KAMANDA wa UVCCM Mbeya Vijijini, ORAN
NJEZA, akihutubia wananchi wa eneo la Jojo, kata ya Santilya, wilaya ya
Mbeya, kwenye kampeni za udiwani, ambapo alishangiliwa aliposema kuwa
''Kipele kimempata mkunaji'' akiwa na maana kuwa anatosha kuwa kamanda
wa UVCCM wilayani humo.
KAMANDA wa UVCCM Mbeya Vijijini, ORAN NJEZA,(kulia),akizungumza na vijana wa UVCCM kata ya Santilya wilaya ya Mbeya, Jimbo la Mbya Vijijini, jana.
Mkutano wa kampeni Jojo kata ya Santilya wilaya ya Mbeya.
KAMANDA wa UVCCM Mbeya Vijijini, ORAN NJEZA,(kulia),akizungumza na vijana wa UVCCM kata ya Santilya wilaya ya Mbeya, Jimbo la Mbya Vijijini, jana.
Mkutano wa kampeni Jojo kata ya Santilya wilaya ya Mbeya.
MTAALAM
aliyebobea katika masuala ya mifumo ya benki barani Afrika, Oran Njeza, amesema
kuwa ajira nzuri iliyobaki kwa vijana wa kitanzania ni kilimo.
Hayo ameyasema
jana Februari 8, mwaka huu, alipokuwa akizungumza na vijana wa kata ya Santilya wilaya ya Mbeya, Jimbo
la Mbeya Vijijini wakiwa wanajiandaa kuelekea katika uchaguzi mdogo wa udiwani
wa kata hiyo, uliomalizika jana jioni.
Njeza,
ambaye pia ni kamanda wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) UVCCM katika wilaya
hiyo, alisema vijana wengi hawawezi kumwelewa kirahisi kwasababu ya mazoea.
‘’Najua
wengi hamnielewi, lakini ajira nzuri Tanzania ni kilimo ambacho kwa hekali moja
ukilima vizuri, kwa mwaka unaweza kupata Milioni mbili na zaidi, sifanyi
utafiti maana mimi nimeacha kazi za benki Lagos nchini Nigeria sasa nalima, na
nimelima karibia maisha yangu yote’’ alisema Njeza.
Akijibu maswali
ya vijana hao ambao baadhi walihoji kuwa tatizo ni upatikanaji wa ardhi na
masoko, alisema siyo kweli, kwasababu katika nchi ambayo haina tatizo la ardhi
ni Tanzania. Ila vijana wengi wanachagua ardhi na wanataka kulima maeneo ya
kwao tu, ila suala la soko alikiri kuwepo na tatizo hilo.
Aliwaonya vijana
kote nchini, kujiepusha kuanzisha vurugu katika chaguzi mbaimbali kwa kutumiwa
na wanasiasa ambao kiuhalisia hawawezi kubadilisha maisha yao kiuchumi bali wao
wenyewe wanapaswa kutia bidii katika kufanya kazi.
‘’Taifa
linapoharibika wanaoumia ni vijana kwa kutumika kwenye miparaganyiko na
wanasiasa, kila mmoja ajiulize anawajibu gani kwa taifa maana ukitaka ushindi
mzuri siyo magoli bali ni uchumi. Mimi nipo tayari kushirikiana kwa ushauri na
yeyote anayetaka kujishughulisha katika kilimo ili kujikwamua kiuchumi’’alisema
Njeza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni