Jumapili, 2 Machi 2014

MBEYA CITY YASHINDWA KUENDELEZA UBABE KWA JKT OLJORO YATOKA 0-0



LIGI kuu ya Vodacom imeendelea leo jioni katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya kwa kuzikutanisha timu za Mbeya City na JKT Oljoro ambapo hadikipyenga cha mwisho kinapulizwa timu hizo zimetoka suluhu ya bila kufungana.
Mechi hiyo ambayo ilihudhuriwa na watazamaji wachache kutokana na tiketi kuuzwa sh.5,000 badala y ash. 3,000 ilianza kwa kasi kwa kila timu kulishambulia lango la mwenzie.
 
Mashabiki wachache waliohudhuria mechi hiyo walikosa ladha halisi ya mchezo huo kutokana na timu hizo kutoonesha kandanda safi na hivyo kuwa ni mpira wa piga nikupige.
 
Hadi Kipindi  cha kwanza kinamalizika timu zote zitoka uwanjani bila kufungana ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadiliko, Mbeya City walibadilisha wachezaji wa watatu na JKT Oljoro ilibadilisha wachezaji wawili.
 
Mbeya City iliwaingiza Peter Mapunda badala ya Francis Casto,Mwagane Yeya aliingia badala ya Jeremiah John na Deus Kaseke aliingia badala ya Alex Sethi, wakati kwa upande wa timu ya Oljoro Hasira Hamis aliingia badala ya Uda Solita na Paul Malipesa alichukua nafasi ya Babu Ally Seif.
 
Hadi kipenga cha kumaliza mpira cha mwamuzi Martin Saanya kinapulizwa timu hizo zimetoka suluhu ya bila kufungana.
 
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa chama cha Mpira wa miguu mkoa wa Mbeya (MREFA) aliwaomba radhi wapenzi wa soka Jijini Mbeya kutokana na tiketi kuuzwa bei ya Sh.5,000 badala ya Sh.3,000 na bei hiyo imepangwa na Shirikisho la Soka nchini TFF.
 
Alisema hali hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza mapato ya mechi hiyo kutokana na idadi ya mashabiki wachache walioingia uwanjani ikiwa ni pamoja na tiketi kuchelewa kuuzwa.
 
Leoligi hiyo inaendelea kwa kuwakutanisha maafande wawili ambao ni timu mwenyeji ya Prison inayoikaribisha timu ya Mgambo JKT kutoka mjini Tanga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...