Jumatatu, 24 Novemba 2014
MAGAZETINI LEO NOVEMBA 2014
NIPASHE
Chama cha Wananchi CUF kimemtaka Waziri mkuu Mizengo Pinda ajiuzulu kwa kupotosha umma kuhusu kashfa ya fedha zaidi ya bilioni300 zilizochotwa katika akaunti ya Escrow ndani ya benki kuu ya Tanzania ‘BoT’.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa CUF Ibrahim Lipumba wakati akitoa taarifa kuhusu sakata hilo lililotokea na mkataba wa kuuziana umeme wa dharura kati ya Tanesco na IPTL.
Alisema kuwa Waziri mkuu ndiye kiongozi wa Serikali ambaye Mei mwaka huu aliupotosha umma na kudai fedha za Escrow zilizoibiwa si za wananchi bali ni za wanahisa.
“Tunamtaka Waziri mkuu awajibike kwa kitendo cha kupotosha umma,kama asipojiuzulu basi afukuzwe kazi mara moja,amekua akitafuta visingizio vya kufuta mjadala na taarifa ya CAG,”Alisema Lipumba.
NIPASHE
Jeshi la Zimamoto na uokoaji nchini limesema ukosefu wa vitendeakazi,rasilimali watu na ufinyu wa fedha wanazokusanya kutoka kwa wananchi ni changamoto zinazokwamisha jeshi hilo kushindwa kutoa huduma za uhakika kwa jamii pindi majanga ya moto yanapotokea.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano kwa umma wa jeshi hilo Miraji Kilolo alisema wanapokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kutokana na kutoridhishwana huduma zetu,lakini sisi tumejipanga kumaliza changamoto zote na kutoa huduma bora kwa jamii hasa katika majanga ya moto.
Alisema kuwa magari makubwa ya kuzimia moto yaliyopo hivi sasa hayaendani na mabadiliko ya kukua kwa miji nchini kutokana na hivu sasa magorofa marefu yanayojengwana jeshi hilo hayana vifaa vya kisasavya kuzimia moto.
Alisema jeshi hilo lmefanya mazungumzo na Wenyeviti wa Serikali za mitaa wote kujenga visima vya maji katika mitaa yao ili janga lolote la moto likitokea wapate huduma kwa haraka.
NIPASHE
Ripoti ya uchunguzi wa kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya IPTL ya uchotwaji wa shilingi bilioni306 kwenye akaunti ya Tegeta Escrowiliyopobenki kuu ya Tanzania BOT zimeibwa na kuzua mambo.
Kufuatiatukio hilo Jeshi la Polisi Dodoma limewatia mbaroni vijan wawili wanaotuhumiwa kusambaza mitaani ripoti feki ya ukaguzi wa hesabu za fedha hizo uliofanywa na CAG kuhusiana na kashfa hiyo.
Vijana hao ambao wanadaiwa kuwa ni baadhi ya watu waliomo katika kikosi cha Waziri mmoja kilichongia mijini Dodoma,wanadaiwa kusambaza ripoti hiyo feki kwa kutumwa na Waziri huyo.
Kamanda wa Polisi DodomaDavis Misime alithibitisha kukamatwa kwa vijana hao tangu juzi na kusema kuwa walipohojiwa walikiri kupewa nyaraka hizo na mmoja wa Wabunge,ambaye hata hivyo alikataa kumtaja kwa sababu za kiuchunguzi.
UHURU
Watu sita wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi iliyoambatana na mvua kubwa katika chuo cha Mifugo na Uvuvi katika Wilaya ya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma.
Kamanda wa Polisi Mkoani humo Mihayo Msekele alisema tukio hilo lilitokea juzi usiku ambapo mvua kubwa ilinyesha ikiambatana na mvua kubwa ambapo wanachuo wawili na wapishi wanne waliokua katika vibanda wakikwepa mvua walifariki baad aya radi kuwapiga.
“Wanafunzi walikua wanakula katika vibanda vyao huku waiikinga na mvua na ndiporadi hiyo ilipiga na sita kati yao walifariki papo hapo na wengine wawili kujeruhiwa na sasa wapokatika ,hospitali ya Wilaya wakipatiwa matibabu,”alisema Mihayo.
Mihayo alisema kulitokea mwanga mkali wakati tukio hilo likitokea na sauti kubwa ambayo ilisababisha nguzo za vibanda hivyo kuchanikachanika huku wanafunzi wengine wakikimbia.
UHURU
Utupaji watoto wachanga katika mto Ngarenaro Mkoani Arusha umekithiri hali inayohatarisha maisha ya wkaazi wa maeneo hayo ambayo hutumia maji ya mtu huo kwa shughuli zao za kila siku.
Kutokana na hilo wakazi wa eneo hilo hulazimika kufanya usafi mara kwa mara na kulalamikia kukuta miiili ya vichanga ambayo hutupwa maeneo hayo kila wakati.
Baadhi ya wakazi hao walisema mto huo ambao chanzo chake kinatoka katika Mlima Meru ni muhimu kwao kutokana na maji yake kutumika kwa matumizi ya nyumbani na hata umwagiliaji wa mboga mboga.
“Unaweza kwenda kuteka maji ukakutana na mabaki ya miiili ya watoto huku wengine wakitupa taka kwa kukwepa kulipa ushuruwa takataka ambao ni shilingi 1000 kwa Halmashauri ya jiji.
MTANZANIA
Chama cha wamiliki wa Mabasi Tanzania TABOA kinakusudia kusitisha huduma za usafiri wa mabasi nchi nzima muda wowote kuanzia sasa,endapo madai yao ya msingi hayatashughulikiwa na mamlaka ya uthibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini Sumatra.
Uamuzi wa kufikiwa kwa mgomo huo ambao unatarajiwa kusababisha tatizo la usafiri wakati huu wa kuelekea katika sikukuu za mwisho wa mwaka,ulifikishwa juzi katika mkutano mkuu wa TABOA uliofanyika jijini Dar es salaam.
Mweka Hazina wa Chama hicho Issa Nkya alisema mgomo huo una lengo la kuishinikiza SUMATRA ili isikilize kero zao ambazo zimedumu kwa muda mrefu sasa.
Alisema kitendo cha Sumatra kugoma kuhudhuria mkutano mkuu waChama hicho unaonyesha wazi namna ambavyo haiko tayari kumaliza matatizo na wamiliki wa mabasi.
Alisema katika mkutano huo wamiliki wa mabasi wamelitaka Jeshi la Polisi na Sumatra kuacha kufungia makampuni pindi basi mojawapo linapopata ajali.
MWANANCHI
Serkali imeunda kamati ya watu10 kutoka kada tofauti wakiwamo viongozi wa dini ambao watapea jukumu la kufanya kazi ya usuluhishi kwenye vijiji vyenye migogoro baina ya wakulima na wafugaji Wilayani Kiteto Mkoani M anyara.
Waziri mkuu Mizengo Pinda alisema hayo jana wkaati akiwasilisha salamu za Serikali kwenye ibada ya kumweka wakfu Askofu wa sita wa Dayosisi ya Central Tanganyika ya kanisa la Anglikana Dk Dickson Chilongani lililofanyika kwenye kanisa kuu mjini Dodoma.
Alisema hali ya Kiteto si shwari na inahitajika ufumbuzi ili kuzuia mapigano na migogoro inayoendelea kwa sasa na kusema wameteua kamati maalum itakayokwenda kufanya usuluishi baina ya vijiji hivyo.
“Tunataka kutumia Kiteto kama mradi wa majaribio kwenye suala la kutafuta amani kwenye maeneo yake,watu wanauana kwa sababu ya ha sira,ni hasira ga ni hiyo inayokufanya mpaka uweze kuta roho ya mwenzako huu ni unyama lazima tusimame kidete”alisema Pinda.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni