Jumatatu, 14 Julai 2014

PROF. SIGALLA; DR. MWANJELWA ANAO UWEZO WA KIUONGOZI

 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akikaribishwa leo na wanawake katika ukumbi wa OTTU Mbeya, kwa ajili ya ufunguzi wa semina ya ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla.
 Wanawake hoyeee. Kulia ni mgeni rasmi, mkuu wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla.
 Baadhi ya washiriki ukumbini.
 Mwandaaji wa semina hiyo ya stadi za uongozi. Dr. Mary Mwanjelwa, akisema neno..
 Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla, akifungua semina ya wanawake, kuhusu stadi za uongozi Jijini Mbeya, katika ukumbi wa OTTU, ambapo wanawake kutoka wilaya tisa za mkoa wa Mbeya, walihudhuria.
 Mmoja wa watoa mada katika semina hiyo, Tumaini Mwakatika, akisema neno mbele ya kamera ya TBC1.
 Kulia ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akipongezwa  na Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla, kwa kuandaa semina ya stadi za uongozi kwa wanawake wa wilaya tisa za mkoa wa Mbeya.
MKUU wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla,  amewaasa wanawake nchini, kuacha kudharauliana ili waweze kufikia nafasi ya hamsini kwa hamsini katika uongozi.
 

Ameyasema hayo jana, alipofungua semina ya wanawake kutoka wilaya zote za mkoa wa Mbeya, iliyoandaliwa na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, MNEC, Dr, Mary Mwanjelwa, kuhusu stadi za uongozi na mbinu za kufanikiwa kisiasa ndani ya vyama vingi.



Prof. Sigalla, alisema kuwa, wanawake wengi wanashindwa kuchaguliwa kwenye nafasi mbalimbali kutokana na kutopendana na kutosimamisha mwanamke shupavu.



“Mkimsimamisha mwanamke kama Dr. Mwanjelwa, hata mimi nitamchagua siyo kwasababu ni mwanamke, bali kwasababu anao uwezo wa kuongoza na mwonekano’’ alisema Prof. Sigalla.



Mwandaaji wa mafunzo hayo, Dr. Mary Mwanjelwa, alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa wanawake, maana ukimwezesha mwanamke umewezesha jamii nzima.



“Mwanzo semina kama hii niliwaandalia madiwani wanawake wote wa mkoa wa Mbeya kisha na madiwani wanaume na sasa viongozi hawa ngazi ya matawi na kata ambao naamini watapeleka elimu watakayoipata kwa jamii’’ alisema Dr. Mwanjelwa.



Mmoja wa wawezeshaji wa semina hiyo ambayo inahusu mada ya stadi za uongozi na mbinu za kufanikiwa kisiasa ndani ya demokrasia ya vyama vingi, Tumaini Mwakatika, alisema kuwa semina hiyo ya siku tatu, itawawezesha wanawake hao kutambua mambo ya msingi katika uongozi.



“Watapata kujua changamoto za uongozi, nadharia ya uongozi na tabia za viongozi, mambo ya msingi katika uongozi na misingi ya utawala wa kidemokrasia na matarajio ya wananchi”alisema Tumaini Mwakatika.



Baadhi ya washiriki akiwemo Everada Mwangwala na Agatha Ngole, walisema kuwa, matarajio yao katika semina hiyo ni kupata ujasiri wa kujiamini kwa manufaa ya wananchi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...