TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 09.09.2014.
KATIKA
TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA LEVIS MLENGA (43) MKAZI WA LUFITA NCHINI MALAWI ALIFARIKI DUNIA AKIWA AMEFUNGIWA
KATIKA CHUMBA KIMOJA KATIKA OFISI YA KATA BAADA YA KUPIGWA NA WANANCHI
WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KUTOKANA NA TUHUMA ZA WIZI WA NG’OMBE
WAWILI MALI YA EMMANUEL KILEMBE,
MKAZI WA KIJIJI CHA ILONDO.
TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA TAREHE 06.09.2014 HUKO KATIKA KIJIJI NA
KATA YA MALANGALI, TARAFA YA BULAMBYA, WILAYA YA ILEJE, MKOA WA MBEYA. INADAIWA
KUWA MAREHEMU ALIKAMATWA NA ASKARI POLISI WA NCHINI MALAWI NA ALIPOJARIBU
KUTOROKA NDIPO WANANCHI WENYE HASIRA KALI WALIMKIMBIZA NA WALIPOMKAMATA
WALIANZA KUMSHAMBULIA NA KUMSABABISHIA MAJERAHA SEHEMU ZA KICHWANI HALI
ILIYOPELEKEA KUTOKWA DAMU PUANI NA MDOMONI.
AIDHA, WATU WATATU WAMEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO
AMBAO NI 1. EMMANUEL KILEMBE 2. ITISON
NDIMBWA WOTE WAKAZI WA ILONDO NA 3.
FURAHA KIBONA, KAIMU MTENDAJI KATA YA MALANGALI. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA – ITUMBA.
KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA
KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA
KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA
TUKIO LA PILI:
WATU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. MORTINA
(30) 2. EDINA JASON (22). 3. PAULO MWANYALILA, PADRI KANISA LA
ROMANI CATHOLIC KYELA NA MWANAMKE MMOJA
AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA LAKE MARA MOJA WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA
MAGARI MAWILI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.241
BKZ AINA YA TOYOTA COASTER IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA
MAKAZI YAKE KUGONGANA NA GARI ISIYOFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI IKIENDESHWA
NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 08.09.2014 MAJIRA YA SAA
19:00 JIONI HUKO MAENEO YA GARIJEMBE, KATA YA UTENGULE, TARAFA YA BONDE LA
USONGWE, WILAYA YA MBALIZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUKUYU. AIDHA
KATIKA AJALI HIYO WATU WATATU WALIJERUHIWA AMBAO NI 1. SAMWEL ASANGA (34) 2. MAWAZO GASPER NA 3. MTOTO WA KIUME,
UMRI KATI YA MIAKA 02 – 03 AMBAYE
HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA LAKE.
CHANZO CHA AJALI HIYO BADO KINACHUNGUZWA. MIILI YA
MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA MAJERUHI WAMELAZWA
HOSPITALINI HAPO. MADEREVA WA MAGARI YOTE MAWILI WALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI
HIYO, JUHUDI ZA KUWATAFUTA ZINAENDELEA.
KATIKA
TUKIO LA TATU:
MTOTO WA MIAKA MIWILI (02) ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA GROLIA LEVOKATUS MKAZI WA ITEWE AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA
NA GARI ISIYOFAHAMIKA IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 08.09.2014 MAJIRA YA SAA
19:30 JIONI HUKO ITEWE, WILAYA YA MBALIZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA
MBEYA/IRINGA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA
JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA
KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA
USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. PIA ANATOA WITO KWA
WATEMBEA KWA MIGUU NA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA KUZINGATIA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI IKIWA NI PAMOJA NA KUVUTA MAENEO YENYE VIVUKO. AIDHA ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA [MADEREVA] AZITOE KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni