Jumanne, 7 Januari 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 07.01. 2014.


 KAMANDA WAPOLISI MKOA WA MBEYA, AHMED MSANGI.

WILAYA YA CHUNYA – MAUAJI.
MNAMO TAREHE 06.01.2014 MAJIRA YA SAA 00:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA IGUNDU, KATA YA SANGAMBI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA,   MKOA WA MBEYA. PAUL S/O MWASHEMELE, MIAKA 57, MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA IGUNDU ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU  NYUMBANI KWA  NDUGU ZAKE. CHANZO NI BAADA YA KUCHOMWA KISU TUMBONI TAREHE 01.01.2014 MAJIRA YA  SAA 12:00HRS NYUMBANI KWA NGANGA S/O NYAPINI, MIAKA 48, MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA IGUNDU BAADA YA  KUMFUMANIA UGONI AKIWA NA MKE WAKE. MAREHEMU ALIENDELEA KUPATA MATIBABU KWA NDUGU ZAKE MPAKA ALIPOFARIKI DUNIA. MTUHUMIWA ALIKAMATWA TAREHE 02.01.2014 NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA SHAMBULIO DHIDI YA  MKE WAKE AITWAE TUMAIN D/O LUSAMBA, MIAKA 43, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA IGUNDU, MTUHUMIWA YUPO GEREZANI RUANDA.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO JAMII KUACHANA NA TAMAA ZA KIMWILI KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA NA BADALA YAKE WATAFUTE MPENZI MMOJA WA KUISHI NAE.
WILAYA YA MBEYA MJINI – MAUAJI.
MNAMO TAREHE 06.01.2014 MAJIRA YA SAA 06:00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA RUFAA JIJINI MBEYA, STEPHEN S/O PHILIPO,MIAKA 28,MSAFWA,MKULIMA,MKAZI WA KIJIJI CHA NSUNGWI JUU ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU. MAREHEMU  ALIPIGWA KITU KIZITO KICHWANI NA KAKA YAKE LUCAS S/O PHILIPO,MIAKA 25, MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA NSONGWI JUU TAREHE 06.01.2014 MAJIRA YA  SAA 05:10HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA NSONGWI JUU KATA YA  NSONGWI, TARAFA YA  TEMBELA WILAYA YA  MBEYA VIJIJINI. CHANZO NI UGOMVI WA MASHAMBA BAINA YA  WANANDUGU HAO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUTATUA MIGOGORO YAO YA KIFAMILIA KWA NJIA YA AMANI KWA KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO ILI KUFIKIA MUAFAKA.
WILAYA YA MBARALI – AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA BAISKELI NA            
                                           KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 06.01.2014 MAJIRA YA SAA 09:45HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA CHAMSALAKA, KATA YA CHIMALA, TARAFA YA ILONGO, BARABARA YA MBEYA/NJOMBE WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. GARI T.265 BKG AINA YA M/FUSO BASI LIKIENDESHWA NA DEREVA ZUNDA S/O ERICK, MBUNGU, MKAZI WA MBEYA LILIMGONGA MPANDA BAISKELI DAUD S/O MWAMBENE, MIAKA 53, MNDALI, MKAZI WA RUAHA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO CHA AJALI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIAMARA BAADA YA TUKIO NA KULITELEKEZA GARI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA NOTI BANDIA.
MNAMO TAREHE 06.01.2014 MAJIRA YA SAA 21:25HRS HUKO ENEO LA SOKOMATOLA, KATA YA SISIMBA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, MTU MMOJA AITWAYE MARRY D/O ABRAHAM, MIAKA 24, KYUSA, MKULIMA NA MKAZI WA SOKOMATOLA ALIKAMATWA AKIWA NA FEDHA ZIDHANIWAZO KUWA NI BANDIA NOTI 07 @ TSHS 10,000/= ZIKIWA NA THAMANI YA TSHS 70,000/=. MTUHUMIWA ALIKAMATWA BAADA YA KWENDA KWENYE KIBANDA CHA M-PESA CHA GRACE D/O STEWART, MIAKA 24, KYUSA, MFANYABIASHARA NA MKAZI WA MAJENGO NA KUTAKA KUZIHIFADHI FEDHA HIZO KWENYE SIMU YAKE. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWEMAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII HASA WAFANYABIASHARA KUWA MAKINI NA MATAPELI NA KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
[AHMED.Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...