Ijumaa, 15 Mei 2015

TAARIFA KUTOKA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI TANZANIA



JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo   : “N G O M E”          Makao Makuu ya Jeshi,

Simu ya Mdomo : DSM  22150463      Sanduku la Posta 9203,

Telex                     : 41051                       DAR ES SALAAM,    15, May 2015

Tele Fax                : 2153426

Barua pepe       : ulinzimagazine@yahoo.co.uk

Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz

                  

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linasikitishwa na  taarifa za uvumi zilizotolewa  kuenea kwenye mitandao ya kijamii face book, whatsapp na twitter zikieleza kuwa JWTZ inafanya usaili leo tarehe           15 May 2015 katika Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) kwa wale waliosoma fani ya Computer science, IT, Electronics na Mechanical Enginering.

JWTZ linapenda kuwajulisha wananchi pamoja na watumiaji wa mitandao hiyo kuwa taarifa hizo si za kweli ni uvumi, JWTZ lina utaratibu wake wa kuandikisha Jeshini ambapo hutoa taarifa katika vyombo vya habari kwa utaratibu ulio sahihi.

   Aidha, Jeshi linaendelea kusisitiza wananchi kuwa halina akaunti za mitandao hiyo na ni kinyume cha sheria kusambaza ujumbe kwa kutumia jina au nembo ya JWTZ watakao bainika watachukuliwa hatua za kisheria dhidi yao.

Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano

Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.

Kwa Mawasiliano zaidi: 0783-309963.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 14.05.2015.



KATIKA TUKIO LA KWANZA:

KIJANA MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA TOTOE WILAYANI CHUNYA MKOANI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DAUD CHARLES (20) ALIUAWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI NA KISHA KUCHOMWA MOTO.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 13.05.2015 MAJIRA YA SAA 05:40 ALFAJIRI HUKO KATIKA OFISI YA SERIKALI YA KIJIJI CHA TOTOE, KATA YA TOTOE, TARAFA YA SONGWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.

INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI TUHUMA ZA WIZI. UCHUNGUZI ZAIDI WA TUKIO HILI UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA KUWABAINI WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

TAARIFA ZA MISAKO:

JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. DANACHO WOLD (24) 2. NATABILA MARCOS (23) 3. KABOWO BURE (21) NA 4. ATSON MASEBO (24) WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.

WAHAMIAJI HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 13.05.2015 MAJIRA YA SAA 22:00 USIKU HUKO KATIKA ENEO LA KYELA KATI, KATA YA KYELA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO ANATOA WITO KWA WAGENI KUTII SHERIA BILA SHURUTI KWA KUFUATA TARATIBU ZA KUINGIA NCHINI ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.

Imesainiwa na:
[NYIGESA R. WANKYO – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

MAMIA WAMUAGA ALIYEKUWA MWANDISHI WA HABARI WA STAR TV FREDY BAKALEMWA, MWILI WASAFIRISHWA KWENDA BUKOBA

 Maremu Fredy Bakalemwa enzi za Uhai wake 
Mke wa Marehemu

Alhamisi, 7 Mei 2015


Bwawa la Bubinza hatarini Kutoweka kutokana na Miundombinu yake Kuhujumiwa


BWAWA la maji la Bubinza lililopo katika Kata ya Lubugu, Wilaya ya Magu, Mwanza, ambalo lilijengwa na Serikali kwa ajili ya kutoa huduma ya maji kwa wananchi wa eneo hilo, linakabiliwa na hatari ya kutoweka kutokana hujuma zinazofanywa na baadhi ya watu wasioaminika kwa kung’oa mabomba yanayosambaza maji kutoka katika bwawa hilo, FikraPevu imebaini.

Kwa sasa bwawa hilo limeanza kuota majani na magugumaji, huku likionekana kugeuzwa kuwa sehemu ya kunyweshea maji mifugo yao, baada ya miundombinu yake ya mabomba kuharibiwa na watu wasiojulikana.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo, wameiambia FikraPevu kwamba hujuma hizo za wizi na uharibifu wa miundombinu ya bwawa hilo, si tu unahatarisha uhai wa bwawa hilo, bali unaweza kusababisha zaidi ya watu 10,000 wa vijiji vinavyolizunguka kukosa maji kwa ajili ya matumizi yao ya nyumbani. Bwawa hilo ndilo pekee linategemewa kwa maji na wananchi wa vijiji vya Bubinza, Ihale na Sola.

Baadhi ya wananchi hao wamelalamikia kitendo cha baadhi ya watu kuanza kuharibu kwa makusudi mabomba ya bwawa hilo, huku wakitoa ombi maalum kwa vyombo vya dola kufanyia uchunguzi suala hilo na hatimaye kuwakamata wahusika.

“Kuna koki mbili za mabomba ya bwawa hili la Bubinza zimeharibiwa, na inabidi kuingiza miti ili kuzuia maji yasiendelee kutoka. Wizi huu unafanyika huku viongozi wa Serikali ya Kijiji wakiwa wapo hapa hapa. Kwanini wahusika hawakamatwi?” amehoji Kiongozi wa Kamati ya Kusimamia Miradi Eendelevu (CMC) Kijiji cha Bubinza, Mathayo Lugwisha.

Kwa upande wao, Mariam Joseph na Kabihe Merick, wakazi wa kijiji cha Kisamba kinachozunguka bwawa hilo la Bubinza, wamesema iwapo mradi huo utakufa kutokana na maji yake kukauka, wananchi hasa wanawake wa maeneo hayo watalazimika kutembea umbali wa kilometa zaidi ya 10 kwa ajili ya kupata maji kutoka Ziwa Victoria.

“Kule Kisamba, pindi visima vinapokauka maji, ndoo moja ya maji inauzwa kati ya Sh 500 na 1,000. Sasa ukiangalia hili bwawa la Bubinza limejaa magugumaji. Watu wananyweshea mifugo yao na maji yanachafuka mno. Wanawake watateseka sana kama bwawa hili litafutika,” amesema Mariam.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Bubinza, Juma Kasomi, amekiri kuwepo kwa hujuma hiyo, akisema wanafanya uchunguzi ili kuwabaini wahusika wa hujuma hizo, na kwamba yeyote atakayebainika kufanya uharibifu huo atachukuliwa hatua za kisheria.

Mratibu wa Shirika la Uangalizi wa Miradi Eendelevu (TCSD) nchini, Damas Nderumaki amesema uharibifu huo na uchafuzi wa mazingira unatokana na uelewa mdogo wa jamii kuhusu faida ya utunzaji mazingira.

“Wananchi wa Kijiji na Kata ya Lubugu, lazima watambue kwamba wanao wajibu wa kulinda rasilimali zote zinazowazunguka, ikiwemo miradi ya maendeleo. Inawapasa washirikiane kuondoa magugumaji ambayo yameanza kujaa kwenye bwawa la Bubinza,” amesema.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...