Vunja ukimya wa watoto njiti wa Tanzania!
Paza sauti yako kwa ajili yao!
Zaidi ya watoto 210,000 huzaliwa njiti Tanzania kila mwaka
Ni sawa na mtoto 1 kati ya kila watoto 9 wanaozaliwa hai Tanzania ni njiti
Watoto wachanga 9,400 hufariki kila mwaka kutokana na matatizo ya kuzaliwa njiti
Idadi hiyo ni sawa na karibu robo ya vifo vyote vya watoto wachanga

Habari njema ni kuwa kuna njia rahisi zinazoweza kusaidia kuwaokoa wengi!
- matumizi ya njia za uzazi wa mpango;
- uanzishaji mapema wa unyonyeshaji na unyonyeshaji maziwa ya mama pekee;
- kuhakikisha watoto wanapewa joto la mwili hasa ngozi kwa mgozi baina ya mzazi na mtoto mchanga (njia hii inajulikana pia kama kangaroo mothercare);
- uangalizi sahihi baada ya kuzaliwa, kujifungulia kwenye vituo vya afya na kuhakikisha mtoto anachunguzwa na wataalamu na kupata uangalizi sahihi baada ya kuzaliwa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni