Jumatano, 29 Oktoba 2014

MTOTO WA KIKE ATEKWA MBEYA

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Biton Bomani Mwashilindi, mkazi wa Airport Jijini Mbeya anatuhumiwa kumteka mtoto Zalida Rogers (2),  kutoka kwa mama yake mzazi aitwaye Juliana Josia(22) eneo la Mwanjelwa Jijini hapa.


Tukio hilo limetendeka eneo la Kituo cha mafuta Mwanjelwa Oktoba 27 mwaka huu, majira ya mchana baada ya mtekaji kufanikiwa kumfungua mbeleko mama ya mtoto kisha kufanikwa kuvuka barabara kuu kuelekea upande wa pili kutokea Airport kuelekea eneo la Makunguru.


Mama huyo alitoa taarifa katika kituo cha Polisi Mwanjelwa na kuanza kumsaka mtekaji huyo bila mafanikio huku mtekaji akituma ujumbe kupitia simu yake ya kiganjani akimtaka mama wa mtoto huyo ili kuyajenga  na aweze kumkabidhi mtoto wake.


Hata hivyo mtekaji huyo aliendelelea kutuma ujumbe wa vitisho kwa mama mzazi wa mtoto huyo kuwa wafanye mazungumzo eneo la njia panda Magege ili amwachie mwanawe na asipofanya hivyo hatamkabidhi mtoto wake.


Jana mtekaji huyo alimtaka Juliana Josia aende eneo la Magege akiwa peke yake ili wazungumze kisha amkabidhi mtoto na ndipo Juliana akiwa na Askari kanzu walifika eneo hilo majira ya mchana huku akitumia simu ya rafiki yake na Askari walipofika eneo husika mtuhumiwa alimtuma rafiki yake ambaye hakufahamika mara moja na yeye kutokomea na mtoto kusiko julikana.


Polisi wanamshikilia rafiki yake Biton kwa mahojiano ingawa Biton mwenyewe akiendelea kutuma jumbe za vitisho mfululizo na moja ya ujumbe ukidai kwa kuwa Polisi wamemkamata rafiki yake basi ataozea jela lakini yeye hatamkabidhi mtoto.


Taarifa zinadai kuwa mama wa mtoto huyo, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa na mtuhumiwa miaka miwili iliyopita na mtuhumiwa alidai kuwa huyo ni mtoto wake.



Jalada la uchunguzi  limefunguliwa kituo kikuu cha Polisi Mbeya, lenye namba MB/RB/9384/2014 .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...