Jumatano, 10 Desemba 2014

KONGAMANO LA SIKU MBILI LA UKATILI WA JINSIA DHIDI YA WANAWAKE NA WALEMAVU LILILOANDALIWA NA SHIRIKA LA SEED TRUST LAFIKIA TAMATI MKOANI MOROGORO DESEMBA 9-2014

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Seed Trust, Margareth Mkanga (MB) akizungumza katika kongamano hilo. Kulia ni Mwenyekiti wa Shirika hilo, Stephen Mashishanga. Kongamano hilo la Majadiliano kuhusiana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na walemavu limeshirikisha wadau mbalimbali kutoka baadhi ya mikoa ya Tanzania na kuandaliwa na Shirika la Seed Trust la mjini Morogoro kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA).
Mwenyekiti wa Shirika hilo, Stephen Mashishanga, akichangia mada katika kongamano hilo.
Dk.Ernest Rugiga akitoa mada kuhusu afya ya uzazi.
Mwezeshaji Victor Mulimila akizungumzia kwa ujumla kuhusu vitendo vya ukatili. Kulia ni Dk.Ernest Rugiga
Ofisa Tarafa wa Manispaa ya Morogoro, Mlange Pakalapakala Jumamosi, akichangia mada kwenye kongamano hilo.
Wanahabari walikuwepo kwenye kongamano hilo wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi. wa Bwalo la JKT mkoani humo.
Maofisa wa Shirika la Seed Trust wakiwa kwenye kongamano hilo.

Washiriki wa kongamano hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...