Jumatatu, 2 Desemba 2013

MADA YA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA DR.MARY MWANJELWA KWA WASOMI WA VYUO VIKUU MBEYA LEO TEREHE 1/12/2013. UKUMBI WA MTENDA SUNSET SOWETO MBEYA.


 1.    UTANGULIZI
ASILIMIA ya Wanaume katika uongozi ni kubwa kuliko ya Wanawake. Hii ni katika Nyanja zote. Na sio kwa Tanzania tu, tatizo hili ni a kidunia.
Kutokana na data za Bunge la Kidunia, Wanawake wameendelea kuwa ni ‘’minolity’’ katika Mabunge, wakiwa ni asilimia 12.7 dunia nzima(1999). Hii ni pamoja na kwamba Wanawake ndio wapiga kura walio wengi.
Asilimia kubwa Bungeni kwenye nchi za Nordic ilikuwa asilimia 38.9, na asilimia ndogo ilikuwa 3.4 katika nchi za Uarabuni. Nchi za Nordic walifanikiw kutokana na kuwathamini wanawake kiusawa katika elimu na umuhimu wao wa kupiga kura.
   2.    WANAWAKE.
Uwezo wa kuongoza hauangalii jinsia. Mtu yeyote anaweza kuongoza. karama na uwezo wa mtu.
Tanzania Wanawake hawajashirikishwa kwa asilimia ya kutosha. Mfano; Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wamekuwa ni wanaume tangu enzi na enzi hizo, na dalili ya kubadilisha hili ni finyu.
Itabidi tuliangalie kwenye katiba mpya kama Wanawake kwa maana ya kwamba tunaendelea na mchakato wa katiba mpya.
Wanawake wanaonekana kuwa sehemu yao ni kazi za nyumbani tu, kuzaa watoto, kulea familia na wanaume, hivyo hawana sauti.
  3. MWANAMKE KATIKA MAAMUZI KIDUNIA
Kidunia, maamuzi mengi yamekuwa yakifanyika kuhakikisha wanawake wanapata haki sawa na wanaume katika maamuzi ya uongozi na utawala (Platform for Action 1995 (SADC) ambayo inataka serikali iji-commit katika suala zima la usawa wa kijinsia katika ngazi zote-sheria, uwakilishi wa wananchi, Executive, taasisi binafsi, Asasi mbalimbali n.k Viongezeke.
Tanzania, kabla ya uhuru mwaka 1961 ilikuwa inatawaliwa kichifu ingawa tulitofautiana kijamii. Machifu hawa walikuwa ni wanaume.
Tanzania Wanawake ni asilimia 52 zaidi ya wanaume. Hii ina maana kwamba mchango wao katika jamii, uchumi pia ni mkubwa kulinganisha na wanaume.
Ingawa serikali na vyama vya siasa wanazungumzia umuhimu wa kuwashirikisha wanawake katika maamuzi, bado asilimia ni ndogo; haijafanya juhudi za utekelezaji wa kutosha.
Tanzania, statistics za vyama vingi(Multi parties) ilianza mwaka 1995. Kwa sasa Tanzania Mawaziri wanawake ni 9 kati ya mawaziri wanaume 30.
Wabunge wanawake sasa ni 100 kati ya wabunge 350 na hii ni kwasababu ya viti maalum.
Katiba ibara ya 46 (1)(a)(g)-Haki za wanawake; Kuheshimiwa, kuthaminiwa, kutambuliwa.
   4.    SABABU ZINAZOSABABISHA MWANAMKE KUTOPEWA NAFASI ZA KIMAAMUZI.
·       Mila na desturi, katika nchi nyingi Wanawake wanachukuliwa kama daraja la pili.
·       Structure ya kisiasa ilivyokaa na utawala wake(tunahitaji hii tuibadilishe na iingie kwenye katiba mpya) i.e viti maalum 50/50 majimboni.
·       Wanawake kutojiamini.
·       Social Attitude i.e Wanawake kutopendana, i.e wivu roho ya kwa nini?
5. MAONI NA MWELEKEO UJAO-TUFANYEJE?
·       Wanawake LAZIMA wawe ‘empowered’ wawe ‘sensitized’ wapewe mafunzo na wawekwe vizuri katika uongozi/ujuzi ili waweze kushiriki vema kama walivyo Wanaume.
Wanawake ambao wako kwenye uongozi waungane kuwapa moyo wengine na kuwasaidia, wasiwe wabinafsi ili nao wagombee nafasi mbalimbali katika level zote na kuwa kitu kimoja na sauti moja kama Wanawake. Wasijione wao zaidi kwa vile wamepata.
·       Wanawake wanaharakati wasaidie kupinga vikali mila potofu zozote za kumdidimiza mwanamke.
·       ‘Empowerment’ ya Mwanamke ianze ndani ya famiia, watoto wa kike na wa Kiume tangia umri mdogo wanavyolelewa. Hii itasaidia maana mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
·       Serikali pia iandae program maalum ya –empower Wanawake (capacity bulding).
·   Kuwepo na tume/chombo cha kushughulikia haki na masuala ya Wanawake tu.

·       Wanawake wasibaguliwe.
                                              AHSANTENI !!!!!!
 
ZAIDI SOMA MTANDAO WA MBUNGE HUYO www.marymwanjelwa.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...