Jumanne, 29 Aprili 2014

BULEMBO: BIMA YA MOTO SHULE ZA WAZAZI TANZANIA NI LAZIMA



  Mwenyekit wa Jumuiya ya wazazi(CCM) Taifa, Abdallah Majura Bulembo, akimkabidhi Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Sekondari Ivumwe Jijini Mbeya, Dr. Victoria Kanama, kiasi cha Shilingi Milioni tatu (Tsh. 3,000,000/=) kwa ajili ya ukarabati wa mabweni ya wavulana wa shule hiyo, yaliyoteketea April 23, mwaka huu.
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi(CCM) Taifa, Abdallah Majura Bulembo, akiwapa pole wanafunzi wa Sekondari ya Ivumwe, Jijini Mbeya jana, baada ya shule hiyo kupata janga la moto ulioteketeza mabweni saba ya wavulana wa shule hiyo, April 23, Mwaka huu na kusababisha hasara ya Milioni 30.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ivumwe Jijini Mbeya jana.
 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi(CCM) Taifa, Abdallah Majura Bulembo(kulia), akiwa anakagua moja ya bweni la wavulana wa shule ya Sekondari Ivumwe Jijini Mbeya jana, baada ya shule hiyo kupata janga la moto.

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania(CCM), Abdallah Majura Bulembo, ameamuru shule zote zinazomilikiwa na jumuiya hiyo kote nchini kukata bima ya moto.

Agizo hilo alilitoa jana mjini Mbeya, alipokuwa akikagua uhalibifu uliojitokeza baada ya janga la moto kuteketeza mabweni saba ya wavulana katika shule ya Sekondari Ivumwe, iliyopo Jijini hapa.

Alisema katika bima ambazo ni rahisi na bei nafuu nchini ni bima ya moto, lakini ndiyo bima pekee ambayo haikatwi na wananchi na taasisi nyingi.

“Kuanzia sasa, suala la bima ya moto ni la lazima kwa shule zote za jumuiya ya wazazi wa CCM Tanzania. Baraza kuu tutakutana kwa dharula mjini Dodoma Mei 17, mwaka huu na tutakachokipata tutakileta haraka kwenu ili kusaidia katika janga hili la moto’’ alisema Bulembo.

Mbali na agizo hilo, aliwapa pole wanafunzi waliounguliwa na vitu vyao vyote na kuwataka wawe wavumulivu, pia alitoa mchango wa Milioni tatu (3,000,000/=)kwa ajili ya ukarabati wa mabweni hayo na mahitaji mengine ya haraka na kuahidi kuwashirikisha wadau wengine wa elimu ili kuwasaidia wanafunzi waliokuwa wakiishi kwenye mabweni hayo.

Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo, Dr. Victoria Kanama, alimshukuru Mwenyekiti huyo wa wazazi Taifa na kwamba kutokana na mchango wake, mabweni hayo yatakamilika ndani ya mwezi mmoja.

“Umetupa nguvu sana na tutahakiisha tunakarabati mabweni haya ndani ya mwezi mmoja na kufanya jitihada za kuongeza ufanisi wa ufaulu katika shule yetu kuanzia kidato cha kwanza mpaka kidato cha sita” alisema Dr. Kanama.

Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo ya Ivumwe, Emerry Muhondwa alisema janga la moto lilitokea April 23, mwaka huu majira ya saa 3 hadi saa 4 asubuhi wakati wanafunzi wapo madarasani.

“Mabweni saba ya wavulana ndiyo yaliteketea na moto uliteketeza Vitanda 93, Magodoro 186, mashuka 372, Mablanketi 186, mabegi 186, matranker 186 pamoja na vitabu na madaftari, vyote vikiwa na jumla ya Milioni 30’’ alisema Mwalimu Mohondwa.

Katika taarifa yake kwa Bulembo, mkuu huyo wa shule alisema kwa sasa wanafunzi hao wanalala katika madarasa na wameazima magodoro katika shule ya wasichana ya Loleza ya Jijini hapa.

Ivumwe, ni kati ya shule zenye sifa ya kufaulisha, ambapo katika mtihani wa utamilifu(Mock), kidato cha sita mwaka huu, shule hiyo imeshika nafasi ya pili kati ya shule 26 zilizokuwa na watahiniwa 30 katika kanda ya Nyanda za juu kusini mikoa ya Mbeya, Rukwa na Katavi.

Jumapili, 27 Aprili 2014

MUUNGANO WETU 26.04.2014 JIJINI DAR ES SALAAM


SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR ZAFANA UJERUMANI: PROFESA MUHONGO, MGENI RASMI

 Kikundi cha ngoma za sanaa kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania  kikitumbuiza  kabla ya kuanza kwa sherehe hizo.
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb) akizungumza na  baadhi ya wajumbe waliohudhuria  sherehe hizo

 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb) akibadilishana mawazo  na balozi wa heshima wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Hamburg Petra Hammelmann. Kulia ni mume wa balozi huyo Bw.Bertold Zink.
 Waziri wa Nishati na  Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb) (wa  pili kutoka kulia) akiwa amesimama kwa heshima na wajumbe wengine wakati wimbo wa taifa ukipigwa na kikundi cha ngoma za sanaa cha Jeshi la Wananchi Tanzania
 
 Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo akimkaribisha Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ili afungue maadhimisho hayo
 Waziri wa Nishati na  Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb) akifungua sherehe hizo
 Mhadhiri kutoka chuo  kikuu cha Dar es salaam Profesa Palamagamba Kabudi (wa tatu kutoka kulia) akichangia mjadala juu ya historia ya ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani wakati wa maadhimisho ya sherehe hizo
Timu ya wataalamu kutoka Tanzania waliohudhuria sherehe hizo wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania Nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo (wa kwanza kulia)

credit;matukio-michuzi

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 27.04.2014.





·  MTOTO WA MIAKA MITATU AUAWA KWA KUPIGWA NGUMI NA BABA YAKE MZAZI.   

MTOTO WA MIAKA MINNE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI.


KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTOTO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA VANESA PATRICK NJOJO (03) MKAZI WA ISISI, WILAYANI MBARALI ALIUAWA KWA KUPIGWA NGUMI NA BABA YAKE MZAZI AITWAYE PATRICK  NJOJO (23) MKAZI WA ISISI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 26.04.2014 MAJIRA YA SAA 23:45 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISISI, KATA NA TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILI ULEVI WA POMBE ZA KIENYEJI WA BABA HUYO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA MBARALI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUEPUKA ULEVI KWANI NI HATARI KWA AFYA ZAO NA UNA MADHARA KATIKA JAMII. AIDHA ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWAFUNDISHA WATOTO WAO KWA UTARATIBU MZURI ILI KUEPUKA MATATIZO.


KATIKA TUKIO LA PILI:

MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 4 – 5 ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FESTO  MBIGA, MKAZI WA NSALAGA AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI SM 9124 AINA YA FAW LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA RAMADHANI MWALYOYO (30) MKAZI WA ILOMBA JIJINI MBEYA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 26.04.2014 MAJIRA YA SAA 14:45 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA NSALAGA, KATA YA UYOLE, TARAFA YA IYUNGA, BARABARA KUU YA MBEYA/IRINGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA NA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.


                                                      Signed by:
                                      [AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

KIPAUMBELE MAGAZETI YA KIKRISTO JUMAPILI YA APRIL 27,2014

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

KANISA KATOLIKI KUTANGAZA WATAKATIFU LEO

vatican Kanisa katoliki leo Tarehe 27/04/2014, linategemea kuwatangaza watakatifu ambao huandikwa katika kitabu cha maisha ya watakatifu,Papa John Paul II na John XXIII wanatarajiwa kutangazwa watakatifu katika tukio litakaloongozwa na kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis huko St Peter’s Square  jijini Vatican.

Alhamisi, 24 Aprili 2014

MARY MWANJELWA; UVUNJIFU WA UTAWALA BORA UPO ZAIDI VIJIJINI

MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Mbeya(CCM) Mary Mwanjelwa, amesema kuwa, uvunjifu wa masuala ya utawala bora umezidi kushamili zaidi Vijijini.
 
Ameishauri serikali kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha viongozi wa vijiji kuacha kujifanya miungu watu.
 
Hayo aliyasema juzi katika mkutano wa kamati ya ushauri ya mkoa wa Mbeya(RCC), uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa Jijini Mbeya.
 
Kwa upande wake Waziri wa nchi Ofisi ya Rais(Utawala Bora) George Mkuchika amewataka watumishi wa umma kuzingatia maadili katika utendaji wao ili kuepuka watendaji kupigiwa mifano ya utoaji na upokeaji Rushwa.


Alisema serikali ya awamu ya nne inaamini ujenzi na uimarishaji wa Utawala Bora ndiyo njia pekee yenye ubora sahihi na yenye uhakika katika jitihada za kuondokana na matatizo ya rushwa, umaskini na uendeshaji mbovu wa huduma za umma.

Alisema serikali kwa kuzingatia muongozo wa Taaifa wa mwaka 1999 kuhusu Utawala Bora(Good Governance) imeanzisha programu mbalimbali kwa lengo la kujenga na kuimarisha Utawala Bora nchini.

Mkuchika alisema kuwa baadhi ya programu hizo ni marekebisho ya kuboresha utendaji katika utumishi wa umma(The Public Service Reform Programe) na  marekebisho ya kuboresha usimamizi wa fedha za umma (The Public Financial Management Programme) na mareekebisho ya kuboresha mfumo wa uendeshaji wa serikali za mitaa( The Local Government Reform Programme).

Jumatano, 23 Aprili 2014

ASKARI WA JESHI LA POLISI NA WENZIE WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 JELA.

Washitakiwa wanne kati ya watano kutoka kushoto juu hadi wa nne wakiwa wanatoka mahakamani chini ya ulinzi mkali.  

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 21.04.2014.



KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AMANI GREYSON (22) MKAZI WA IPOROTO ALIUAWA NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MIKONONI BAADA YA KUMTUHUMU KUIBA NG’OMBE MMOJA MALI YA BABU YAKE AITWAYE GEOFREY SALAMU @ NGOLIA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 20.04.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MAONA, KIJIJI CHA TWINZI, KATA YA BARA, TARAFA YA ITAKA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA.

 INADAIWA MAREHEMU ALIKAMATWA NA ASKARI MGAMBO NA KUWEKWA NDANI. INAELEZWA KUWA MAREHEMU ALIVUNJA MLANGO NA KISHA KUANZA KUKIMBI NA NDIPO WANANCHI WALIMUONA NA KUMSHAMBULIA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA - VWAWA. JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.



KATIKA TUKIO LA PILI:

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA WILLY JUMA (21) MKAZI WA MJERE AMEUAWA KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI NA MTUHUMIWA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NURU MSAFIRI (21) MKAZI WA MJERE.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 20.04.2014MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA MJERE, KATA YA MSHEWE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI ULEVI. TAARIFA ZA AWALI ZINADAI KUWA MAREHEMU NA MTUHUMIWA NI MARAFIKI NA KABLA YA TUKIO WALIKUWA PAMOJA KATIKA KLABU CHA POMBE.

MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA UCHUNGUZI ZAIDI.










KATIKA MISAKO:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. JOYCE MWAKALINGA (30) MFANYABIASHARA NA MKAZI WA ILOMBA NA 2. ASHA  JOHN (28) MKAZI WA LUBELE WAKIWA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 17.

WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA KATIKA MISAKO ILIYOFANYWA KATIKA MAENEO TOFAUTI MNAMO TAREHE 19.04.2014 NA 20.04.2014 MAJIRA YA SAA 12:45 MCHANA KATIKA WILAYA YA KYELA NA JIJINI MBEYA. WATUHUMIWA NI WAUZAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA UUZAJI WA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.



KATIKA MSAKO MWINGINE:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU WAPATAO 82 WOTE JINSI YA KIUME MIAKA KATI YA 18-30, RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.

WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.04.2014 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA BUSALE, KATA YA BUSALE, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA.

TAARIFA ZA AWALI AMBAZO BADO ZINAFANYIWA UCHUNGUZI INASADIKIWA WATUHUMIWA HAO WAMETOKEA NCHINI MALAWI BAADA YA KUFUKUZWA NA KISHA KUKIMBILIA NCHINI TANZANIA. KATIKA HARAKATI ZA KUKIMBILIA NCHINI TANZANIA RAIA WEMA WALIWAONA NA KISHA KUTOA TAARIFA ZILIZOSAIDIA KUKAMATWA. TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI KWA TARATIBU ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO ILI WAKAMATWE NA KUFANYIWA UCHUNGUZI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.


Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...