Watoto waliohai ambao Madaktari wanaendelea kuwapa matibabu katika Hospitali ya Wazazi Meta Mbeya.
*Baridi na
usafi vyatajwa chanzo cha vifo
*Mapacha waliobaki
wanaharisha, wawekwa chini ya uangalizi.
MADAKTARI wa
hospitali ya Rufaa ya Mbeya kitengo cha wazazi(META), wametaja chanzo cha mapacha
wawili kati ya wanne wa Aida Nakalawa(25), mkazi wa Chiwanda wilaya ya Momba
mkoani hapa, aliyejifungua watoto Januari mosi mwaka huu.
Wawamesema watoto hao baada
ya kuruhusiwa kutoka hospitalini, walikumbwa na ugonjwa wa kuharisha na kubanwa
na kifua.
Daktari ambaye hakutaka kuandikwa jina lake kwa kile alichodai kuwa siyo
msemaji, alisema waliwapokea mapacha watatu Machi 4, mwaka huu, huku mmoja
akiwa na hali mbaya zaidi ya wenzake.
Alisema muda
mfupi mtoto mmoja alifariki kwa kile walichobaini kuwa alikuwa ameshambuliwa na
uchafu kifuani ambao ulimsababishia kushindwa kupumua.
Alipoulizwa
ruhusa ya mama huyo baada ya kujifungua, alisema kuwa Mama huyo alikatazwa
kuondoka hospitalini, lakini yeye alilazimisha kuondoka na baadaye aliruhusiwa.
‘’Hawa
waliobaki baada ya vipimo tuligundua kuwa hawana matatizo yeyote ya moyo, bali walikuwa wanaharisha na kukohoa sana,
tunajitahidi kuokoa maisha yao wanaendelea na matibabu’’ alisema Dr. Paul.
Kwa upande
wake Aida Nakalawa, alisema huo ni uzao wake wa Nne na mtoto wake wa kwanza ana
umri wa miaka saba na mwingine miaka mitano na mwingine alifariki kabla ya
kujifungua mapacha hawa wanne ambao wawili wameaga dunia.
Alijifungulia
katika Hospitali ya Vwawa wilayani Mbozi Januari 1, mwaka huu, ndipo
alipohamishiwa hospitali ya Meta kwa ajili ya kuwatunza watoto hao wanne ambao
walikuwa na uzito wa Kg.2, 1.9, 1.6 na 1.5.
‘’Tunaishi
na mume wangu njia ya kutoka Tunduma kwenda Sumbawanga. Mazingira ya Nyumbani
siyo mazuri sana. Niliomba niruhusiwe kutolewa hapa baada ya kuwakumbuka watoto
wangu, wakanikatalia, lakini baadae nikaruhusiwa, nilipofika nyumbani watoto
wakanenepa, lakini wakaaza kuumwa wakikohoa na kuharisha, mmoja akafa’’ alisema
Aida, huku akiinama chini.
Kuhusu
kuwanyonyesha, alisema alikuwa akiwanyonyesha na kuwapa maziwa watoto wake wote
wanne kama alivyoshauriwa na wataalam mpaka wanafariki wawili kati yao.
Mpaka jana
anasemaa hajui hatima ya watoto wake kwa kile alichodai kuwa kwa sasa ameelezwa
kuwa muda wowote anatakiwa kwenda katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwasababu
katika kitengo hicho cha wazazi hawaruhusiwi kuhudumia watoto waliozidi umri wa
kuanzia miezi miwili.
Mapacha
wawili walio haia, wapo katika chumba cha joto katika hospitali ya Rufaa ya
Mbeya kitengo cha wazazi Meta wakiendelea kupata matibabu na kunyonyoshwa kila
baada ya masaa mawili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni