Mwili
wa mwanafunzi huyo kabla ya kuzikwa mara baada ya kuagwa na ndugu,jamaa
na marafiki.Jeshi la polisi liligharamia shughuli za maziko ya
mwanafunzi huyo na hapo ndipo shitaka likaanza kuunguruma mahakamani.
HABARI KAMILI
MAHAKAMA
Kuu kanda ya Mbeya imemhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa askari wa jeshi la
polisi F 5842 DC Maduhu aliyekuwa akikabiliwa na shitaka la mauaji ya
mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) Daniel Mwakyusa.
Aidha
mahakama hiyo pia imewaaachia huru washitakiwa wengine wawili wa kesi hiyo F
7769 DC Shaban na WP 6545 DC Neema baada ya kuwakuta hawana hatia.
Hukumu
hiyo ya kesi namba 16 ya mwaka 2013 imetolewa leo(Nov 19) na jaji Rose Temba
baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili.
Awali
ilielezwa mahakamani hapo na mawakili wa serikali Archiles Mulisa akisaidiwa na
Catherine Paul kuwa washitakiwa walifanya mauaji ya kukusudia mnamo Februari 14
mwaka 2012 kinyume cha kifungu namba 196 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama
ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Kwa
mujibu wa Wakili Mulisa washitakiwa hao kwa pamoja walihusika na mauaji ya
Daniel Mwakyusa baada ya kumpiga marehemu huyo kwa kutumia silaha inayodhaniwa
kuwa ni bunduki nje ya ukumbi wa starehe ujulikanao Univesal uliopo Uyole
jijini Mbeya.
Akitoa
hukumu ya kesi hiyo,jaji Temba amesema mshitakiwa namba moja DC Maduhu
anahusika moja kwa moja na mauaji hayo kutokana na ushahidi wa kimazingira
ikiwamo yeye kuwa mtu wa mwisho kuondoka na marehemu eneo la tukio na kumpeleka
kwenye gari,risasi tatu kupungua kwenye bunduki yake na pia kuwa mtu wa mwisho
kurejesha silaha kituoni.
Credit;lyamba lya mfipa blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni