Jumatano, 1 Oktoba 2014

· WATU WANNE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KATIKA TUKIO LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA WILAYA YA MOMBA.






JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE WANATUHUMIWA KUHUSIKA KATIKA TUKIO LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA (PANGA) LILILOTOKEA MNAMO TAREHE 30.09.2014 MAJIRA YA SAA 22:40 USIKU HUKO KATIKA MTAA WA KALOLENI, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.

INADAIWA KUWA, MFANYABIASHARA MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EDDY MWILA (29) MKAZI WA MIGOMBANI – TUNDUMA AKIWA NA MWENZAKE AITWAYE SHIDA MWAMPASHI (28) MKAZI WA MIGOMBANI WAKIWA WANATOKA KATIKA SHUGHULI ZAO ZA KUBADILISHA FEDHA, GHAFLA WALIPOFIKA MTAA WA KALOLENI WALIVAMIWA NA KUNDI LA WATU AMBAO IDADI YAO BADO KUFAHAMIKA NA KUMNYANG’ANYA EDDY MWILA KIASI CHA FEDHA TASLIMU TSHS. 1,000,000/= PAMOJA NA Z.K 700,000/=.

WAKATI WA TUKIO HILO, SHIDA MWAMPASHI ALIJERUHIWA KICHWANI KWA KUKATWA NA PANGA ALIPOKUWA AKIMSAIDIA MWENZAKE. BAADA YA TUKIO HILO, ASKARI WALIOKUWA DORIA WALIPATA TAARIFA NA KUENDESHA MSAKO MKALI NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MUSSA SHABANI (27) MKAZI WA CHIANGA NCHINI ZAMBIA AKIWA NA PANGA LENYE DAMU NA BAADA YA MAHOJIANO ALIKIRI KUHUSIKA NA UNYANG’ANYI HUO.

MTUHUMIWA HUYO ALIWATAJA WENZAKE WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILO AMBAO NI 1. IDDY MWAMKINGA (32) MKAZI WA MPAKANI 2. MUSSA MBUGHI (23) MKAZI WA MWAKA – TUNDUMA NA 3. GEORGE MGODE (22) MKAZI WA KILIMAHEWA.

AIDHA, MSAKO MKALI UNAENDELEA KUWATAFUTA WATUHUMIWA WENGINE WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILO.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...