Jumanne, 25 Machi 2014

KIKUNDI CHA WATU WANAOISHI NA VVU, CHAPANIA KUJIKWAMUA KIUCHUMI..

 Wanakikundi cha Matumaini wakiwa na vifaa vya kilimo kwa ajili ya shamba lao lililopo katika kijiji cha Ikokoto, Wilayani Kilolo. Ni kijiji cha mwisho kuanza mlima kitonga.
Mmoja wa wanakikundi akilisha mifugo yake..
 
NA FRANK KIBIKI
 
Kikundi cha watu wanaoishi na VVU, cha matumaini kilichopo Ikokoto, Wilayani Kilolo kimepania kujikwamua kiuchumi, kutokana na shughuli zao za kilimo, ili kuondokana na ugumu wa maisha.
 
Wanachama wote wa kikundi hicho, wamekuwa wakijadili masuala yahusuyo afya zao, sambamba na namna ya kupata lishe bora ili waweze kuwasaidia watoto wao na familia zao.
 
Wenyewe, hawana wasi wasi na wanaufurahia umoja wao, kwani wawapo kazini hufanya kazi kwa bidii na wanaimani, kwamba hakuna maisha magumu ikiwa utaamua kupiga kazi....
 
Chanzo;mwitikio blog

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...