Jumatatu, 29 Desemba 2014

ZIARA YA MABALOZI WA TANZANIA, UHURU PEAK

 Mabalozi wakiwa katika Mwamba wa Pundamilia “Zebra Rock” katika safari ya kuelekea Kilele cha Uhuru (Uhuru Peak).

(Picha zote na Charles Ndagulla)

Mlima Kilimanjaro (Tanzania) una vilele vitatu, Kibo, Mawenzi na Shira. Mlima huu umepewa heshima na kuingizwa katika maajabu saba hapa ulimwenguni hasa ikizingatiwa ni mlima uliosimama pekee yake bila kuungwa kwenye safu za milima kama ilivyo Everest (Asia) kwenye mapangano ya milima ya Himalaya, Drakensburg kwenye safu za milima ya Drakensburg (Afrika Kusini).


Mlima huu una urefu wa meta 5,895 sawa na futi 19,341 kutoka usawa wa bahari (a.s.l).
Ndagulla Blog inaufunga mwaka 2014 ikiwa na rekodi ya kuupanda mlima huo.
Tukio hili la kuupanda mlima lilianza Desemba 16 hadi 21 kupitia geti la Marangu hadi kilele cha Uhuru (Uhuru Peak).
Mandhari nzuri katika safari hiyo kunadhihirisha na namna gani mlima huu ulistahili kupewa heshima.
Katika safari hiyo Ndagulla blog iliongoza na Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi akiwemo Batlida Buriani anayeiwakilisha Tanzania nchini Kenya.
Balozi Lazia Msuya, anayeiwakilisha Tanzania huko Bondeni kwa Madiba alikuwepo katika safari hiyo ngumu.
Mabalozi wengine
Na.
Jina la Balozi
Nchi anayowakilisha
1
Dkt. Batlida Buriani
Kenya
2
Radhia Msuya
Afrika Kusini & Swaziland
3
Adadi Rajabu
Zimbabwe & Maritius
4
Dkt. Ladislaus Komba
Uganda
5
Mbarouk N. Mbarouk
UAE
6
Dkt. Aziz P. Mlima
Malaysia
7
Dkt. Bernard Achilwa
8
Shamimu Nyanduga
Msumbiji & Madagascar
9
Grace Mwijuma
Zambia
10
Patrick TSere
Malawi
11
Ramadhan Mwinyi
UN
12
Mbelwa Kairuki
Mkurugenzi wa Asia
13
Celestine Mushi
Mkurugenzi Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya nje
14
Daniel Ole Njoolay
Nigeria
15
Joseph Sokoine
Mkurugenzi Idara ya Amerika na Ulaya
16
John Kijazi
17
Charles A. Sanga
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii
Hebu Tazama mtiririko mzima wa safari hiyo.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumza na mabalozi kabla ya kuwakabidhi bendera ya taifa la Tanzania katika safari kuelekea kilele cha Uhuru (Uhuru Peak).


















Safari hiyo iliratibiwa na TANAPA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...