Jumanne, 25 Machi 2014

ANGLIKANA YAKABIDHI BAISKELI KWA WAELIMISHAJIRIKA WA UWAKI

Afisa Mradi wa UWAKI wa kanisa la Anglikana Bw.Patrick Cosima(aliyevaa skafu)akimkabidhi afisa mtendaji wa kata ya Ilembo Jairo Shira baiskeli kwaajili ya kuwakabidhi waelimishajirika wa mradi huo kutoka kata za Ilembo na Masoko BAISKELI 22 zenye thamani ya jumla ya shilingi 3,740,000 zimekabidhiwa kwa waelimishaji rika wa mradi wa Kupinga ukatili wakijinsia(UWAKI) na ukatili dhidiya watoto katika kata za Ilembo na Masoko wilayani Mbeya. 

Baiskeli hizo zimekabidhiwa mwishoni mwa wiki na kanisa la Anglikana linaoendesha mradi huo katika kata hizo kwa hisani ya watu wa marekani kupitia shirika la Watereed.

Akikabidhi baiskeli hizo,Afisa mtendaji wa kata ya Ilembo Jairo Shira amewataka waelimishaji rika kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi wao. 

Shira ameendelea kusisitiza kuwa suala la kupinga ukatili wa kijinsia ni jukumu la kila mwana jamii kutokana na athari mbaya za ukatili huo ambazo ni pamoja na kushuka kwa uchumia wa familia husika. 

Kwa upande wake afisa mradi wa UWAKI wa kanisa la Anglikana Patrick Cosima amesema ni imani ya kanisa kuwa kwa kuwawezesha waelimishaji rika kuwa na usafiri wa baiskeli wataweza kuifikia jamii kwa haraka zaidi na kueneza elimu ya kupinga ukatili.

Cosima amesisitiza kuwa kutolewa kwa baiskeli hizo ni mwanzo wa kuhakikisha jamii yote ya wakazi wa kata za Ilembo na Masoko inabadilika na kuwa mfano wa kuigwa kwa wakazi wa maeneo ya jirani kwa kuacha vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...