Ijumaa, 26 Septemba 2014

TAREHE YA USAILI WA JESHI LA POLISI TANZANIA KWA WAKAZI WA MBEYA.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, akizungumza na wanahabari ofisini kwake mkoani Mbeya.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, AHMED Z. MSANGI – SACP anawatangazia Wananchi wote ya kuwa vijana waliomaliza Kidato cha Nne mwaka 2013 na cha Sita mwaka 2014 na kuchaguliwa kufanya usalii wa kujiunga na Jeshi la Polisi, Usaili huo utafanyika kuanzia Tarehe 28.09.2014 hadi Tarehe 01.10.2014 kuanzia majira ya saa 08:00 Asubuhi hadi saa 16:00 jioni katika Shule ya Sekondari Mbeya Day.

Muhimu:

·         Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili aje na vyeti vyake vyote vya masomo [(Academic Certificate(s)/Results slip(s) & Leaving certificate(s)], nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (Original Birth certificate). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
·         Mwombaji awe na namba ya simu itakayotumika kumjulisha endapo atachaguliwa.
·         Kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili. Pia waombaji waje na kalamu za wino kwa ajili ya usaili wa kuandika.

Ni muhimu sana kwa kila mwombaji kuzingatia tarehe ya usaili na muda wa kuanza usaili.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...