Alhamisi, 6 Novemba 2014

KYELA..... AKAMATWA KWA KUWAUZIA WENZAKE NYAMA YA MBWA




MTU mmoja amekamatwa na Jeshi la polisi baada ya kuwauzia wananchi wenzake kitoweo cha Nyama ya Mbwa.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la polisi mkoani Mbeya kwa vyombo vya habari LEO, imesema kuwa, jeshi hilo linamshikilia kijana Ahadi Jesikaka(20), ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Ngyekye wilayani Kyela kwa kosa la kuwauzia watu nyama ya mnyama huyo.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi, Ahmed Msangi, imeeleza kuwa, tukio hilo lilitokea Novemba 4, mwaka huu.

‘’Tukio hilo limetokea tarehe 4.11.2014, majira ya saa saba mchana, huko katika kijiji cha Ngyekye, kata ya Matema, tarafa ya Ntebela wilaya ya Kyela mkoani Mbeya” imeeleza taarifa hiyo.

Watu waliouziwa na kutumia kitoweo hicho cha nyama ya Mbwa ni Enock Nsemwa(52), George Nsemwa(26) na Anyandwile Mbwilo(29), wote wakazi wa Ngyekye.

Kutokana na tukio hilo, jeshi la polisi limetoa wito kwa wananchi kuwa makini hususani wanaponunua vyakula ili kujiepusha na madhara ya kiafya yanayoweza kujitokeza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...