KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AMANI GREYSON
(22) MKAZI WA IPOROTO ALIUAWA NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA
MIKONONI BAADA YA KUMTUHUMU KUIBA NG’OMBE MMOJA MALI YA BABU YAKE AITWAYE GEOFREY SALAMU @ NGOLIA.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 20.04.2014
MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA MAONA, KIJIJI CHA TWINZI, KATA YA BARA, TARAFA YA ITAKA,
WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA MAREHEMU ALIKAMATWA NA ASKARI MGAMBO
NA KUWEKWA NDANI. INAELEZWA KUWA MAREHEMU ALIVUNJA MLANGO NA KISHA KUANZA
KUKIMBI NA NDIPO WANANCHI WALIMUONA NA KUMSHAMBULIA. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA - VWAWA. JUHUDI ZA KUWATAFUTA
WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA
WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA
KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA WILLY JUMA
(21) MKAZI WA MJERE AMEUAWA KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI NA MTUHUMIWA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NURU MSAFIRI
(21) MKAZI WA MJERE.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 20.04.2014MAJIRA
YA SAA 23:00 USIKU HUKO KATIKA
KIJIJI CHA MJERE, KATA YA MSHEWE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA YA MBEYA
VIJIJINI. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI ULEVI. TAARIFA ZA AWALI
ZINADAI KUWA MAREHEMU NA MTUHUMIWA NI MARAFIKI NA KABLA YA TUKIO WALIKUWA
PAMOJA KATIKA KLABU CHA POMBE.
MTUHUMIWA
AMEKAMATWA NA MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA
KWA UCHUNGUZI ZAIDI.
KATIKA MISAKO:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. JOYCE MWAKALINGA (30) MFANYABIASHARA NA
MKAZI WA ILOMBA NA 2. ASHA JOHN (28)
MKAZI WA LUBELE WAKIWA NA POMBE HARAMU YA
MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 17.
WATUHUMIWA HAO
WALIKAMATWA KATIKA MISAKO ILIYOFANYWA KATIKA MAENEO TOFAUTI MNAMO TAREHE 19.04.2014 NA 20.04.2014 MAJIRA YA SAA 12:45 MCHANA KATIKA WILAYA YA KYELA NA
JIJINI MBEYA. WATUHUMIWA NI WAUZAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAFANYIKA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUJIHUSISHA NA UUZAJI WA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
KATIKA MSAKO MWINGINE:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU WAPATAO 82 WOTE JINSI YA KIUME MIAKA KATI YA 18-30, RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI
BILA KIBALI.
WATUHUMIWA HAO
WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.04.2014
MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO
KATIKA KIJIJI CHA BUSALE, KATA YA BUSALE, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA,
MKOA WA MBEYA.
TAARIFA ZA AWALI
AMBAZO BADO ZINAFANYIWA UCHUNGUZI INASADIKIWA WATUHUMIWA HAO WAMETOKEA NCHINI
MALAWI BAADA YA KUFUKUZWA NA KISHA KUKIMBILIA NCHINI TANZANIA. KATIKA HARAKATI
ZA KUKIMBILIA NCHINI TANZANIA RAIA WEMA WALIWAONA NA KISHA KUTOA TAARIFA
ZILIZOSAIDIA KUKAMATWA. TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI KWA TARATIBU
ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA
KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA
MAENEO YAO ILI WAKAMATWE NA KUFANYIWA UCHUNGUZI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni