Sudan Kusini imeepuka baa la njaa lakini ukosefu wa chakula wasalia kuwa suala nyeti hasa mwakani.
Weledi wa
masuala ya mlo wameonya kwamba watu wengi wataathirika na njaa endapo
hatua za dharura hazitachukuliwa mara moja kuchanga fedha na kusambaza
vyakula nchini humo.
Ripoti
ambayo imetolewa hivi punde na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nchini
Sudan Kusini inasema kuwa ingawa hali ya chakula imeanza kuimarika hasa
msimu huu wa mavuno, kuendelea kwa vita kumemaanisha sekta ya kilimo
iliathirika na hali ilivyo sasa ni mbaya zaidi ikilinganishwa na miaka
mingine.
Maeneo ambayo hayajashuhudia vita yamechangia kuzalisha chakula nchini humo.
Licha ya hayo, imekadiriwa kuwa watu milioni moja u nusu wanakumbwa na ukosefu wa chakula.
Idadi hiyo
inatarajiwa kuongezeka maradufu ifikapo mwaka ujao endapo hatua za
dharura hazitachukuliwa kukabiliana na utapia mlo na njaa.
Ripoti hiyo imetolewa na mashirika 14 yanayofanya kazi nchini Sudan Kusini yakiwa pamoja na Umoja wa Mataifa.
Chanzo; BBC/SWAHILI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni