Ijumaa, 29 Agosti 2014

AJALI MBAYA YAUA WATU ZAIDI YA NANE MBALIZI MBEYA ASUBUHI YA LEO


 Eneo la ajali Mbaliz, mashuhuda na wananchi wengine wakiwa eneo la tukio asubuhi hii.
 Gari ya polisi ikiondoka na miili ya marehemu kuelekea hospitali ya Mbalizi Ifisi, baada ya ajali na kuzoa baadhi ya viungo vya marehemu.
 Hii ndiyo hiace iliyokuwa na abiria baada ya ajali eneo la Mbalizi Mbeya asubuhi ya leo. Ajali ni mbaya sana.

Call for Organisational Development expert for new TMF

August 29, 2014  
 
Hivos Tanzania, which manages the Tanzania Media Fund (TMF) until May 2015, is looking for an organisational development expert. The right candidate will assess and address the capacity strengthening needs for TMF and help design a programme of organisational strengthening, towards the establishment of an independent TMF. The assignment will take place in September 2014, for a maximum of 15 actual working days.

Applications must be submitted before the close of business on 4th September, 2014. For more information, download the Call for Expressions.

Jumatano, 27 Agosti 2014

TAARIFA YA ULINZI NA USALAMA KANDA NO 2 MKOA WA MBEYA TAREHE 26.08.2014.



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.


 


       R.P.C                                                                                               Ofisi ya Kamanda wa Polisi,                                                                                                                                                                                                                                                                                      Mkoa wa Mbeya,
Namba ya simu 2502572                                                                                          S. L. P. 260,
Fax -+255252503734                                                                                                    MBEYA.
E-mail:rpc.mbeya@tpf.com.tz
Unapojibu tafadhali taja 

MBR/C.5/900/VOL.I/251.                                                                  Tarehe: 26 Agosti, 2014.

Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P 9141,
DAR ES SALAAM.

                       YAH: TAARIFA YA ULINZI NA USALAMA KANDA NO 2 MKOA
                                                         WA MBEYA TAREHE 26.08.2014.

Tafadhali husika na kichwa cha habari tajwa hapo juu.
Pamoja na barua hii ninakutumia taarifa ya hali ya ulinzi na usalama Kanda no 2 Mkoa wa Mbeya ya  masaa 24 yaliyopita kufikia tarehe 26.08.2014.
Naomba kuwasilisha tafadhali.


                                                  [Barakael Masaki – ACP].
          Kny         KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA


Nakala kwa:  Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai,
                        Makao Makuu ya Upelelezi,
                        S.L.P 9093,
                        DAR ES SALAAM. - Kwa taarifa tafadhali.

                        Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai,
                        Mkoa wa Mbeya,
                        S.L.P 260,
                        MBEYA – Kwa taarifa




[i] MATUKIO YA UHALIFU/AJALI ZA USALAMA BARABARANI.
S/NO
Tarehe
Muda
Maelezo ya Kosa / Tukio.
Watuhumiwa
01.
26.08.2014
03:30hrs
MB/IR/6898/2014 – AJALI YA MOTO.
Huko Iyunga, Kata na Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya. Mtu mmoja aitwaye DAVID S/O IMWMAMU, miaka 39, Mkurya, DSO – Mbeya, Mkazi wa Iyunga aligundua kuungua kwa Nyumba aliyopanga inayomilikiwa na RICHARD S/O YAONDE, miaka 45, Mnyiha, Mfanyabiashara na Mkazi wa Sumbawanga yenye Vyumba Vitano [05]. Moto huo uliteketeza vitu vyote vilivyokuwa sebuleni, stoo pamoja na Master Bed Room na paa lote la Nyumba hiyo isipokuwa sehemu ndogo sana ya paa hilo. Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika. Moto huo ulizimwa kwa Jitihada za Kikosi cha Zima moto na Uokoaji, Askari Polisi pamoja na Wananchi. Thamani halisi ya mali iliyoteketea bado kufahamika. Hakuna madhara yoyote ya kibinadamu yaliyoripotiwa. Kiongozi wa Zone namba 01 Kanda A amekagua tukio, Upelelezi unaendelea.
---

[ii] MATUKIO YATOKANAYO NA MAFANIKIO YA DORIA/MISAKO.
S/NO
Tarehe
Muda
Maelezo ya Kosa / Tukio.
Watuhumiwa
01.
25.08.2014
16:30hrs
MB/IR/6880/2014 – KUPATIKANA NA BHANGI.
Huko Ilolo, Kata ya Sinde, Tarafa ya Sisimba, Jiji na Mkoa wa Mbeya, Zone namba 05, Kanda A. Askari Polisi wakiwa Doria/Msako waliwakamata 1. HANS S/O PIUS, miaka 27, Kyusa, Mkazi wa Ilolo 2. ZAWADI S/O ANDREW, miaka 22, Msafwa na Mkazi wa Sinde B 3. KINGSLEY S/O MWAMAJA, miaka 24, Kyusa, Mkulima na Mkazi wa Isanga na 4. SIKUJUA S/O ELIA, miaka 25, Kyusa, Mkulima na Mkazi wa Sangu wakiwa na Bhangi Uzito wa Gramu 03 ndani ya Mfuko wa kaki.
04
02.
25.08.2014
12:14hrs
MBO/IR/1261/2014 – KUPATIKANA NA RISASI ZA SMG NA SHORT GUN.
Huko katika Kitongoji cha Ilembo “B” Mtaa wa Ilembo, Kata na Tarafa ya Vwawa, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Mbeya, Zone namba 06 Kanda B. Askari Polisi wakiwa Doria/Msako walimkamata GABRIEL S/O MWAMPASHI, miaka 25, Mnyiha, Mkazi wa Ilembo “B” akiwa na risasi 07 za Bunduki aina ya SMG na risasi 01 ya Bunduki aina ya Short Gun nyumbani kwake wakati akiwa anapekuliwa kutokana na kuhusika na makosa ya Uvunjaji.

01
03.
25.08.2014
15:30hrs
MKI/IR/961/2014 – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
Huko katika Kitongoji cha Mamba, Kata ya Mamba, Tarafa ya Kipembawe, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, Zone namba 23. Askari Polisi wakiwa Doria/Msako waliimkamata DAUDI S/O GABRIEL@ BUKUKU, miaka 32, Kyusa, Mkulima na Mkazi wa Mamba “A” akiwa na Pombe Haramu ya Moshi [Gongo] ujazo wa lita 07 Nyumbani kwake. Mtuhumiwa ni Muuzaji wa Pombe hiyo.
01

[iii] MATUKIO YATOKANAYO NA UNYANYASAJI WA KIJINSIA.
S/NO
Tarehe
Muda
Maelezo ya Kosa / Tukio.
Watuhumiwa
   --
--
      --
--
--

A: Migogoro /Maafa- Hakuna.
Ø  Kisiasa – Umefanyika Mkutano wa Chama cha Siasa cha Chadema Huko katika Kata ya Itiji, Tarafa ya Sisimba, Mkoa wa Mbeya. Katika Mkutano huo Mgeni Rasmi alikuwa ni Mbunge wa Mbeya Mjini Mh.Joseph Mbilinyi ambaye alikuwa amefuatana na Viongozi Waandamizi wa Chadema ngazi ya Mkoa na Wilaya. Agenda zilikuwa ni kufanya tathmini juu ya ahadi zake kwa Wananchi zilizotolewa na Mbunge huyo. Katika Mkutano huo Hapakuwa na Lugha za Matusi na Mkutano ulimalizika majira ya saa 18:20 jioni na wananchi kutawanyika kwa amani na utulivu.
Ø  Wakulima na Wafugaji – hakuna.
Ø  Wakulima/Wananchi na Wawekezaji – Hakuna
Ø  Dini – Hakuna.
B: Idadi ya watendaji.
Ø  Jumla ya askari 1,458 waliingia kazini, doria na malindo mbalimbali.
Ø  Jumla ya watumishi raia waliopo ni 17.
Ø  Jumla ya  vikundi vya ulinzi jirani vilivyopo  Mkoa wa  Mbeya  262,  jumla ya  vikundi vilivyoshiriki  ni  101  na walinzi   394  walishiriki katika doria/malindo mbalimbali.
Ø  Jumla ya askari Mgambo waliopo Mkoa wa Mbeya ni 2,253.
Ø  Jumla ya Polisi wasaidizi waliopo ni 420.





C: Mafanikio yaliyopatikana.
§  Mafanikio yaliyopatikana kupitia doria,misako na operesheni ni kama ifuatavyo:-
v  Bhangi –
v  Dawa za kulevya {drugs} – Hakuna.
v  Pombe ya Moshi – Hakuna.
v  Silaha – Hakuna
v  Nyara za Serikali – Hakuna.

D: Ukamataji wa makosa ya Usalama Barabarani.

§  Jumla ya  makosa yaliyokamatwa –  262
§  Jumla ya  makosa yaliyolipa - 237
§  Jumla ya magari yaliyokaguliwa kwa siku – Hakuna.
§  Tozo lililopatikana kutokana na ukaguzi wa magari – Hakuna.
§  Kesi zilizopelekwa Mahakamani – Hakuna.
§  Jumla ya Tozo [Notification] Tshs 7,110,000/=.

E: Watuhumiwa waliokamatwa kwa makosa mbalimbali.
  • Jumla ya watuhumiwa waliokamatwa ni 43.
  • Jumla ya wahalifu wazoefu{harbitual} Mkoa wa Mbeya   139.
  • Wahalifu wazoefu {Harbitual} – waliokamatwa – 05.
  • Jumla ya wahalifu waangaliwa {Supervisee} Mkoa wa Mbeya 86.
  • Wahalifu waangaliwa {Supervisee} – waliokamatwa – 03.
  • Jumla ya kesi zilizofikishwa Mahakamani – 65.
  • Kusomewa Mashitaka {fresh Cases} – 07.
  • Jumla ya kesi zilizosikilizwa {Hg}– 50.
  • Jumla ya kesi zilizotajwa {M}– 65.
  • Kusomewa maelezo ya awali {Phg} – 26.
  • Watuhumiwa waliofungwa {Convicted} – 04.
  • Watuhumiwa waliachiliwa huru {Acquited} - Nil.

F: HITIMISHO:
Kwa leo tarehe 26.08.2014 kumekuwa na idadi ya matukio “Hakuna” kama ifuatavyo:-
  • Mauaji – Hakuna.
  • Unyang’anyi wa Kutumia Silaha – Hakuna.
  • Ajali ya Gari Kusababisha Vifo – Hakuna.       

Jumamosi, 23 Agosti 2014


Shule waliyosoma Rais Joseph Kabila (wa DRC), Assah Mwambene yachakaa vibaya!

Posted By - (2656) Views
SHULE ya Sekondari ya Irambo inayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), iliyopo katika Wilaya ya Mbeya Vijijini inakabiliwa na tatizo la uchakavu wa miundombinu ya majengo hali inayotajwa kufanyiwa ukarabati ili kuendana na hadhi ya shule hiyo. 


Shule hiyo inatwajwa kuongoza kutoa matokeo bora ya kitaaluma tangu kuanzishwa kwake, ambapo pia shule inatwajwa kuwa ndiyo waliyosoma viongozi maarufu Nchini Tanzania akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assa Mwambene na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Irambo
Uchunguzi uliofanywa na FikraPevu leo Agosti 19, 2014 mkoani humo umebaini kuwa licha ya viongozi hao kusoma shuleni hapo, ufaulu wa shule hiyo umeshuka kwa kiwango kikubwa tofauti na ilivyokuwa hapo awali. 



Makamu Mkuu wa shule hiyo, Aliko Mwanjala, amebainisha kuwa shule hiyo haina miundombinu ya kutosha licha ya kuwa na uhaba wa vifaa vya kufundishia huku akisema hali ya majengo ya shule hiyo kuwa sio rafiki. 




Amesema awali shule hiyo ilikuwa ni shule ya mfano kitaaluma na kimalezi katika mkoa wa Mbeya na kuwa juhudi za kuinusuru na kuiinua kupitia kwa wadau mbalimbali wakiwemo wanafunzi waliowahi kusoma katika shule hiyo bado zinaendelea. 



Mmoja wa watu waliowahi kusoma katika shule hiyo akiwemo Sambwee Shitambala, ambaye sasa ni Mwanasheria alikaririwa na FikraPevu akisema “Nitajitahidi kuwashirikisha wenzangu kuhusu hali hii naona majengo yamechakaa sana tofauti na tulivyokuwa tunasoma hapa kikiwemo jingo lenye chumba alichokuwa analala, Rais Kabila”.

Madarasa

Sehemu ya madarasa ya Shule ya Irambo
 
 
Hata hivyo, amebainisha kuwa hapo awali shule hiyo ilikuwa inatumimiw ana watu wengi waliokuwa wakiwekwa kwa ajilio ya kufanya kazi kwenye idara nyeti za serikali na hivyo kuwataka watu wote waliosoma katika shule hiyo kwende shuleni hapo na kutoa misaada ya kuikarabati shule hiyo.
Darasa la Kabila
Chumba ambacho kilikuwa bweni ambalo, Rais Joseph Kabila, wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), alikuwa akikitumia kwa ajili ya kulala kwa sasa hili ni darasa la kidato cha pili, aliyesimama ni mwandishi wa habari Gordon Kalulunga
 
 
Taarifa za ndani kutoka kwa wanafunzi waliosoma katika shule hiyo waliopo katika maeneo mbalimbali nchini, wameidokeza FikraPevu kuwa mwanzoni mwa mwezi Septemba, 2014 wanakusudia kutoa misaada mbalimbali kwa ajili ya shule hiyo kupitia kikundi ambacho hawajapenda kukiweka wazi kilicho mbioni kusajiliwa kwa ajili ya shule hiyo.

CHANZO; FIKRA PEVU YA JF

Jumanne, 19 Agosti 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA JAJI LEWIS MAKAME


Marehemu Jaji Mstaafu,Lewis Makame enzi za uhai wak


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za  Rambirambi Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, National Electoral Commission (NEC) kufuatia taarifa za kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame kilichotokea katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Agosti, 2014.


“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania na Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) chini ya Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa, Mheshimiwa Lewis Makame ambaye amelitumikia Taifa letu katika Utumishi wa Umma kwa uaminifu, uadilifu, bidii na umahiri mkubwa”, amesema kwa masikitiko Rais Kikwete katika Salamu zake.


Katika utumishi wake, Marehemu Jaji Lewis Makame, enzi za uhai wake, alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kabla ya kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa na baadaye Mwenyekiti wa NEC ambayo aliiongoza kwa miaka 17 mfululizo hadi alipostaafu mwaka 2011.  Uongozi wake ulichangia sana kuimarisha amani, utulivu, umoja na mshikamano wa kitaifa katika mazingira mapya ya demokrasia ya vyama vingi vya siasa hapa nchini.


“Ni kwa kutambua kipaji kikubwa cha uongozi alichokuwa nacho Marehemu Jaji Lewis Makame, Taifa letu limepoteza mtu muhimu sana kwani hata baada ya kustaafu kwake alikuwa bado anahitajika sana kutokana na mchango wake wa ushauri katika mambo mengi yanayohusu maendeleo ya nchi yetu”, amesema Rais Kikwete na kuongeza,


“Kutokana na msiba huu mkubwa, nakutumia Salamu za Rambirambi kwa kumpoteza aliyekuwa Kiongozi Mahiri wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kupitia kwako, naomba Salamu zangu za Rambirambi na pole nyingi ziifikie Familia ya Marehemu kwa kumpoteza Kiongozi na Mhimili Madhubuti.  Namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza Mahala Pema Peponi Roho ya Marehemu, Jaji Lewis Makame, Amina”, amesema Rais Kikwete akiomboleza msiba huu.  


Amewahakikishia Wanafamilia kuwa yuko pamoja nao katika kuomboleza msiba huu mkubwa, na anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema awape moyo wa uvumilivu, ujasiri na subira Wanafamilia wote, ndugu na jamaa wa Marehemu, ili waweze kuhimili machungu ya kuondokewa na Mpendwa wao kwa kutambua kuwa yote ni Mapenzi yake Mola.  



Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.

19 Agosti, 2014

Alhamisi, 14 Agosti 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 13.08.2014.




KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MWANAMKE MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA ANGELINA KAMZELA (29) MKAZI WA IDIWILI ALIKUTWA AMEUAWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA SHINGONI, USONI NA KISOGONI NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA PORINI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 12.08.2014 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA IDIWILI, KATA NA TARAFA YA IYULA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, MAREHEMU ALITOWEKA NYUMBANI KWAKE TANGU TAREHE 06.08.2014 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI NA HAKUONEKANA HADI HAPO JANA MWILI WAKE ULIPOKUTWA PORINI.

CHANZO CHA TUKIO HAKIJULIKANI, HAKUNA MTU/WATU WALIOKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILI. MSAKO MKALI UNAENDELEA KUWATAFUTA WALE WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERAIA ZICHUKULIWE DHDI YAO.


KATIKA TUKIO LA PILI:

MTEMBEA KWA MIGUU AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA LAKE WALA MAKAZI YAKE, UMRI KATI YA MIAKA 30-32 AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.542 BBH AINA YA TOYOTA COASTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE PEREGLIN ALEX (38) MKAZI WA KYELA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 12.08.2014 MAJIRA YA SAA 09:40 ASUBUHI HUKO MAENEO YA KILIMO – UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI BADO KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA AMEKAMATWA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA/KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.


Imesainiwa na kutolewa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...