MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Mbeya(CCM) Mary Mwanjelwa, amesema kuwa, uvunjifu wa masuala ya utawala bora umezidi kushamili zaidi Vijijini.
Ameishauri serikali kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha viongozi wa vijiji kuacha kujifanya miungu watu.
Hayo aliyasema juzi katika mkutano wa kamati ya ushauri ya mkoa wa Mbeya(RCC), uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa Jijini Mbeya.
Kwa upande wake Waziri wa nchi Ofisi ya Rais(Utawala
Bora) George Mkuchika amewataka watumishi wa umma kuzingatia maadili
katika utendaji wao ili kuepuka watendaji kupigiwa mifano ya utoaji na
upokeaji Rushwa.
Alisema serikali ya awamu ya nne
inaamini ujenzi na uimarishaji wa Utawala Bora ndiyo njia pekee yenye
ubora sahihi na yenye uhakika katika jitihada za kuondokana na matatizo
ya rushwa, umaskini na uendeshaji mbovu wa huduma za umma.
Alisema serikali kwa kuzingatia
muongozo wa Taaifa wa mwaka 1999 kuhusu Utawala Bora(Good Governance)
imeanzisha programu mbalimbali kwa lengo la kujenga na kuimarisha
Utawala Bora nchini.
Mkuchika alisema kuwa baadhi ya
programu hizo ni marekebisho ya kuboresha utendaji katika utumishi wa
umma(The Public Service Reform Programe) na marekebisho ya kuboresha
usimamizi wa fedha za umma (The Public Financial Management Programme)
na mareekebisho ya kuboresha mfumo wa uendeshaji wa serikali za mitaa(
The Local Government Reform Programme).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni