Mashabiki a Mbeya City, wakiipokea kwa shangwe timu yao.
MASHABIKI wa
timu ya Tanzania Prison, wamesema kuwa Mgambo kazi yao ni kufundisha
mchakamchaka na wala siyo kucheza mpira, hivyo timu ya Mgambo, wajiandae
kufungwa katika uga wa Sokoine.
Kocha wa
timu ya kukuza vipaji ya Mbeya umoja Sports Academy, ambaye ni shabiki wa timu ya Tanzania Prison, Peus Nsheka,
aliyasema hayo jana ukumbi wa magereza, wakati wa hafla ya mapokezi ya timu
hiyo mbele ya mkuu wa magereza mkoa wa Mbeya(RPO), Emmanuel Sanguti.
Wadau hao
walikabidhi matunda na juice kwa wachezaji ambapo nahodha wa timu hiyo Lugano
Mwangama, alipokea zawadi hizo kwa niaba ya wachezaji wenzake.
Shabiki
mwingine, Christopher Nyenyembe, ambaye ni mwandishi wa habari, aliuambia uongozi
wa timu hiyo kuwa, hawapaswi kubadilisha walimu kwasababu imeonesha kuwa walimu
wazalendo wanao uwezo mkubwa wa kufundisha timu za Tanzania.
“Makocha
kutoka nje ya nchi wanakula fedha za timu pasipo sababu yeyote. Fedha hizo
zinapaswa kuimarisha timu badala ya kuwapa makocha hao kwasababu makocha
wazalendo akiwemo Mwamwaja wanao uwezo mzuri’’ alisema Nyenyembe.
Mkuu wa
Magereza mkoa wa Mbeya, aliwapongeza wachezaji, mashabiki, askari na vyombo vya
habari kuifikisha timu hiyo hapo ilipo na kwamba mchezo uliooneshwa na timu
hiyo kwenye uwanja wa Chamanzi wa Azam Jijini Dar es Salaam, inaonesha timu
hiyo inao uwezo wa kufikia nafasi ya tatu bora.
“ Kila mechi
iwe fainali, kama ilivyokuwa pale chamanzi, Azam waliomba mechi iishe haraka na
hizi timu kubwa zina mambo yao, tulinyimwa penati zaidi ya tatu lakini
tuliishusha kutoka kileleni’’ alisema Sanguti.
Mkuu wa
gereza la Ruanda, SSP Ismail Misama, aliwaambia wachezaji wa timu hiyo kuwa
hawapaswi kubweteka ili kufikia nafasi ya tatu bora na kwamba uwezo na nia kwa
pamoja na umoja wa wadau ipo.
Naye mkuu wa
chuo ambaye ni mlezi wa timu hiyo, Mashaka Soja na mhamasishaji SP Enock
Lupyuto, walisema timu zilizobakiza mechi na timu hiyo zijiandae kisaikolojia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni