Alhamisi, 4 Septemba 2014

NENO LANGU KWENU

Itakuwa utakaposikia Sauti ya Bwana Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana Mungu wako atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani.

Na Baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.

Utabarikiwa uzao wa tumbo lako na uzao wa nchi yako na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya Ng’ombe wako na wadogo wa kondoo zako.

Litabarikiwa kapu lako na chombo chako cha kukandia unga. Utabarikiwa uingiapo na utabarikiwa utokapo. Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako, watakutokea kwa njia moja , lakini watakimbia mbele zako kwa njia saba.

Bwana ataiamuru Baraka iwe juu yako katika ghala zako na mambo yote utakayotia mkono wako, naye atakubarikia katika nchi akupayo Bwana Mungu wako.

Bwana atakuweka uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia, utakaposhika maagizo ya Bwana, Mungu wako, na kutembea katika njia zake. Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la Bwana nao watakuwa na hofu kwako.

Bwana atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako, katika nchi Bwana aliyowaapia baba zako kwamba atakupa.

Atakufunulia Bwana hazina yake nzuri, nayo ni mbingu, kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubarikia kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi wala hutakopa wewe.

Bwana Mungu atakufanya uwe kichwa, wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapoyasikiza maagizo ya Bwana Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya. Msipokengeuka katika maneno niwaamuruyo leo kwa lo lote, kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto, kwa kuifuata miungu mingine na kuitumikia.

Lakini itakuwa, usipotaka kuisikiliza sauti ya Bwana,  Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.

Utalaaniwa mjini, utalaaniwa mashambani, utalaaniwa kapu lako na chombo chako cha kukandia. Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maogeo ya ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo zako.

Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo, Bwana atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako uliyoniacha kwayo.

Bwana atakuambatanisha na tauni, hata atakapokwisha kukuondoa katika nchi uingiayo kwa kuimiliki. Bwana atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie.

Na mbingu zako zilizo juu ya kichwa chako zitakuwa shaba, na nchi yako iwe vumbi na mchanga; itakujilia juu yako kutoka mbinguni hata uangamie. 

Kumbukumbu la Torati 28; 1-24

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...