Jumapili, 9 Februari 2014

MBUNGE WA CCM MBEYA VIJIJINI, AJERUHIWA KWENYE UCHAGUZI MDOGO SANTILYA

 Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini Mch. Luckson Mwanjale.(Picha na maktaba ya kalulunga media)

*SABA WAKAMATWA, WENGINE WASAKWA.

MBUNGE wa Mbeya Vijijini, Mchungaj Luckson Mwanjale, amejuruhiwa na vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), alipokuwa eneo la Shipongo akifuatilia uchaguzi mdogo wa kata ya Santilya katika Jimbo hilo leo asubuhi.

Habari zinasema kuwa, Mbunge huyo alifika katika eneo hilo na kukuta uchaguzi  unaendelea salama ingawa awali kulikuwa na rabsha za hapa na pale kati ya vijana wageni katika eneo hilo na vijana wa CCM wenyeji.

Vyanzo vyetu vya uhakika, vimesema kuwa, vijana hao wageni, walipohojiwa kuwa walikuwa wakitafuta nini walidai kuwa wao ni mawakala wa Chadema ili hali mawakala walikuwa kweye vyumba vya uchaguzi.

Imeelezwa kuwa, vijana hao waitawanywa na askari polisi kisha wakapigiana simu na wenzao ambao walienda umbali wa zaidi ya mita 300 ambako walimvizia Mbunge huyo na kumjeruhi vibaya kichwani na wakati wanataka kukimbia, walikumbana na mkono wa dola huku wengine wakifanikiwa kukimbia.

Mbali na Mbunge huyo, mwingine aliyejeruhiwa ni Mchumi wa CCM wilaya hiyo, aliyefahamka kwa jina la Mwanjuguja.

Baada ya hapo, gari moja lilishikiliwa na polisi huku lingine walilokuwa nalo vijana hao lilitolewa upepo eneo hilo. Gari lililokuwa limetolewa upepo mpaka majira ya saa saba mchana lilikuwa eneo la tukio ni lenye namba za usajiliT 222 AKG Toyota Hilux.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...