Jumanne, 24 Juni 2014

SIKU YA KUPIGA VITA DAWA ZA KULEVYA KUFANYIKA MBEYA KESHO KUTWA TAREHE 26/06/2014

MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO.

Kutokana na mkoa wa Mbeya kuwa ni moja ya mikoa hapa nchini yenye milango ya kupitisha dawa hizo na pombe zinazoitwa haramu(viroba), Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, alisema Mkoa wake umepata bahati ya kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya kitaifa.

Aliitaja siku hiyo kuwa ni kesho kutwa June 26, mwaka huu na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais, Dr. Mohmed Gharib Bilal na shughuli zote zimeanza katika viwanja vya Ruanda Nzovwe Jijini Mbeya tangu leo Juni 24, mwaka huu.

Alitaja lengo la maadhimisho hayo kuwa ni kuiasa na kuikumbusha jamii juu ya athari za utumiaji wa madawa ya kulevya na pia kuihamasisha jamii kuachana na matumizi ya dawa hizo.

“Maonyesho yatakuwa na lengo la kutoa elimu ya jinsi ya kuzuia uingiaji wa dawa hizo, kupima waathirika na kutoa tiba kwa waathirika na taasisi zaidi ya 10 zitashiriki zikiwemo TFDA, Mkemia Mkuu wa serikali, Hospitali ya mkoa wa Mbeya, Rufaa, Ofisi ya kamanda wa polisi na NGO’s’’ alisema Kandoro.

Sanjari na hayo, alisema mkoa wa Mbeya unazalisha bangi, jambo ambalo serikali imeendelea kupambana nalo kwa kushirikiana na serikali za mitaa na vijiji ili kufichua wanaolima zao hilo.
 
 
*Tani 2.5 zanaswa


Wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya nchini, wamekamatwa huku wengine wakiendelea kusakwa.

Akieleza mbele ya waandishi wa habari, mchambuzi mkuu wa tume ya kudhibiti dawa za kulevya nchini, January Ntisi, alisema kuwa wafanyabiashara hao tayari wamefikishwa kwenye vyombo vya sheria.

“Kwa muda wa miezi sita tayari dawa za kulevya tani 2.5 zimekamatwa katika baadhi ya njia kuu ikiwemo bahari ya Hindi, bandari ya Dar es Salaam na wanaendelea kukamatwa’’ alisema Ntisi.

Mbali na jitihada hizo za serikali kudhibiti dawa hizo za kulevya hapa nchini, alisema kuna kazi ngumu ya kupambana na vigogo hao ambao alikiri kuwa mtandao wao ni mkubwa na wana uwezo wa kununua hata boti ziendazo kasi na manohari, lakini vyombo vingi vinaendelea kushughulika nao.

Kiongozi huyo, alilazimika kueleza jambo hilo baada ya kuulizwa kama tume yake inashindwa kutokomeza tatizo hilo nchini ili kuendelea kulinda ajira zao kwasababu wakitokomeza, kitengo hicho kinaweza kufutwa.

Ofisa kutoka kitengo cha mkemia mkuu wa serikali, Grolia Omary, alisema ofisi yake inafanya kazi kwa uadilifu mkubwa, hivyo tatizo la kwamba dawa zinabadilika kutokea ofisi yake si kweli, bali wao wanapima wanachopelekewa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...