Jumatano, 6 Desemba 2017

MHE MWANJELWA AUTAKA UONGOZI WA KIWANDA CHA KUSINDIKA NA KUCHAKATA CHAI CHA ITONA KUTOA AJIRA ZA UHAKIKA SIO VIBARUA

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua Jinsi uzalishaji wa Chai unavyohifadhiwa wakati alipotembelea Kiwanda cha Kusindika na Kuchaka Chai cha  Itona kilichopo Wilayani Mufindi Mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili Mkoani humo, Jana Disemba 5, 2017. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua mashamba ya Chai Kijijini Itona, Kata ya Ifwagi wakati alipotembelea Kiwanda cha Kusindika na Kuchaka Chai cha  Itona kilichopo Wilayani Mufindi Mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili Mkoani humo, Jana Disemba 5, 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na wakulima wa zao la Chai katika Kijiji cha Itona, Kata ya Ifwagi, Wilaya ya Mufindi wakati wakati wa ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Iringa . Jana Disemba 5, 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua Jinsi zao la Pareto linavyochakatwa kiwandani wakati alipotembelea Kiwanda cha kuchakata Pareto cha PCT cha Mjini Mafinga wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili Mkoani Iringa. Jana Disemba 5, 2017.

Na Mwandishi Wetu

Wamiliki wa viwanda nchini wametakiwa kutoa ajira za uhakika/mkataba kwa wafanyakazi wao ili kuongeza ufanisi wa ajira kwani asilimia kubwa ya viwanda nchini vinaajiri wafanyakazi kama vibarua jambo ambalo linaweka mashakani ajira zao.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alipotembelea Kiwanda cha Kusindika na Kuchaka Chai cha  Itona kilichopo Wilayani Mufindi Mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili Mkoani humo.

Mhe Mwanjelwa Alisema kuwa kutoa ajira zisizo na mikataba/vibarua ni sehemu ya kuwazalilisha wananchi hususani watanzania kwani wanasalia kufanya kazi kubwa huku wakiishi kwa hofu badala yake ajira hizo za mikataba zinaweza kuendelea kwa wageni na sio wazawa.

Mbele ya Mkutano wa hadhara uliofanyika Kijijini Itona, Kata ya Ifwagi Wilayani Mufindi Mhe Mwanjelwa aliwahakikishia wakulima kuboreshwa soko la zao hilo kwa kutangaza bei elekezi ya serikali hivi karibuni ili kupunguza unyonyaji unaofanywa na wamiliki wa viwanda kwa kununua malighafi hizo kwa bei ya chini ambayo kwa kiasi kikubwa haiwanufaishi wakulima.

Aliwataka wamiliki wa kiwanda cha Kusindika na Kuchaka Chai cha  Itona kuongeza nguvu katika ununuzi wa Chai kwa wakulima kwani asilimia 21 ya chai wanazonunua kwa wakulima wote wa zao hilo ni chache ukilinganisha na uzalishaji wao mkubwa.

Alisema wanapaswa kuongeza tija katika ununuzi angalau kufikia asilimia 40 ili kuwaongezea soko wakulima hao jambo litakalowanufaisha ikiwa ni pamoja na kuongeza uzalishaji ukilinganisha na uzalishaji mdogo wa sasa.

Sambamba na hayo pia aliwataka kuanzisha mashamba darasa kwa ajili ya kutoa elimu ya kilimo bora cha zao la chai kwa wakulima hao ili waweze kuwa na uzalishaji bora katika zao hilo.

Katika hatua nyingine Mhe Mwanjelwa aliwapongeza wamiliki wa kiwanda hicho cha kusindika na kuchakata chai cha Itona kwa idadi kubwa ya kuajiri wazawa ambapo zaidi ya watanzania 1500 wameajiriwa huku wageni wakiwa wanne pekee.

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa amehitimisha ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Iringa ambapo alitembelea pia kiwanda cha kuchakata Pareto cha PCT cha Mjini Mafinga na kukagua maabara ya kupima ubora wa Pareto sambamba na kuzungumza na uongozi wa kiwanda hicho ili kuboresha na kuongeza bei ya ununuzi wa zao hilo kwa wakulima.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...