VYAMA viwili
pekee, ndivyo vimethibitisha na kurejesha fomu za kugombea nafasi ya Mwenyekiti
wa Mtaa wa Mbalizi, Mbeya Vijijini,mkoani hapa, ili kuunda mji mdogo wa
Mbalizi.
Msimamizi wa uchaguzi wa eneo hilo, ambaye ni afisa mtendaji
wa Kijiji cha Mbalizi, Malongo Sumuni, alivitaja vyama hivyo kuwa ni Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na Chama cha demokrasia na Maendeleo(Chadema).
Aliwataja
wagombea wa nafasi hiyo kuwa ni Asifiwe Godwin
Mwakalonge(CCM), na Elia Wilson
Mkono(Chadema), ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho na ni diwani wa
kata ya Utengule Usongwe kupitia Chadema.
“Mbali na
kurejesha fomu na kuteuliwa kuwania nafasi hiyo, hawaruhusiwi kufanya kampeni
mpaka zitakaporuhusiwa tarehe 30/11/2014 na mwisho itakuwa Desemba 13, mwaka
huu” alisema msimamizi huyo.
Alipoulizwa
idadi ya wakazi wa eneo hilo, alisema kuwa takwimu alizonazo zinaonesha wakazi
13,690, takwimu ambazo amesema siyo halisi.”Tuna vitongozji vitano ambavyo ni
Mlimareli yenye kaya 2900 wakazi 3700, Chapa Kazi kaya 1800 wakazi 3200, DDC
kaya 1534 wakazi 2320, Pipeline kaya 1250 wakazi 1650 na Mtakuja kaya 1650
chenye wakazi 3200” alisema Sumuni.
Uchunguzi umebaini kuwa, ofisi yake ilipelekewa idadi ndogo ya wakazi kwa
kile wenyeviti wa vitongozi walichokuwa wakihofia katika ukusanyaji wa michango,
kuwa endapo wakazi wachache wangechagia, wangesumbuliwa wao kufuatilia.
Mji huo wa
Mbalizi, ndiyo kitovu cha siasa za Jimbo la Mbeya Vijijini, ambapo vyama vine
vya siasa vimekuwa vikichuana vikiwemo Chama cha wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi,
CCM na Chadema.
Baadhi ya wananchi wa eneo hilo wameendelea kujiandikisha kwa ajili ya upigaji kura wa
viongozi wa serikali za mitaa ifikapo Desemba 14, mwaka huu, huku kila kituo
kikiwa na mawakala wa vyama vya siasa, hususani CCM na Chadema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni