu ya huduma zao za kawaida kwa wananchi.
 
 
‘’Huduma zetu zinazingatia mahitaji ya jamii inayotuzunguka bila kujali faida,’’alisema Langreney.
 
 
Alibainisha kuwa kuwepo kwa uwanja huo kutatoa fursa ya ajira kwa wananchi wa maeneo hayo na kuinua uchumi wao.
 
 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya  Wilaya ya Chunya Sophia Kumbuli alisema kuwa uwanja huo utakuwa ni sehemu ya Mapato ya Halmashauri hiyo na kuwa wadau mbalimbali wamejitokeza kuchangia uwanja huo kwa nguvu zao na mali zao.
 
 
Alisema kuwa fursa ya kuwepo kwa uwanja huo wa kisasa itainua michezo ndani ya wilaya hiyo na mkoa wa Mbeya kwa ujumla hivyo wadau wanapaswa kujitokeza kuchangia maendeleo ya uwanja huo.
 
 
Naye Katibu wa Kamati ya Ujenzi wa uwanja huo Solo Tuyagaje alisema kuwa hadi sasa jumla ya sh. Milioni 107 zilichangwa na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na makampuni yanayochimba madini wilayani humo na wachimbaji wadogo.
 
 
Alisema wadau wengine waliochangia ni pamoja na Mbunge wa Lupa Victor Mwambalaswa aliyechangia jumla ya Milioni 11 ambapo Halmashauri ya wilaya imechangia jumla y ash. Milioni 30 kwa mwaka wa fedha wa 2013/14.
 
Credit;mkwinda blog

Jumanne, 29 Julai 2014

NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Simu: 022-2110146/2110150/2, 211679, Faksi: 022-2113271, Tovuti: www.moe.go.tz
NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015
UTANGULIZI
Moja ya mikakati ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika kuandaa walimu mahiri ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti ni wale wenye ufaulu mzuri katika mtihani ya kidato cha NNE. Ili kufanikisha azma hii, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itadahili wanafunzi wenye ufaulu wa Daraja la Tatu kwa ajili ya Cheti na wenye ufaulu wa alama 26 au 27 (mwaka 2004 hadi 2012) na alama 33 au 34 (mwaka 2013) watadahiliwa katika programu ya mafunzo kabilishi ya mwaka mmoja.
Aidha, kipaumbele katika udahili kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo ya Sayansi, Hisabati, English na Kiswahili. Watakaojiunga na mafunzo ya ualimu na kufaulu mafunzo yao watapatiwa ajira moja kwa moja kulingana na taratibu za Serikali.
VIGEZO
Vigezo vifuatavyo vitatumika kuchagua wanachuo wa kujiunga na mafunzo ya ualimu mwaka 2014/15.
1:
MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA CHETI DARAJA ‘A’: MUDA MIAKA 2
(i)    Cheti Ualimu wa kawaida katika vyuo vya Ilonga, Kabanga, , Kitangali, Mandaka , Murutunguru , Ndala , na Tarime
(ii)  Cheti Ualimu Elimu ya Awali katika vyuo vya Kabanga, Kinampanda, Mhonda, Mtwara (U), Singachini, Tandala, Tarime
(iii) Cheti Ualimu Elimu kwa michezo katika vyuo vya Ilonga, Tarime, Ndala na Mtwara (U)
Mwombaji awe:
Mhitimu wa Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 mwenye ufaulu wa kiwango kisichopungua Daraja la III katika Mtihani uliofanyika katika kikao kimoja.
2:
MAFUNZO KABILISHI NGAZI YA CHETI (BRIDGING COURSE) KWA AJILI YA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI:- MUDA MWAKA 1
Mafunzo katika vyuo vya ualimu Bustani, Kinampanda, Mhonda, Mpuguso, Mtwara (U), Nachingwea, Singachini, Tandala, Katoke na Sumbawanga
Mwombaji awe:
(i)             Amehitimu wa Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 hadi 2012 na awe amefaulu kwa kiwango kisichopungua Daraja la IV kwa alama 26 au 27 (kwa mtihani wa mwaka 2004 hadi 2012) na alama 33 au 34 (mtihani wa mwaka 2013) kwa mitihani iliyofanyika katika kikao kimoja; na
(ii)           Mwenye ufaulu wa angalau kiwango cha D katika masomo ya Sayansi, Hisabati, English na Kiswahili katika Mtihani wa Kidato cha IV.
Tanbihi: Watakaofaulu mtihani wa mafunzo kabilishi wataendelea na mwaka wa pili wa mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti Daraja A
3:
ELIMU MAALUM: MIAKA 2 katika chuo cha Patandi:-
Mwombaji awe:
(i)        Mwalimu wa Daraja ‘A’ mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
(ii)      Mwenye ufaulu angalau somo moja la Sayansi katika Mtihani wa Kidato cha IV.
Tanbihi:Walimu wanaofundisha Elimu Maalum hata kama hawana mafunzo maalumu ni sifa ya nyongeza (uthibitisho uambatishwe).
MAELEZO MUHIMU
(i)            Vigezo vilivyoelekezwa kwa waombaji wa mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti ni kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali;
(ii)          Muombaji wa chuo cha ualimu cha Serikali anatakiwa kuchagua vyuo visivyopungua vitano ambavyo angependa kujiunga navyo akianzia kile anachokipendelea zaidi;
(iii)         Wahitimu Kidato cha IV mwaka 2013 waliojaza nafasi ya mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti Daraja ‘A’ kwenye ‘Selforms’ wakati wanamaliza Elimu ya Sekondari wanatakiwa kuomba upya mafunzo hayo;
(iv)          Waombaji wa mafunzo ya Ualimu walioajiriwa watakaopatiwa nafasi za mafunzo watapaswa kupata ruhusa (Release) kutoka kwa waajiri wao;
(v)           Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Serikali yatatolewa kwenye Tovuti za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz), OWM-TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz) na NACTE (www.nacte.go.tz)
(vi)         Waombaji watakaochaguliwa watatumiwa barua za kujiunga na mafunzo na Wakuu wa vyuo vya Ualimu watakakokuwa wamepangwa kupitia anuani zao;
(vii)        Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara: www.moe.go.tz, OWM TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz na NACTE: www.nacte.go.tz na kwenye ofisi za Makatibu Tawala (M) na vyuo vya ualimu.
Namna ya kutuma maombi:
a)    Waombaji watume maombi yao kwa njia ya MTANDAO (online application) kupitia tovuti zifuatazo: www.moe.go.tz  AU  www.nacte.go.tz

Maombi kwa njia ya mtandao yataambatana na ada ya shilingi 10,000 itakayolipwa kwa kutumia MPESA. Maelekezo ya kina kuhusu namna ya kutuma maombi kwa njia ya mtandao yanapatikana katika tuvuti ya wizara www.moe.go.tz na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi www.nacte.go.tz
Malipo ya maombi yanaweza kufanyika kupitia MPESA kama ifuatavyo:
1.       Piga *150*00#
2.      Chagua 4. (Lipa kwa MPESA);
3.      Chagua 1. (Weka LIPA Namba);
4.      Weka LIPA Namba (ingiza namba 607070);
5.      Ingiza kiasi (ingiza kiasi cha 10,000.00);
6.      Weka Enter Reference No. ( ingiza 1234);
7.      Weka namba ya SIRI (ingiza namba yako ya siri); na
8.      Ingiza 1 kuthibibitisha malipo.
AU
b)    Barua kwa:
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
S.L.P. 9121
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)

Jumapili, 20 Julai 2014

UMEME KUTUA VIJIJINI, MKOANI RUVUMA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akielekea eneo la jukwaa mara baada ya kuwasili katika eneo palipofanyika uzinduzi wa mradi wa kusambaza umeme vijijini unaosimamiwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) wilaya ya Nyasa mwishoni mwa wiki, kushoto kwake ni Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo.

Meneja wa Shirika la umeme nchini, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi,   Bi Salome Nkondola akiwasilisha taarifa fupi ya utekelezaji wa miradi ya umeme kwa mkoa wa Ruvuma mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete.

Rais Jakaya M. Kikwete akichukua mkasi kwa ajili ya kukata utepe tayari kuelekea katika eneo la uzinduzi wa mradi wa usambazaji wa umeme wilayani Nyasa mkoa wa Ruvuma, kulia kwake ni Waziri mwenye dhamana na nishati Prof. Sospeter Muhongo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete pamoja na viongozi wa serikali wakiwepo Waziri wa Ardhi na maendeleo ya Makazi, Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Ujenzi wakiwa wameshika utepe tayari kwa Rais kuukata na kuelekea kubonyeza kitufe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi huo wa umeme.

Rais akifunua kitambaa mahali palipowekwa kitufe kwa ajili ya uzinduzi rasmi
Rais akifunua kitambaa mahali palipowekwa kitufe kwa ajili ya uzinduzi rasmi
Rais akibonyeza kitufe
Rais akifurahia uzinduzi mara baada ya zoezi hilo kukamilika
Burudani wakati wa sherehe hizo.
 
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amezindua mradi wa kusambaza umeme vijijini unaosimamiwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) utakaowanufaisha wakazi wa Mkoa wa Ruvuma utakaochangia kuongeza kasi ya maendeleo vijijini. 
 
 Rais Jakaya Kikwete yuko katika  ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo katika mkoa huo lengo likiwa ni kutimiza azma ya serikali ya kuwa kila mwananchi anapata huduma ya nishati ya umeme. 
 
 Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo amewahakikishia wakazi hao kwamba hadi ifikapo mwezi Novemba mwaka huu vijiji vyote vilivyoko katika mradi wa kusambaza umeme vijijini awamu ya II watakuwa tayari wanatumia nishati hiyo kwa wale watakao wamemudu gharama ya Shilingi Elfu Ishirini na Saba ya kuunganishiwa nishati hiyo. 
 
 Imeelezwa kwamba mradi wa usambazaji wa umeme vijijini katika mkoa wa Ruvuma utagharimu kiasi cha Tsh. 26.53 bilioni zitakazohusisha ujenzi wa njia za umeme zenye msongo wa kilovolti 33 zenye jumla ya urefu wa km 538, ujenzi wa njia ya umeme msongo wa kilovolti 11 yenye urefu wa km 23, ujenzi wa njia ya umeme msongo wa kilovoti 0.4 yenye urefu wa km 272, ufungaji wa transfoma 129 za ukubwa mbalimbali pamoja na kuunganisha wateja 7,488. 
 
 Mradi huu utatekelezwa na kampuni ya Lanka Transfomers Limited, (LTL) ya nchini SRILANKA kwa mkoa wa Ruvuma. Mradi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni 2015 na kunufaisha wakazi wa wilaya za Songea, Tunduru, Mbinga na Nyasa. 
 
 Pamoja na uwepo wa mradi huo pia kuna mradi wa kuongeza nguvu ya umeme kwenye wilaya za Mbinga na Tunduru unaotekelezwa na kampuni ya Taikai Co.Ltd ambapo tayari amekamilisha survey ya vituo vyote na ameshawasilisha transifoma ya kituo cha Tunduru. 
 
 Prof. MUHONGO amesema mradi wa kuongeza nguvu ya umeme utagharimu kiasi cha pesa za kitanzania Shilingi bilioni 2.27 zitakazohusisha ujenzi wa vituo viwili vya kuongeza nguvu ya umeme kutoka kilovoti 11 hadi kufikia kilovoti 33 kwa ajili ya kufikisha umeme katika vijiji vilivyoko mbali. 
 
Vituo hivyo vitakuwa na transifoma zenye uwezo wa kilowati 3,000 (3.0MW) kila kimoja. Kwa upande wake Mbunge wa MBAMBABAY Captain JOHN KOMBA ameishukuru serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama hicho ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara hasa madaraja, kuwawekea umeme, na kupandishwa hadhi kituo cha afya na kuwa hospitali ya wilaya. 
 
 Miradi ya REA awamu ya II imeanza kutekelezwa rasmi Novemba 2013 na inatakiwa kukamilika ifikapo Juni2015 kwa nchi nzima hivyo kuchangia katika kuongeza kiasi cha wananchi waliofikiwa na huduma ya umeme kufikia asilimia 30. 
 
CREDIT;Michuzi blog

NDOO ZA MSUMBIJI MARUFUKU KUNUNULIA MPUNGA KYELA

NDOO zinazotoka nchini Msumbiji, zimepigwa marufuku kununulia mpunga katika kata ya Ipande,wilayani Kyela mkoani Mbeya, kutokana na ndoo hizo kuwa na ujazo mkubwa.

Marufuku hiyo imepgwa na Halmashauri ya  Chama Cha Mapinduzi(CCM), Ipande, na kwamba atakayekutwa akinunulia ndoo hizo au kuwapeleka watu kununua mpunga kwa kutumia ndoo hizo, atatozwa faini ya Tsh.20,000/=

Diwani wa kata hiyo, Steven Mwangalaba, amethibitisha na kwamba, wao hawakatazi mtu kununua mpunga wala kuuza, bali wanazikataa ndoo hizo kwasababu zinawanyonya wakulima.

Jumanne, 15 Julai 2014

MBUNGE VITI MAALUM MKOA WA MBEYA, DR.MARY MWANJELWA, ATIMIZA AHADI YA VIJANA WALIOMUOMBA JEZI NA MIPIRA ISYESYE MBEYA MJINI

 MBUNGE viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr, Mary Mwanjelwa, akifurahia jambo na kocha mkuu wa timu ya Isyesye FC, Steve Kasalila (KULIA) na Katibu wa wanawake wa CCM kata ya Isyesye, Zainab Kessy(KULIA).
 MBUNGE viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr, Mary Mwanjelwa, akifunga gori la penalti, na kumwacha mlinda mlango wa timu ya Isyesye.


 MBUNGE viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr, Mary Mwanjelwa, akimkabidhi kocha mkuu wa timu ya Isyesye Jijini Mbeya,Steve Kasalila, jozi ya jezi na mipira mitano leo.

 MBUNGE viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr, Mary Mwanjelwa, akihutubia wananchi na wachezaji wa timu ya Isyesye na Veta leo jioni, katika uwanja wa Isyesye, Vingunguti Relini Jijini Mbeya, wakati wa kukabidhi jozi moja ya jezi na mipira mitano kwa timu ya Isyesye Jijini Mbeya.

 MBUNGE viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr, Mary Mwanjelwa, akihutubia wananchi na wachezaji wa timu ya Isyesye na Veta leo jioni, katika uwanja wa Isyesye, Vingunguti Relini Jijini Mbeya, wakati wa kukabidhi jozi moja ya jezi na mipira mitano kwa timu ya Isyesye Jijini Mbeya.

 Mweyekiti wa UVCCM Mbeya Mjini, Maranyingi Matukuta, akifungua jezi, wakati wa MBUNGE viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr, Mary Mwanjelwa, akihutubia wananchi na wachezaji wa timu ya Isyesye na Veta leo jioni, katika uwanja wa Isyesye, Vingunguti Relini Jijini Mbeya, kisha kukabidhi jozi moja ya jezi na mipira mitano kwa timu ya Isyesye Jijini Mbeya.
 Akipokea bahasha kutoka kwa machifu wa eneo la Isyesye, Jijini Mbeya leo.


 MBUNGE viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr, Mary Mwanjelwa, akisalimiana na wachezaji wa timu ya VETA NA ISYESYE Jijini Mbeya, eneo la uwanja wa vingunguti Relini Jijini Mbeya, wakati wa kukabidhi jozi moja ya jezi na mipira mitano kwa timu ya Isyesye Jijini Mbeya.




MBUNGE viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr, Mary Mwanjelwa, akipiga penlti kwa ustadi mkubwa, baada ya kuhutubia wananchi na wachezaji wa timu ya Isyesye na Veta leo jioni, katika uwanja wa Isyesye, Vingunguti Relini Jijini Mbeya, na kukabidhi jozi moja ya jezi na mipira mitano kwa timu ya Isyesye Jijini Mbeya.

MORAVIAN JIMBO LA KUSINI MAGHARIBI, WACHUNGAJI WATAKA KUFUNGA OFISI, SERIKALI YANUSURU.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla akiongea na baadhi ya wachungaji na waumini wa kanisa la Moravian kuwaomba wafunguo ofisi hizo ili mazungumzo yafanyike



 Mmoja wa wachungaji hao, Edward Chilale akiongea na Baadhi ya waandishi wa habari

Makamu Mwenyekiti jimbo hilo, Sichone, alisema kuwa amesikitishwa na kitendo kilichofanywa na kundi hilo ndani ya kanisa kwa kuwa kimeenda tofauti na taratibu za kanisa, ambapo mambo yote hufanywa kupitia vikao.




Moja ya waumini wa kanisa hilo akifungua mnyororo uliofungwa ofisini kwa Askofu 



HALI si shwari katika Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi kufuatia mgogoro wa muda mrefu ambapo safari hii baadhi ya waumini na wachungaji walitaka kufunga ofisi za Jimbo hilo wakishinikiza kujiuzulu kwa Askofu, Alinikisa Cheyo.
Tukio la kufunga ofisi za Jimbo hilo limetokea leo majira ya saa 12 asubuhi  ambapo baadhi ya Wachungaji na waumini wa kanisa hilo walifika katika makao makuu ya Jimbo yaliyoko Jakaranda jijini Mbeya wakiwa na makufuri yao.
Kanisa la Moraviani Tanzania, jimbo la kusini Magharibi kwa zaidi ya mwaka mmoja limekuwa katika mgogoro wa kiuongozi, baada ya kamati tendaji (KTM-JKM) kumsimamisha Mwenyekiti aliyechaguliwa kihalali kupitia mkutano Mkuu (Sinod), Nosigwe Buya, kwa madai ya kushindwa kulisimamia kanisa na kumpandisha aliyekuwa Makamu wake, Zacharia Sichone, jambo lililoibua mpasuko.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla King ndiye aliyenusuru kufungwa kwa kanisa hilo  baada ya kuwasihi wachungaji na Waumini wenye jazba kuwa na subira wakati Serikali ikijaribu kuona namna ya kutatua mgogoro huo.
Akizungumza na kundi hilo, Prof. Sigalla aliyefika eneo hilo majira ya saa 3:20 aliwaomba wachungaji hao, kusitisha azima yao hiyo ya kuzifunga ofisi za Makao Makuu ya kanisa na kuwa na subira kwani siku inayofuata  serikali ingetoa msimamo juu ya mgogoro huo.
Akizungumza baada ya kukubali ombi la Mkuu wa Wilaya, mmoja wa wachungaji hao, Edward Chilale, alisema wamefika hatua hiyo baada ya Askofu Mkuu wa kanisa hilo,kupuuza madai yao ya kutaka kuitishwa kwa Mkutano Mkuu wa kanisa (Sinod) utakaoamua hatima ya mgogoro baada ya kusimamishwa kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa jimbo hilo, Mwenyekiti Buya.
Mchungaji Chilale alisema licha ya kuheshimu kauli ya serikali ya kutaka kusitisha mpango wao wa kulifunga kanisa, bado shinikizo lao la kutaka Askofu Cheyo kujiuzulu bado liko palepale, kwani yeye ndio chanzo cha yote.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti jimbo hilo, Sichone, alisema kuwa amesikitishwa na kitendo kilichofanywa na kundi hilo ndani ya kanisa kwa kuwa kimeenda tofauti na taratibu za kanisa, ambapo mambo yote hufanywa kupitia vikao.
Alisema tayari wametoa taarifa jeshi la polisi na kwamba tukio hilo liliongozwa na wachungaji sita wa ushirika wa Bethlehemu ambalo kwa muda mrefu limekuwa likiendesha mambo kinyume na taratibu za kanisa.
Wachungaji hao pamoja na kukubali kufungua ofisi waliweka misimamo yao ambayo Miongoni mwa maazimio hayo ni kuutaka uongozi huo wa kanisa kubatilisha mara moja maamuzi yake ya kumsimamisha kazi Mwenyekiti huyo na asibughudhiwe hadi Mkutano Mkuu wa Sinodi.
Pia waliitaka halmashauri kuu iwe imeitisha Mkutano Mkuu wa Sinodi  Machi 3 mwaka huu na kwamba isipotii maazimio hayo ya wakristo watachukua hatua ya kuzifunga ofisi zote za jimbo na kufanya maandamano ya amani kwa kibali cha vyombo vya dola.



Credit; mbeya  yetu

PROF;MWANDOSYA AKUTANA NA UONGOZI WA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA LEO MBEYA


Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Mbeya University of Science and Technology-MUST) (Chancellor),Profesa Mark Mwandosya (kulia) akiwa kwenye mkutano na uongozi wa Chuo hicho ofisini kwake Ikulu,Dar es Salaam.Ujumbe huo,ukiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo umempa taarifa Mkuu wa Chuo kuhusu maendeleo ya Chuo, changamoto zinzokikabili,na mipango ya kukiimarisha Chuo kifedha,kitaaluma,na miundombinu yake.

credit;michuzi blog

Jumatatu, 14 Julai 2014

PROF. SIGALLA; DR. MWANJELWA ANAO UWEZO WA KIUONGOZI

 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akikaribishwa leo na wanawake katika ukumbi wa OTTU Mbeya, kwa ajili ya ufunguzi wa semina ya ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla.
 Wanawake hoyeee. Kulia ni mgeni rasmi, mkuu wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla.
 Baadhi ya washiriki ukumbini.
 Mwandaaji wa semina hiyo ya stadi za uongozi. Dr. Mary Mwanjelwa, akisema neno..
 Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla, akifungua semina ya wanawake, kuhusu stadi za uongozi Jijini Mbeya, katika ukumbi wa OTTU, ambapo wanawake kutoka wilaya tisa za mkoa wa Mbeya, walihudhuria.
 Mmoja wa watoa mada katika semina hiyo, Tumaini Mwakatika, akisema neno mbele ya kamera ya TBC1.
 Kulia ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akipongezwa  na Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla, kwa kuandaa semina ya stadi za uongozi kwa wanawake wa wilaya tisa za mkoa wa Mbeya.
MKUU wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla,  amewaasa wanawake nchini, kuacha kudharauliana ili waweze kufikia nafasi ya hamsini kwa hamsini katika uongozi.
 

Ameyasema hayo jana, alipofungua semina ya wanawake kutoka wilaya zote za mkoa wa Mbeya, iliyoandaliwa na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, MNEC, Dr, Mary Mwanjelwa, kuhusu stadi za uongozi na mbinu za kufanikiwa kisiasa ndani ya vyama vingi.



Prof. Sigalla, alisema kuwa, wanawake wengi wanashindwa kuchaguliwa kwenye nafasi mbalimbali kutokana na kutopendana na kutosimamisha mwanamke shupavu.



“Mkimsimamisha mwanamke kama Dr. Mwanjelwa, hata mimi nitamchagua siyo kwasababu ni mwanamke, bali kwasababu anao uwezo wa kuongoza na mwonekano’’ alisema Prof. Sigalla.



Mwandaaji wa mafunzo hayo, Dr. Mary Mwanjelwa, alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa wanawake, maana ukimwezesha mwanamke umewezesha jamii nzima.



“Mwanzo semina kama hii niliwaandalia madiwani wanawake wote wa mkoa wa Mbeya kisha na madiwani wanaume na sasa viongozi hawa ngazi ya matawi na kata ambao naamini watapeleka elimu watakayoipata kwa jamii’’ alisema Dr. Mwanjelwa.



Mmoja wa wawezeshaji wa semina hiyo ambayo inahusu mada ya stadi za uongozi na mbinu za kufanikiwa kisiasa ndani ya demokrasia ya vyama vingi, Tumaini Mwakatika, alisema kuwa semina hiyo ya siku tatu, itawawezesha wanawake hao kutambua mambo ya msingi katika uongozi.



“Watapata kujua changamoto za uongozi, nadharia ya uongozi na tabia za viongozi, mambo ya msingi katika uongozi na misingi ya utawala wa kidemokrasia na matarajio ya wananchi”alisema Tumaini Mwakatika.



Baadhi ya washiriki akiwemo Everada Mwangwala na Agatha Ngole, walisema kuwa, matarajio yao katika semina hiyo ni kupata ujasiri wa kujiamini kwa manufaa ya wananchi.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...