Bingwa wa magonjwa ya
Akinamama pamoja na Uzazi Dr. John Frances akifafanua jambo juu ya ugonjwa
wa Fistula katika hospitali ya wazazi Meta Jijini Mbeya.
Baadhi ya
wagonjwa wa Ugonjwa wa Fistula toka maeneo mbalimbali ya mkoa wa mbeya ambao
wamelazwa katika hospital hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
IDADI ya wagonjwa wanaokwenda kutibiwa ugonjwa fistula katika Hospital ya
Rufaa Mbeya kitengo cha Wazazi (META) na vituo vingine vya afya katika jiji la Mbeya imeendelea kupungua
mwaka hadi mwaka.
Bingwa wa Magonjwa ya Akina mama na Uzazi ambaye pia ni Mkuu wa
Hospital ya Wazazi Meta, Dr. Frances John amethibitisha jambo hilo.
Amesema
kupungua kwa ugonjwa huo, kunatokana na juhudi za serikali na
wadau katika utoaji wa elimu na
upatikanaji wa matibabu yenye uhakika.
Katika Hospital hiyo wanahakikisha wanadhibiti ugonjwa huo
hasa kwa mama ambaye anataka kujifungua na wapo madaktari Bingwa pamoja na
vifaa vya kutosha.
Amefafanua kuwa, asilimia kubwa ya wajawazito wanaopata ugonjwa huo wamekuwa
wakikaa na uchungu kwa muda mrefu bila
kuhudhuria katika vituo vya afya kitendo ambacho kimechangia kuwepo kwa hali
hiyo.
Ametoa
wito kwa Madaktari ambao wamesomea magonjwa ya akina mama kuhakikisha
wanawasaidia akina mama ambao wanasumbulia na ugonjwa huo kwani ni ugonjwa wenye kutia aibu ambao pia umechangia kwa asilimia kubwa kuwepo
kwa manyanyaso ndani ya familia zao
pamoja na jamii kuwatenga.
Dalili za ugonjwa huoni maumivu, kutokwa haja kubwa laini bila mgonjwa
kujitambua, hivyo kuchafua nguo hivyo hali hiyo humsababishia mgonjwa msongo wa
mawazo, kutokujiamini na adha katika jamii kutokana na kutoa majimaji hayo ya
choo ambayo huwa na harufu mbaya.
Credit; jamiimoja.blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni