Jumamosi, 22 Machi 2014

HUJUMA ZA MIUDOMBINU YA MAJI, YASABABISHA VINYESI KUZAGAA

 Huu ni mfuniko wa chemba ya maji taka, ambapo mifuniko ya chuma imekuwa ikiibwa na wahalifu jambo ambalo linaendelea kuikwamisha kutoa huduma bora Mamlaka ya maji Mbeya na kutokea malalamiko hasa nyakati za mvua ambapo maji yakiingia, chemba nyingi zinafurika uchafu.
 Juu na chini, maandamano yakiwa katikati ya Jiji la Mbeya.
 Maandamano yakiendelea. Hapa tayari safari ya kurudi ofisi za Mamlaka kwa ajili ya hotuba na sherehe kwa ujumla.

 Hiyo ndiyo kauli mbiu ya mwaka huu 2014. UHAKIKA WA MAJI NA NISHATI
 Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji Mbeya, Mhandisi, Simon Shauri na Mwenyekiti wa bodi wa Mamlaka hiyo, Jaji Atuganile Ngwala(wa pili kushoto), wakiongoza maandamano ya mshikamano.

 Kulia ni Mwanafunzi OMBENI, wa shule ya Msingi Isanga, anayesoma darasa la tatu, akiwa na kuni pembeni ya maandamano hayo ya mshikamano ambayo hayajaleta bugudha yeyote ya kijamii katikati ya Jiji la Mbeya na njia zote yalipopita.


 Sasa tunakaribia kufika na kuhitimisha maandamano yetu......

 Maandamano yakiingia kwenye lango kuu la ofisi za Mamlaka ya maji Mbeya...
 Kisima cha Mamlaka ya Maji Mbeya, ambacho kinatumika kwa kufuga samaki. Kipo katikati ya ofisi za maji Mbeya eneo la Ujenzi Jijini Mbeya. 



IKIWA mwishoni mwa wiki imefanyika sherehe ya kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji, wananchi wa eneo la DDC Kalobe Jijini Mbeya, wameilalamikia Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Jijini hapa (MBEYA-UWSA) kushindwa kutengeneza miundombinu imara ya maji taka.

Wananachi hao walisema kuwa, familia zao zipo hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko hasa watoto baada ya kila inaponyesha mvua, matenki(Chember) za maji machafu kufurika vinyesi na kuzagaa kwenye maeneo wanayoishi.

Walisema kuwa, taarifa hizo wamezifikisha kwenye mamlaka husika lakini bado tatizo linazidi kuwa kubwa.

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo ambaye pia ni Mhandisi wa ufundi, Martin Kimambo, alipohojiwa alikiri kuwepo kwa tatizo hilo nyakati za mvua kwa kile alichosema kuwa ni kutokana na wizi wa mifuniko ya chuma ya chemba hizo kukithiri.

‘’Tatizo hilo lipo kutokana na Mamlaka kuhujumiwa na wahalifu ambao wanaiba mifuniko ya chemba za maji machafu, hivyo maji yanapokuwa mengi yanasababisha chemba zingine kuzidiwa’’ alisema Injinia Kimambo.

Alisema chemba za Mamlaka hiyo, zina uwezo wa kuhimili maji yanayotumika kwenye vyoo tu, hivyo mvua zinaponyesha na maji kujaa kwenye chemba ambazo zimeibiwa mifuniko ambayo kila mmoja haupungui Shilingi Laki mbili, ndiyo chanzo cha wananchi walio katika maeneo ya  kalobe kupata tatizo hilo.

Katika tatizo hilo, imegundulika kuwa mifuniko mingi imeibwa eneo la katikati ya Jiji likiwemo eneo jirani na kituo kikuu cha Polisi mkoani hapa, ambayo inasadikika kuwa wezi hao wanaiuza kama vyuma chakavu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Mhandisi, Simeon Shauri, alizitaja changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni pamoja na baadhi ya vyanzo vya maji kuendelea kupungukiwa maji, hali inayochangiwa na uharibifu wa mazingira pamoja na mabadiliko ya haidrolojia.

Alitaja baadhi ya vyanzo vinavytishiwa na upungufu huo wa maji kuwa ni pamoja na chanzo cha mto Lunji na Mfwizimo na Iduda.

‘’Wizi wa dira za maji na uhujumu wa miundombinu ya Majisafi na maji taka na baadhi ya wateja hususani Taasisi za umma kutolipa ankara za maji kwa wakati au kutolipa kabisa’’ alieleza changamoto hizo, Mkurugenzi Mtendaji huyo.

Mbali na changamoto hizo aliyataja mafanikio ya Mamlaka hiyo kuwa ni pamoja na kuzalisha maji safi na salama na kuyasambaza kwa wakazi takribani asilimia 96 wa Jiji la Mbeya, wanaopata huduma hiyo kati ya masaa 15-24 kila siku.

Mafanikio mengine alisema ni kuendelea kuboresha miundombinu kupitia miradi ya wafadhili na kufanikiwa kupeleka maji uwanja wa ndege wa Songwe na kuendelea kufanya juhudi za kuhifadhi vyanzo vya maji kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...