Baadhi ya Wanawake
wa kijiji cha Masoko wakiwa wamekusanyika ili kuzungumza na mwandishi wa habari
hii, hayupo pichani.
WAJAWAZITO
wa vijiji vya Masoko na Busoka vinavyopatikana kata ya Busale wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya,
wamekuwa wakitumia usafiri wa baiskeli wakati wa kwenda kupima maendeleo ya
ujauzito katika zahanati ya Lema, ambayo iko umbali wa km sita kutoka vijiji hivyo.
Zawadi Oscar
(22) mkazi wa kijiji cha Masoko anasema
alipokuwa na ujauzito alikuwa akitumia usafiri wa baiskeli kwenda kliniki
,kutokana na zahanati ya Lema kuwa mbali na kijiji hicho.
“Nilikuwa na
ujauzito wa miezi nane, ,lakini
niliendesha baiskeli kwenda kliniki, maana afadhali kwenda huko kwa
baiskel kuliko kutembea kwa mguu, unachoka sana” anaeleza Zawadi.
Chistina
Musa mkazi wa kijiji cha Masoko anasema
usafiri wa baiskeli kwa wajawazito katika kijiji hicho ni kitu kilichozoeleka,
kwani hata yeye hutumia usafiri huo anapoenda kliniki katika zahanati ya Lema.
Anasema
haoni tatizo kuendesha baiskeli, japo alikiri kwamba baada ya kutoka zahanati
hujisikia kuchoka, lakini hana namna kwani katika kijiji anachoishi hakuna
zahanati.
Mganga mkuu
wa zahanati ya Lema, Mariam Ninde anasema ni kweli wajawazito kutoka vijiji vya
Masoko na Busoka hutumia usafiri wa baiskeli na kuutaja usafiri huo kutokuwa na
madhara kiafya kwa wajawazito.
“Mjamzito
anapoendesha baiskeli ni moja kati ya mazoezi kwa hiyo hakuna ubaya,” anaeleza
Ninde.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni