Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi(CCM) Taifa, Abdallah Majura Bulembo, akiwapa pole wanafunzi wa Sekondari ya Ivumwe, Jijini Mbeya jana, baada ya shule hiyo kupata janga la moto ulioteketeza mabweni saba ya wavulana wa shule hiyo, April 23, Mwaka huu na kusababisha hasara ya Milioni 30.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ivumwe Jijini Mbeya jana.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi(CCM) Taifa, Abdallah Majura Bulembo(kulia), akiwa anakagua moja ya bweni la wavulana wa shule ya Sekondari Ivumwe Jijini Mbeya jana, baada ya shule hiyo kupata janga la moto.
MWENYEKITI
wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania(CCM), Abdallah Majura Bulembo, ameamuru shule
zote zinazomilikiwa na jumuiya hiyo kote nchini kukata bima ya moto.
Agizo hilo
alilitoa jana mjini Mbeya, alipokuwa akikagua uhalibifu uliojitokeza baada ya
janga la moto kuteketeza mabweni saba ya wavulana katika shule ya Sekondari
Ivumwe, iliyopo Jijini hapa.
Alisema katika
bima ambazo ni rahisi na bei nafuu nchini ni bima ya moto, lakini ndiyo bima
pekee ambayo haikatwi na wananchi na taasisi nyingi.
“Kuanzia
sasa, suala la bima ya moto ni la lazima kwa shule zote za jumuiya ya wazazi wa
CCM Tanzania. Baraza kuu tutakutana kwa dharula mjini Dodoma Mei 17, mwaka huu
na tutakachokipata tutakileta haraka kwenu ili kusaidia katika janga hili la
moto’’ alisema Bulembo.
Mbali na
agizo hilo, aliwapa pole wanafunzi waliounguliwa na vitu vyao vyote na kuwataka
wawe wavumulivu, pia alitoa mchango wa Milioni tatu (3,000,000/=)kwa ajili ya
ukarabati wa mabweni hayo na mahitaji mengine ya haraka na kuahidi kuwashirikisha
wadau wengine wa elimu ili kuwasaidia wanafunzi waliokuwa wakiishi kwenye
mabweni hayo.
Mwenyekiti
wa bodi ya shule hiyo, Dr. Victoria Kanama, alimshukuru Mwenyekiti huyo wa
wazazi Taifa na kwamba kutokana na mchango wake, mabweni hayo yatakamilika
ndani ya mwezi mmoja.
“Umetupa
nguvu sana na tutahakiisha tunakarabati mabweni haya ndani ya mwezi mmoja na kufanya
jitihada za kuongeza ufanisi wa ufaulu katika shule yetu kuanzia kidato cha
kwanza mpaka kidato cha sita” alisema Dr. Kanama.
Kwa upande
wake mkuu wa shule hiyo ya Ivumwe, Emerry Muhondwa alisema janga la moto
lilitokea April 23, mwaka huu majira ya saa 3 hadi saa 4 asubuhi wakati wanafunzi
wapo madarasani.
“Mabweni
saba ya wavulana ndiyo yaliteketea na moto uliteketeza Vitanda 93, Magodoro 186,
mashuka 372, Mablanketi 186, mabegi 186, matranker 186 pamoja na vitabu na
madaftari, vyote vikiwa na jumla ya Milioni 30’’ alisema Mwalimu Mohondwa.
Katika taarifa
yake kwa Bulembo, mkuu huyo wa shule alisema kwa sasa wanafunzi hao wanalala
katika madarasa na wameazima magodoro katika shule ya wasichana ya Loleza ya
Jijini hapa.
Ivumwe, ni
kati ya shule zenye sifa ya kufaulisha, ambapo katika mtihani wa
utamilifu(Mock), kidato cha sita mwaka huu, shule hiyo imeshika nafasi ya pili
kati ya shule 26 zilizokuwa na watahiniwa 30 katika kanda ya Nyanda za juu
kusini mikoa ya Mbeya, Rukwa na Katavi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni