Jumamosi, 27 Septemba 2014

ZITAMBUE FAIDA ZA KUMCHA MUNGU

Kumcha Bwana au Mungu maandiko matakatifu ktk zaburi128 yanaeleza kuwa ‘’ heri kila mtu amchae Bwana, Aendaye ktk njia yake’’ HERI: Maana yake ni Baraka, mafanikio, bahati njema, furaha na mambo yanayofanana na hayo.

Njia ya Bwana imenyoooka na njia ya Bwana ni UTAKATIFU; KTK ZAB77:13 Ee Mungu njia yako I katika utakatifu. UTAKATIFU maana yake ni kutengwa na Dunia na mataifa yaani kutengwa na watu wasiomjua Mungu kimwenendo na kitabia kwa ujumla.

Kutengwa na dunia ni kuacha njia za wasiomjua Kristo yaani, kujitakasa na kufikiri kama Kristo, kuwaza kama Kristo, kunena kama Kristo . Hayo yooote ni jumla ya kuwa ndani ya Kristo hivyo anayenena kwako si wewe bali yule aliye ndani yako.

Utakatifu unalindwa, utakatifu unatunzwa. Zaburi 128:1 "Heri kila mtu amchaye Bwana ina maana mtu anaye mcha Bwana ni mtakatifu, ni mtu mwenye Baraka, mafanikio tele, na mengine mengi yanayoonekana kwake. Kumcha Bwana si kwenda kanisani kila siku LA HASHA, NI ZAIDI YA HAPO. Utakatifu ni jumla ya utakaso wa nia zetu ndani na nje ya nafsi,roho na Miili yetu.
Kumcha Bwana ni kuambatana na Mungu hasa ktk Mioyo yetu. Pia huo ni Mwanzo wa Baraka njema na mafanikio bora. Mith1:7.

Utakatifu Ni hali ya moyo uliomshiba Bwana na kuchukia njia za uovu ambazo ni chukizo kwa Mungu. Kiburi, majivuno, ukaidi, unafiki, uongo na mengine yanayofanana na hayo. Ni kutahiriwa kwa Moyo, kuondoa moyo wa jiwe. Ili umpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote akili zako zote lazima ufanyiwe tohara ya moyo. Ni kumpenda Mungu kwa dhati, kumhofu Mungu, kujitoa kwake kwa vyote ulivyo navyo, ni kujikana na kujitwika msalaba wa Yesu. Mtu huyu Mungu ni tumaini lake, nyakati zote Mungu ni msaaada kwake, Mungu kwake ni kimbilio na nguvu na ni chazo za meema yote. Kumb8:18 Mungu ndiye atoaye utajiri.

Mtakatifu huwekewa chuki ya dhambi yeyote, hawezi kukaa nayo dhambi hutubu mara tu apatapo mkasa. Hawezi kusema atatubu jioni au jumapili wakati wa ibada ni pale pale anajitakasa. Ameifia dhambi ambayo ni chukizo kwake na kwa Mungu. Hana vitu vya sirisiri kama vimeseji vyenye password ambavyo hataki mme/mke avione lakini Mungu anaviona au akiwa peke yake mahali au amesafili nje ya watu wanaomfahamu anabaki mtakatifu. Kwake mtakatifu matangazo ya kuja kwa Yesu tar fulani hayamtishi, wala hayamhusu kwani yuko tayari wakati wote. Awe sirini anajua Mungu anamuona.

Mtakatifu wa Mungu amekirimiwa Utajiri wa rohoni na mwilini. Mithali8:15-18 15 Kwa msaada wangu wafalme hutawala na watawala hutunga sheria zilizo za haki,16kwa msaada wangu wakuu hutawala,na wenye vyeo wote watawalao dunia. 17 Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. 18Utajiri na heshima viko kwangu, utajiri udumuo na mafanikio.

Mungu anakupa utajiri wa Mwilini na rohoni au kwa mapenzi yake mwenyewe akakupa kimojawapo yaani utajiri wa rohoni na utajiri wa mwilini kwa kusudi lake mwenyewe. Maana yeye ndiye achunguzaye mioyo na viuno na kumpa kila mmoja kiasi cha matunda ya njia zake au matendo yake.
Tambua kuwa yeye ndiye chanzo cha:

o Nguvu ulizonazo
o Ufahamu, akili njema
o Busara ulizo nazo na hata ufunuo wa namna yeyote ktk neno
o Uwezo, vipawa, karama, kazi, utumishi, wa namna yeyote.
o Uwezo wa kitawala

TAFUTENI KUWA NA AMANI IPITAYO AKILI ZOTE------, NA UTAKATIFU HUO AMBAO-------


FAIDA ZA KUMCHA BWANA
o Unabarikiwa na unapata upendeleo toka kwa Mungu.
o Unahifadhiwa wewe na nyumba yako, yaani mwili wako ambao ni hekalu la Mungu
o Mungu ana fanya favor kwa jamaa yako yaani anafanya mambo ya kiupendeleo kwa familia yako, jamaa yako rafiki zako,kwa taifa yako, kanisa, mali zako na vyote huweka ulinzi wa kipekeee
o Mali ktk namna ya kimwili kama vile watoto, nyumba, magari, mashamba, vyeo nk
o Mali za rohoni kama vipawa, karama hekima, ufahamu nk.
o Kifo cha mcha Mungu kina dhamani sana mbele za Mungu Zab116:15
o Mcha Mungu mambo yake mema yanaonekana/husomeka
o Utaondoka duniani umemaliza kazi au kusudi ambalo Mungu amekuitia duniani na mwendo wako utaumaliza salaama.

  • Kumaliza mwendo ni kumaliza ule mda wako kiutumishi lakini unaendelea kuishi kwa ajili ya watu kujifunza kwako, kuwaachia wosia mbalimbali wengine
  • Kumaliza kazi ni kumaliza kazi ulizokabidhiwa na Mungu uzifanye
o Mcha Mungu anaufahamu wa KiMungu, hekima ya kiMungu, maarifa ya kiMungu
o Mungu humfunulia Mambo ya sirini ya kimungu, na Busara za Kimungu
Hivyo basi ipo fursa ya kila muamini kumcha Mungu na kuibadilisha jamii nzima ikawa sawa na maagizo ya Mungu wetu Mkuu. Hauhitaji kumuomba Mungu akufanye kama wahubiri/manabii wakubwa sana hapa duniani maana hata wao kunagharama walizozitumia. Bali unahitaji kupiga bidii kujitakasa kila siku. Kuulinda utakatifu ni kazi sana, ila kuokoka ni one time action. Ndio maana siku ile wengi watasema tulitoa pepo kwa jina lako, tuliombewa wagonjwa, tulikuwa waimbaji, lakini Mungu hatawatambua maana hawakuulinda utakatifu wao.

BARIKIWA


By Anthony

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...