MBUNGE wa
viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, amewashauri wanawake kote nchini
kuwaheshimu wanaume ili nao wapendwe na kuthaminiwa kama yalivyoagiza maadiko
ya vitabu vya Mungu.
Aliyasema
hayo jana, katika viwanja vya CCM Ilomba Jijini hapa, alipokuwa
akiwahutubia wanawake wakati wa siku ya wanawake duniani na katika jukwaa la
wanawake wa kikristo Tanzania lililofanyika kanisa la Romani Parish ya
Mwanjelwa.
Alisema
Mwanaume ni kichwa cha nyumba lakini mwanamke ni nguzo, na wanaume wanawacheka wanawake kwasababu
hawapendani, hivyo alihimiza upendo, kukosoana kwa hekima na kusameheana kwa
wanawake.
‘’Nalipongeza
dawati la jinsia la Jeshi la polisi ambalo linapambana na suala zima la
unyanyasaji wa kijinsia. Tukiwa na wanawake wanaopendana na kuonyana kwa hekima
tutafaulu kutokomeza mfumo dume’’ alisema Dr. Mwanjelwa.
Alisema
wanawake wana nguvu za kuutumikia umma na mfano mzuri ni kwamba mwanamume
akitangulia mbele za haki, mwanamke anao uwezo mkubwa wa kuwalea watoto na
kuwasomesha kwa kufanya ujasiliamali tofauti na akitangulia mwanamke.
Mchungaji wa
chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU), Mary Kategile, ambaye ni mjane mwenye
watoto saba na wajukuu saba, aliwataka wanawake kujitambua kuwa wana thamani
kubwa mbele za Mungu.
Katibu wa
wanawake wakristo jukwaa la Mbeya, Joyce
Mbeyela, alisema wanawake hao,
wanashughulika na masuala ya maombi na kutembelea wahitaji wakiwemo wagonjwa wa
majumbani, yatima, wasiojiweza, wazee na wajane.
‘’Ibada hii
ya maombezi inalenga kuvunja ukatili wa watoto, walemavu na wazee ikiwa ni
pamoja na kuombea viongozi wa dini hasa mauaji ya viongozi, umoja wetu, nchi
yetu, Bunge la katiba, vijana, ndoa na Mbunge Mary Mwanjelwa’’ alisema Joyce.
Akisoma
risala ya maadhimisho ya wanawake wa Jiji la Mbeya, Rehema Ngao, alisema
ubaguzi wa kijinsia umekuwa unawaweka wanawake na wasichana katika wakati mgumu
hasa wanapopambana na maisha.
Mwalimu
Cecilia Ndele, aliuambia mtandao huu kuwa, wanafunzi wa kike na kiume wamekuwa waathirika wakubwa
katika ndoa zenye migogoro na kufikia hatua ya talaka.
Alisema
wanandoa wanaotarakiana, watoto wao wanabeba mzigo wa kulea familia na
kushindwa kuhudhuria vema masomo huku baadhi ya watoto wa kike wakijiingiza
katika vitendo vya ngono za utototni.
‘’Maadili
yameporomoka, baadhi ni kutokana na Mama zao ambao wamekithri kwa matusi na
malezi ya kuiga nchi za magharibi ndiyo maana leo hii watoto wa kike wenye
miaka 10-12 hawana bikra zao na wakiolewa wanaachika haraka’’ alisema Mwalimu
Cecilia Ndele.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni