AHMED Z. MSANGI-SACP. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
VITENDO vya ubakaji mkoani Mbeya, vimekuwa tishio kwa wanawake na watoto wa kike na kufikia wastani wa kila siku wanawake kubakwa.
Akitoa tathimini
ya uhalifu mkoani hapa kwa kipindi cha mwezi Februari na Januari mwaka huu,
Kamanda wa polisi SACP Ahmed Msangi, alisema zaidi ya wanawake 70 wamebakwa kwa
kipindi hicho.
Msangi
alisema katika makosa dhidi ya binadamu, mwezi Januari vitendo hivyo vilitokea
44 sawa na asilimia 23 na mwezi Februari vilitokea matukio 36 sawa na asilimia
18.
Akieleza kuhusu
vitendo vya ulawiti, alisema mwezi Januari vitendo 6 na mwezi Februari
vilitokea vitendo vitano sawa na asilimia 17.
Usafirishaji
wa binadamu vitendo vitatu vimetokea mwezi Februari wakati mwezi Januari hakuna
tukio ambalo liliripotiwa katika vyombo husika.
Alivitaja vitendo
vingine vya kuhalifu vilivyojitokeza katika mkoa huu kuwa ni pamoja na makosa
ya kuwania mali ikiwemo Unyang’anyi wa kutumia silaha, kutumia nguvu, uvunjaji,
wizi, wizi wa Pikipiki na wizi wa mifugo.
‘’Makosa
dhidi ya maadili ya jamii yatokanayo na jitihada za polisi kwa kushirikiana na
wadau na wananchi mbalimbali ilikuwa ni kupatikana na silaha, Bhangi, Nyara za
serikali, Pombe ya moshi na wahamiaji haramu’’ alisema Kamanda Msangi.
Kwa upande
wa matukio ya usalama barabarani ambako baadhi ya wananachi wanalalamikia hisia
za vitendo vya rushwa dhidi ya askari na makondakta, alisema mabadiliko makubwa
yatatokea hivi karibuni na kupunguza hisia hizo kwa jamii kama si kuondoa
kabisa.
Aliyataja matukio
yaliyotokea kuwa ni pamoja na ajali za kawaida, ajali za vifo huku akiwataja
waliokufa mwezi Januari kuwa walikuwa 30, mwezi Februari 18 na waliojeruhiwa
Januari 49 na mwezi Februari walikuwa 22 huku makosa ya ukiukwaji wa sheria za
barabarani Januari yalikuwa 4,378 na
mwezi Februari yalikuwa 3,788.
Alisema kutokana
na tathimi hiyo, jeshi la polisi mkoani hapa, linajivunia ushirikiano wa
wananchi na kuendelea kupunguza uhalifu.
‘’Mimi
najitambua, umri wangu najua nimebakiza miaka mingapi jeshini, siwezi kuacha
maadili ya kazi na kumlinda mtu, askari yeyote ambaye anaenda kinyume na
maadili ya jeshi na tayari wengine wameanza kukiona’’ alisema Kamanda Msangi
huku akiwa sura ya msisitizo wa kukerwa na taarifa mbaya dhidi ya askari
wanaotuhumiwa kukiuka maadili ya jeshi hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni