Jumatano, 30 Julai 2014

MBEYA CEMENT YAWEKA MKONO UJENZI WA UWANJA WA KISASA WA MICHEZO CHUNYA MBEYA


Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro akikabidhiwa mifuko ya saruji na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya saruji ya Lafarge ya SONGWE mkoani Mbeya ikiwa ni sehemu mifuko 1000 iliyotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo wilayani Chunya.


 

UWANJA wa kisasa wa michezo utakaogharimu jumla ya sh. Bilioni 8, umeanza kujengwa wilayani Chunya Mkoani Mbeya.
 
 
Uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 50,000 pia unatarajiwa kuwa kitega uchumi cha aina yake kuwepo katika wilaya ya Chunya na mkoa wa Mbeya na katika wilaya za mikoa mingine nchini mbali na Jiji la Dar es salaam.
 
 
Akizungumzia ujenzi wa uwanja huo Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro alisema kuwa uwanja huo unajengwa na wananchi wenyewe kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya hiyo ambapo pendekezo la ujenzi wa uwanja huo aliliwasilisha kwenye vikao vya halmashauri na kuridhiwa na baraza la Madiwani.
 
 
Alisema katika vikao vyake, ambapo Halmashauri ya wilaya hiyo ilipendekeza kutenga Sh. Milioni 70 katika bajeti yake ya kila mwaka huku kila mwananchi akiwajibika kuchangia ujenzi wa uwanja huo kuanzia sh.2000 kwa kila mwaka ambapo matazamio uwanja huo unatarajia kukamilika 2016.
 
 
Katika mkakati wa ujenzi huo Kinawiro alisema kuwa wadau mbalimbali wamejitokeza kuchangia ujenzi wa Uwanja huo ambao upo katika hatua za awali wakiwemo Kampuni ya Lafarge inayozalisha saruji aina ya Tembo waliochangia saruji mifuko 1000.
 
 
Akizungumza wakati wa kuchangia ujenzi wa uwanja huo Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Lafarge Catherine Langreney alisema kuwa kampuni yake imepokea maombi hayo kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Chunya na kukubali kuchangia saruji mifuko 1000.
 
 
Langreney alisema kuwa mbali na kufanya biashara kampuni yake inachangia huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi waliopo maeneo ya karibu na kiwanda chao hivyo msaada huo ni sehemu ya huduma zao za kawaida kwa wananchi.
 
 
‘’Huduma zetu zinazingatia mahitaji ya jamii inayotuzunguka bila kujali faida,’’alisema Langreney.
 
 
Alibainisha kuwa kuwepo kwa uwanja huo kutatoa fursa ya ajira kwa wananchi wa maeneo hayo na kuinua uchumi wao.
 
 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya  Wilaya ya Chunya Sophia Kumbuli alisema kuwa uwanja huo utakuwa ni sehemu ya Mapato ya Halmashauri hiyo na kuwa wadau mbalimbali wamejitokeza kuchangia uwanja huo kwa nguvu zao na mali zao.
 
 
Alisema kuwa fursa ya kuwepo kwa uwanja huo wa kisasa itainua michezo ndani ya wilaya hiyo na mkoa wa Mbeya kwa ujumla hivyo wadau wanapaswa kujitokeza kuchangia maendeleo ya uwanja huo.
 
 
Naye Katibu wa Kamati ya Ujenzi wa uwanja huo Solo Tuyagaje alisema kuwa hadi sasa jumla ya sh. Milioni 107 zilichangwa na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na makampuni yanayochimba madini wilayani humo na wachimbaji wadogo.
 
 
Alisema wadau wengine waliochangia ni pamoja na Mbunge wa Lupa Victor Mwambalaswa aliyechangia jumla ya Milioni 11 ambapo Halmashauri ya wilaya imechangia jumla y ash. Milioni 30 kwa mwaka wa fedha wa 2013/14.
 
Credit;mkwinda blog

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...