Jumanne, 28 Oktoba 2014

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI JESHI LA POLISI TANZANIA.






TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 28.10.2014.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA SAMANGOMBE ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA SHIDA WILSON MAZWILE (35) ALIUAWA KWA KUCHOMWA KISU TUMBONI BAADA YA KUVAMIWA NA MTU/WATU WASIOJULIKANA AKIWA AMELALA NYUMBANI NA MKE WAKE MDOGO AITWAYE CHRISTINA SAITON TANDALA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.10.2014 MAJIRA YA SAA 00:01 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA SAMANGOMBE, KATA NA TARAFA YA KAMSAMBA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO HAKIJAFAHAMIKA. JUHUDI ZA KUWATAFUTA WATUHUMIWA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO/WALIPO WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.

KATIKA TUKIO LA PILI:

MTU MMOJA MKAZI WA SENJELE WILAYA YA MBOZI ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA SEMENI SHANGU (22) ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.426 CXT AINA YA YUTONG LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE BRUGE MZAVA (37) MKAZI WA SUMBAWANGA.

AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 27.10.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA SENJELE, KATA YA MYOVIZI, TARAFA YA IYULA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI, DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.

TAARIFA ZA MISAKO:

KATIKA MSAKO WA KWANZA, MTU MMOJA AITWAYE EDAH SING’OMBE (32) MKAZI WA MACHINJIONI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 05 PAMOJA NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA POMBE HIYO.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 27.10.2014 MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.  MTUHUMIWA NI MPIKAJI NA MUUZAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.



KATIKA MSAKO WA PILI, MTU MMOJA AITWAYE JOSHUA MWAKAJA (43) MFANYABIASHARA NA MKAZI WA MAJENGO ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU AINA YA DOUBLE PUNCH PAKETI 66.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 27.10.2014 MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI HUKO KATIKA MTAA WA MAJENGO, KIJIJI NA KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIZO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.


KATIKA MSAKO WA TATU, MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ELIZABETH ERNEST (20) MKAZI WA MAKONGOLOSI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 10.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 27.10.2014 MAJIRA YA SAA 14:30 MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MACHINJIONI, KIJIJI NA KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO.


KATIKA MSAKO WA NNE, MTU MMOJA MKAZI WA MKWAJUNI WILAYANI CHUNYA AITWAYE SHUGHULI SIX (30) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI UZITO WA ROBO KILO.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA NA KUKUTWA NA BHANGI HIYO MNAMO TAREHE 27.10.2014 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KIKUYU, KIJIJI NA KATA YA MKWAJUNI, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKUTWA NA BHANGI HIYO BAADA YA KUPEKULIWA KATIKA BANDA LAKE LA KUUZIA POMBE. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA [BHANGI], POMBE HARAMU YA MOSHI PAMOJA NA POMBE KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU AU MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI NA USAMBAZAJI WA BIDHAA HARAMU ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.

Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...