Jumatatu, 24 Machi 2014

SIMANZI; BABA AMNYONGA MWANAYE!

 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA, AHMED MSANGI.

MTOTO Henry Juma, mwenye umri wa miezi saba, mkazi wa Migombani mjini Tunduma wilayani Momba mkoani hapa, amekutwa ameuawa kwa kunyongwa shingo na Baba yake mzazi, Juma Venance, kisha mwili wake kulazwa kitandani.

Tukio hilo lilitokea Machi 22, mwaka huu, eneo hilo, ambapo baada ya baba huyo (Joka) kufanya ukatili huo, alifunga mlango kwa nje na kufuli na kutokome mahalai kusikojulikana.

Makachero wa Jeshi la polisi kwa kushirikiana na raia wema, walipovunja mlango na kuingia ndani, walikuta maiti ya mtoto huyo ikiwa na upweke kitandani.

Baada ya kuusogelea, walikutana na ujumbe uliokuwa umeandikwa kwenye karatasi ukisomeka ‘’Unyama unyamani, tutafute pesa kwanza niite J.M.A.K.A GAIDI’’

Ujumbe huo unasadikika kuandikwa na mtuhumiwa ambaye mpaka sasa anatafutwa ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Jeshi la polisi mkoani hapa, limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na jamii imeombwa kusaidia kupatikana kwa mtuhumiwa huyo popote alipo.

NB; Uongozi wa Mtandao huu wa kijamii wa www.marymwanjelwa.blogspot.com unalaani vikali mauaji ya namna hii.

TUKIO LA PILI MKOANI HAPA:

BIBI MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LENNAR  KALINGA,  MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 60-70 MKAZI WA IPINDA AFARIKI DUNIA BAADA YA NYUMBA YA NYASI ALIMOKUWA AKIISHI KUSHIKA MOTO NA KUTEKETEA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 22.03.2014 MAJIRA YA SAA 22:25 USIKU HUKO KATIKA KATA YA IPINDA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA. CHANZO CHA MOTO HUO INADAIWA NI BAADA YA MAREHEMU AKIWA NA MUME WAKE KUWASHA KIBATARI KWA LENGO LA KUFUKUZA SIAFU WALIOKUWA WAMEINGIA NDANI NA NDIPO MOTO ULIPO LIPUKA NA KUSHIKA PAA LA NYUMBA HIYO LILILOKUWA LIMEEZEKWA KWA NYASI KAVU NA KUWAKA. MAREHEMU KWA KUONA HIVYO ALIAMUA KURUDI NDANI YA NYUMBA HIYO KWA LENGO LA KUTOA VITU VILIVYOKUWA NDANI NA NDIPO MOTO ULIPOMZIDIA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA KYELA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA MAKINI NA MAJANGA YATOKANAYO NA MOTO KWANI YANA MADHARA MAKUBWA KWA JAMII.

KATIKA TUKIO LA TATU:

MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI CHEKECHEKEA ILONGO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ONESMO HAULE (6) MKAZI WA MKAZI WA MAHENJE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJIRI T.597 BGU AINA YA  TOYOTA COASTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA STANLEY ELIA MWANDA (44) MKAZI WA MWANJELWA JIJINI MBEYA.
            AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 22.03.2014 MAJIRA YA SAA 10:30 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOI CHA ILONGA, KIJIJI NA KATA YA MAHENJE, TARAFA YA MLOWO, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA.

CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI, DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA VWAWA - MBOZI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA NA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI NA WALIMU KUWAELEKEZA WATOTO NAMNA SALAMA YA KUVUKA BARABARA IKIWA NI PAMOJA NA KUVUKA KATIKA MAENEO YENYE VIVUKO [ZEBRA CROSSING].

KATIKA TUKIO LA NNE:

MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI KIWIRA DARASA LA TATU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EVA MATHIAS (11) MKAZI WA KIJIJI CHA IBILIRO AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUSOMBWA NA MAJI YA MTO KIWIRA BAADA YA KUTELEZA KATIKA DARAJA LILILOJENGWA  KIENYEJI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 20.03.2014 MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA ILONGO, KIJIJI CHA IBILIRO, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE. WAKATI TUKIO HILO LINATOKEA MAREHEMU ALIKUWA NA DADA YAKE AITWAYE VERO LUCAS (20)  AMBAE ALITOA TAARIFA ZA KUTOKEA KWA TUKIO HILO NA NDIPO JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZILIPOFANYIKA NA HATIMAE MWILI WAKE KUPATIKANA MNAMO TAREHE 23.03.2014 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI MAENEO YA CHUO CHA MAGEREZA KIWIRA KATIKA MTO HUO HUO.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUACHA TABIA YA KUWATUMA WATOTO PEKE YAO MAENEO YA PORINI KWANI NI HATARI HASA KIPINDI HIKI CHA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA.

Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

KATIKA TUKIO LA PILI:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...