Jumamosi, 27 Septemba 2014

FAMILIA YA WATU WANNE WAFA AJALINI SONGWE MBEYA, MKUU WA CHUO CHA UALIMU CHA ST. AGGREY, AJERUHIWA VIBAYA

Timu ya mafanikio ya taasisi ya St. Aggrey wakiwa katika picha ya pamoja. Mr. Danda wa pili kutoka kulia, ndiye aliyepata ajali.

****************************************************
AJALI mbaya imetokea majira ya saa tatu usiku jana tarehe 26/09/2014 huko eneo la Songwe karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa songwe, wilaya ya Mbeya Vijijini, na kuua watu wanne papo hapo na kusababisha majeruhi wawili.

Marehemu na majeruhi hao, walikuwa kwenye gari aina ya Noah, ambayo iligongana uso kwa uso na lori.

Watu hao imeelezwa kuwa walikuwa wakitokea wilayani Mbozi, wakiwa na mwenyeji wao Mr. Danda, ambaye ni Mkuu wa chuo cha ualimu cha St. Aggrey, Mbeya, ambaye amelezwa katika hospitali ya rufaa ya Mbeya.

Marehemu ni wenyeji wa mkoani Njombe ambapo taasisi ya St. Aggrey, imesafirisha miili hiyo ambayo tangu jana usiku ilikuwa imehifadhiwa katika hospitali ya Ifisi Mbaliz.

Mkurugenzi wa taasisi ya St. Aggrey, Mboka Mwambusi, amesema kuwa wanafanya mpango wa kumpeleka majeruhi katika hospitali ya taifa Muhimbili, ndugu Danda.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...